Makonda, onesha Vyeti vyako halali wanaokutuhumu waaibike

Ni tuhuma sio hukumu. Ni kama walioitwa kwa kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya. Wengi zilikuwa tuhuma za vijiweni tu kama hizi za vyeti lakini polisi wetu walichukua hatua ya kuchunguza! Huoni mambo hayo yanavyofanana?
Tuhuma zilifika mamlakani wakaamua kuwaita kwa mahojiano kwanini na hizi gwajima asizipeleke mahakamani anategemea kanisa?
 
Naona ishu ya katazo la Mkubwa inataka kututoa kwenye agenda kuu. BASHITE tunataka vyeti mezani. Vyetiiiiiiiiii
 
ham
Naona ishu ya katazo la Mkubwa inataka kututoa kwenye agenda kuu. BASHITE tunataka vyeti mezani. Vyetiiiiiiiiii
na vyetii na kaka hataki kumtoa yaani sahizi wakitoa matamko yao wanaonekana kama soud brown tu shilawaduuu ni wa kupuuzwa wote wawili
 
Katika ishu ambazo hazitakaa zife ni hii ya Daudi Bashite. Beleave me not.
 
Kwa muda kuna watu wamejitokeza hadharani kudai vyeti vya watu wengine huku vya kwao wameficha nyumbani.!

Hii imetokea baada ya wauza madawa ya kulevya kubanwa kweli kweli na hawana pa kutokea awamu hii.

Wanafanya kila njia ili Paul Makonda atolewe Dar ili wapate nafasi ya kuuza madawa yao bila shida na hatimae kuuwa Vijana wetu wengi kwa kadiri wawezavyo huku wao wakitajirika kweli kweli.

Cheti cha mtu ni Siri yake na hakuna wa kumlazimisha akiweke hadharani kwenye mitandao.
Kama unahitaji cheti cha mtu fulani unatakiwa umfuate huyo mtu nyumbani kwake.

Kuanzia sasa ukitaka cheti cha mtu fulani kiwekwe mtandaoni, Anza kuweka cheti chako kwanza huko mitandaoni, baada ndio udai na wengine waweke vyeti vyao.

Kudai cheti cha mtu fulani huku cha kwako umeficha uvunguni ni kupungukiwa akili kabisa.

Sasa ni kampeni ya weka cheti chako hadharani alafu dai cheti cha mwingine hadharani.
 
Wakuu poleni na weekend kavu,
Niende kwenye mada moja kwa moja.Nakumbuka hotuba ya Waziri mkuu aliyelazimishwa kustaafu na mwishowe akakkatwa na hatimaye akaenda kununua Chadema ili agombee uraisi kwa tiket ya ukawa.sikumbuki maneno yote ila kuna sehemu katika hotuba ile alisema,Namnukuu" Naona tatizo ni uwaziri mkuu,naona tatizo ni uwaziri mkuu".Naanza kupata fikra mbaya kwamba hii vita ya vyeti vya Bashite sio tatizo,tatizo ni "DONA".kuna ukakasi ndani ya jambo hili,watu wameacha kufocus kwenye "DONA"wanahangaika na vyeti.mimi sio kada wala mfuasi wa chama chochote hapa TZ,nimemaliza Advanced level 1993 mnaweza kukadiria umri wangu,sijawahi kupiga kura hata mara moja,lakini naona kuna watu wanatuzuga sana tuelekee kwenye vyeti,napata hofu wanahusika na biashara hii ya "SEMBE'.Najiuliza tu peke yangu,sasa hivi" Bashite" akifukuzwa,au akijiondokea tutarudi kujadili "SEMBE" au tutatafuta mtu mwingine ambaye hana vyeti au ana vya uwongo?kwa nn tunafanywa wajinga na watu wachache?badala ya kujadili hoja zote mbili ya" DONA" na "BASHITE",tumevurugwa tunajadili upande mmoja ambao hauna madhara.Tuamnkeni jamani tusipelekwe na Upepo.Ingekuwa ni Upinzani umeanzisha hii vita ya "DONA"afu wana Lumumba wanazungumzia vyeti vya Hamad Rashid watu wangetokwa Povu sana na kusema tunapoteza muda ku discuss petty issues!Sisemi Bashite yupo sawa ila tujadili vyote viwili tu!Tunatumia nguvu nyingi kuzima swala la "SEMBE"badala ya kuhangaikana "Bashite".Au kwa vile Freemasson alitajwa?
 
Kushambulia studio na kulazimisha kurushwa habari ya hawara wa Gwajima
haisaidii,
Nafikiri kinachotakiwa ni kubeba vyeti kuanzia Primary school mpaka chuo
ambavyo vina jina moja tu, nafikiri linafahamika!
Hapo kelele zote zitakuwa zimeisha.
 
Nachokiona kati ya jpm na RC ni vita kati ya upinzani na serikali ya jpm hicho ndicho kinampa kiburi mhe. Rc maana mkuu wa nchi hawezi kuchukua hatua japokuwa rc kaharibu ili mradi tuu awakomoe wapinzani wake
 
Kweli Makonda yupo juu, kla mtu usingizi hapati kwa ajili yake 😱

Kwa kweli hatupati usingizi, lakini si kwa ajili yake bali ni kwa ajili ya nchi yetu. Na wengi wetu tunamkumbuka hayati baba wa taifa. "I cannot let my country go to the dogs."

Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Anayesema uongo hata Kama kwa kujifanya hajui ukweli ulio machoni kwake, huyo ni mpenzi wa nani?
 
See no evil, hear no evil, speak no evil! Sio cheti tu, lakini ndio hicho mlichoamua kukishikia bango, mengine yote yanayosemwa hamsikii.

Kwanza kabisa Mimi sio mwanasiasa, siyo mwana harakati. Mimi ni mtanzania mzalendo. Nachukia rushwa kwa nguvu zangu zote, nachukia biashara ya madawa ya kulevya, naamini kupata ujira wangu kwa haki na sipendi kudhulumu. Sipendi udanganyifu wa aina yeyote.

Turudi kwenye mada. Makonda alivyoanza vita vya madawa ya kulevya Mimi binafsi niliona Ina walakini kwa sababu moja kuu unampa mfanyabiashara hiyo siku kadhaa, hao watu dakika tano nyingi kuondoa vidhibiti. Kweli kuna kosa la jinai unaloweza kuprosecute based on hearsay? Kweli unaposema meli ya drugs iko njiani ili iweje? Unataka mwenye nayo asepe asikamatwe? Kingine ni kumtuhumu mtu hadharani wakati huna hata chembe ya ushahidi.

Kingine mali anazotuhumiwa kuwa nazo zimethaminishwa, amezitoa wapi? Mbona nyingine (magari) Zina majina ya aliowashutumu biashara ya kulevya? Mbona ana mawasiliano na watu ambao wako involved na biashara hiyo?

Kingine kutukana watu walio chini yake, kuchongea wenzake kwenye mastage. Kikubwa ni yeye kujifananisha na Mungu. I don't really care on a religious point of view, inachonionyesha huyu sio mnyenyekevu, hata kwa Mungu ambaye anajifanya anamwamini sana na tena inadhihirisha wazi unafiki wake.

Nyie zibeni masikio, funikeni macho na midomo yenu ifungeni kabisa, msikemee uovu kabisa.

Sasa tunataka kuanza na vyeti na ku address yaliyotokana ni hiyo fraud.

Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…