Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 24,523
- 30,084
Makonda! Hawa wanayo haki kuhoji kuhusu Rais wao siyo mwenyekiti wa CCM wala siyo Samia, ni Rais tu. Tatizo lako Paulo ni kudhani Rais ni mali ya CCM watu wengine hawana haki ya kuhoji! Wanahoji kwa sababu wanashida naye za msingi.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema baadhi ya wanaharakati wamekuwa wakitoa hoja zisizo na msingi kuhusu Rais Samia Suluhu Hassan kutoonekana hadharani, akisisitiza kuwa watumishi wa serikali ni wawakilishi wa Rais katika kutekeleza majukumu yake.
"Hasa nchi imekuwa na wanasiasa wanao- hovyo kabisa. Yani hujui jinsia yao ni jinsia gani. Wana uchafu hovyo. Kila siku wanazusha mambo ya kijinga. Mheshimiwa Rais amefiwa na mume wake, yupo kwenye majonzi, kuna mjinga huko anaandika "oh, haonekani", "eh, toeni zimebaki siku ngapi". Kweli wewe maisha unayapanga? Wanampangia Rais lini atoke nje, lini asitoke"
Swala la eda ni la kiimani na sisi serikali haina imani za kudini, siku tukipata Rais mlokole sijui mambo yatakuaje siku za Jumamosi na mikesha yao ya kiimani!
Makonda rais ni mali ya watanzania ila Samia ni mali ya familia yake na CCM hivyo itafutwe njia ya kumrudisha ofisini anapohitajika kikazi na tujue mtumishi wa umma akifiwa anapumzika kwa miezi mingapi.