Makonda: Sikutegemea kwamba leo ndo itakuwa ni siku yangu ya mwisho kuaga, namshukru sana Rais Samia

Makonda: Sikutegemea kwamba leo ndo itakuwa ni siku yangu ya mwisho kuaga, namshukru sana Rais Samia

Makonda anajua kucheza ba akili za viongozi vibaya mno
 
Wakuu,

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukuru Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini mara mbili ikiwemo kumpa nafasi ya kuwa Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na baadaye Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo Makonda amesema licha ya baadhi ya Watu kumkandamiza kisa mapambano yake ya kupinga dawa za kulevya na ushoga lakini bado haikumzuia Rais Samia kumuamini na kumpa fursa.

Akiongea leo June 24, 2025, kwenye Jukwaa la Wanawake lililofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano (AICC) Jijini Arusha, Makonda amesema

Soma Pia: UTEUZI: Balozi Simon Sirro ateuliwa kuwa RC wa Kigoma, Kenan Kihongosi kuwa RC wa Arusha. TRC yapata Mkurugenzi Mpya

“Mh. Mgeni rasmi Balozi (Dkt. Nchimbi), naomba kwa unyenyekevu mkubwa unifikishie salamu kwa Rais Samia kwa kuniamini mara mbili ndani ya utumishi wake wa urais tangu mwaka 2021, kuniteua kuwa Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, sikutarajia leo itakuwa hotuba yangu ya kuaga”


Uage vizuri,Kuna Kila dalili ukamfuata JPM
 
Back
Top Bottom