Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda, amekemea vikali vitendo vya baadhi ya viongozi na wadau wa michezo kutumia vitisho vya kisheria dhidi ya wananchi na wanahabari wanaokosoa muundo na ubora wa jezi za timu ya taifa.
Makonda amesisitiza kuwa Katiba ya Nchi inampa kila mwananchi uhuru wa kutoa maoni na kujieleza, hivyo si jambo la busara kuwatisha au kuwapeleka mahakamani Watanzania wanaosema ukweli pale jezi ya nchi yao inapokuwa mbaya au isiyokidhi viwango.