Makonda: Tukisema jezi ni mbaya mnatupeleka Mahakamani? Hatuna haki ya kutoa maoni?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda, amekemea vikali vitendo vya baadhi ya viongozi na wadau wa michezo kutumia vitisho vya kisheria dhidi ya wananchi na wanahabari wanaokosoa muundo na ubora wa jezi za timu ya taifa.

Makonda amesisitiza kuwa Katiba ya Nchi inampa kila mwananchi uhuru wa kutoa maoni na kujieleza, hivyo si jambo la busara kuwatisha au kuwapeleka mahakamani Watanzania wanaosema ukweli pale jezi ya nchi yao inapokuwa mbaya au isiyokidhi viwango.


Your browser is not able to display this video.

​
 
Angalau mh unapelekwa mahakamani
 
Hayo ya Makonda hayakuwa maoni. Yalikuwa maelekezo maana alisema ataunda tume ya kuchunguza mkataba. Sasa ni maoni gani hayo yanayo husisha uchunguzi wa Mkataba?
Hahaha sasa kilipobuma anafanyaje nani anataka kukaa kizimbani aanze kufurushwa miamala yake ya kibenki aliyoingiziwa bila watu kujua na masiri yake kibao yamwagwe hadharani nani anataka?
 
Sasa kumbe na yeye anataka uhuru wa kutoa maoni mbona wenzao wakitoa hayo maoni wanawateka na kuwaua ?
 
Naye leo analilia na kutaka haki ya kutoa maoni ya kusema "jezi ni mbaya!!!??"

Kumbe wengine wanaposema "serikali yao ya CCM chini ya Samia Suluhu Hassan ni haramu, haifai na imeshindwa" wanakuwa wanahukumu au nao wanakuwa wanatoa maoni vilevile..?

Mbona mnawateka, kuwatesa, kuwafira, kuwalawiti, kuwafungulia makesi mabaya ya ugaidi na uhaini na wengine kuwaua na kupoteza maiti zao..??

Nenda mahakamani kajitetee huko...
 
Shida ilipoanzisha ni pale aliposikia wanasema tunakupeleka mahakamani na yeye kwa kuangalia in fact anajiona amekosea ila muungwana huchutama ukivuliwa nguo sema DAB kavuliwa nguo yeye kakubari kukaa uchi hataki kuchuntama acha watu waangalie nyeti zilivyo
 
Mbona anawazungumzia na wengine ambao hawakusema kitu.Yeye hakuzungumza kama mtanzania wa kawaida asiye na dhamana alizungumza kwa nafasi yake,akaenda mbali zaidi kuhoji naibu waziri kushirikishwa.Intention yake ilikuwa na bad motive na kudharirisha,na kuharibu biashara,kama wangesema wanunuzi wa jezi sawa lakini yeye alizungumza kama kiongozi.Je hukufahamu taratibu alizopaswa kufuata kama alitaka kutoa maoni na pia kwa nini hakutaka kuwasiliana na Sandland kwanza?
 
Mbona Ben Saanane alivyotoa maoni yake kuhoji Phd ya JPM mbona alimteka na kwenda kumuua? Mbona TAL alipotoa maoni yake kuhusu kushitakiwa MIGA mbona aliengenieer kupigwa risasi?
 
Kwani Tanzania Kuna uhuru wa kutoa maoni? Mbona wenzenu wakitoa maoni mnawafungulia kesi za uhaini? Atupishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…