Tutawapa kila kitu maana yake nini?"Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walitegemea tutawaletea Polisi na tutawapiga mabomu, nimwambie kaka yangu Freeman Mbowe awamu hii imebadilika, tutawapa kila kitu lakini kura hamtapata.
Wako bararani wanatembea, wanazurura wanaona raha na kwa kuwa wengine ni wagonjwa tumewapelekea magari ya wagonjwa Ambulance ili kutoa msaada itakapotokea dharura." - Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda akiwa Makuyuni Monduli Arusha
Ameongeza kuwa "Wakati wao wanaandamana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekea nchini Indonesia kwenye vikao vya Kimataifa kutafuta fedha za miradi ya maendeleo."
Source - CloudsTv
Mimi kwa ufahamu wangu haki wanayopata Chadema na vyama vingine vyote ikiwemo CCM vinatokana na katiba, sheria,kanuni na miongozo tuliojiwekea wpte kama nchi.
Sasa huyu bwana division 0 aliekosa hata D mbili haya kayatoa wapi?...ila CCM safari hii mmepatikana