Pre GE2025 Makonda: Vijana achaneni na siasa, hailipi. Pesa ndiyo inalipa

Pre GE2025 Makonda: Vijana achaneni na siasa, hailipi. Pesa ndiyo inalipa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa vijana kuachana na siasa kwakuwa siasa hailipi badala yake wafikirie kuhusu kutengeneza pesa, maana pesa ndio inalipa na ukiikosa hata kwenye uchaguzi huchaguliwi!

Pale ambako mwanasiasa anakwambia siasa hailipi! Kama hailipi mbona haachi?

"Vijana wengi wanawaza siasa, achana na siasa, siasa hailipi, pesa ndiyo inalipa. Point yangu ni kwamba lazima tuwe na mikakati ya kufikiri namna ya kujenga uchumi badala ya kujadili siasa inayojadili majina ya watu na mtu.

"Ukiwa hauna pesa huna pointi. Ukiwa hauna pes ahata kwenye uchaguzi huchaguliwi kama unabisha niulize mimi! Nilikuwa na uwezo lakini sikuwa na pesa wakati nagombea Umoja wa Vijana nikaachwa.

"Kwahiyo niwaombe tuachaneni na siasa Najua maneno haya kuna wengine watayatumia kutengeneza hoja zingine lakini potelea mbali, tuachane na siasa, narudia tena siasa haina mpango!"
 
Sina uhakika kama Makonda amewahi kufanya kazi nje ya Siasa

Tangu nimemfahamu akiwa UVCCM baadaye Mkuu wa Wilaya, Mkoa, mwenezi wa Chama na Sasa ni Mkuu wa Mkoa Arusha.

Ambapo Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Mkuu wa Mkoa ni Kamisaa wa Chama.

Hivyo iwapo Bwana Makonda atakuwa anamiliki nyumba, basi hiyo nyumba imetokana na Fedha za Siasa.

Siasa ndiyo sehemu imewatajirisha Vijana Kwa Wazee wengi Nchi hii
Hivyo Mhe. Makonda ache Vijana wakajiajiri kwenye Siasa maana ajira zenyewe hazipo kwasasa
 
Akamuulize Ally hapi!akajifanyamkulima was nyanya mara akaanza kujirekodi akikimbia mchaka mchaka huku akiimba nyimbo za kuwananga mafisadi,Hadi mama akamkumbuka juzi nimemuona live akirudia mara tati eti "Nchi IPO salama mikononi mwa samiah"kana kwamba haikua salama kabla!!

Makonda siasa inalipa ndugu ndio maana kabudi lilimtoka kubwa"nilitolewa jalalani"kumbe udsm faculty ya Law no jalalani !!!

Weka mbali na watoto!

Dola iliamua siasa ndio iwe iazi inayolipa Sana kuliko usomi wowote ule katika nchi hii!!

Ndio maana vijana wanawekeza kwenye uchawa,na wasomi tulio kazini tunajiona kama panzi mbele ya wanasiasa wateule was rais na wabunge mawaziri hata kama ni std seven!!
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa vijana kuachana na siasa kwakuwa siasa hailipi badala yake wafikirie kuhusu kutengeneza pesa, maana pesa ndio inalipa na ukiikosa hata kwenye uchaguzi huchaguliwi!

Pale ambako mwanasiasa anakwambia siasa hailipi! Kama hailipi mbona haachi?

"Vijana wengi wanawaza siasa, achana na siasa, siasa hailipi, pesa ndiyo inalipa. Point yangu ni kwamba lazima tuwe na mikakati ya kufikiri namna ya kujenga uchumi badala ya kujadili siasa inayojadili majina ya watu na mtu.

"Ukiwa hauna pesa huna pointi. Ukiwa hauna pes ahata kwenye uchaguzi huchaguliwi kama unabisha niulize mimi! Nilikuwa na uwezo lakini sikuwa na pesa wakati nagombea Umoja wa Vijana nikaachwa.

"Kwahiyo niwaombe tuachaneni na siasa Najua maneno haya kuna wengine watayatumia kutengeneza hoja zingine lakini potelea mbali, tuachane na siasa, narudia tena siasa haina mpango!"
Ukisikia anasema hivyo kuwa watu waachane na siasa anamaanisha watu wasiiishabikie cdm, maana kuishabikia cdm kwake ndio kuishabikia siasa.
 
Back
Top Bottom