Makonda wa mabasi ya mikoani, kwanini mnahatarisha maisha yenu kwa kusimama karibu na kioo cha gari?

Makonda wa mabasi ya mikoani, kwanini mnahatarisha maisha yenu kwa kusimama karibu na kioo cha gari?

bodi za Quality Geregy na Guru Nanak mlango wa abiria ulikuwa seat ya tano kutoka mbele, sasa zimekuja hizi michina milango iko mbele kama howo, sijui latra na tbs hawalioni hili kuwa ni tatizo? matrafiki wanapokagua abiria na wana kuta staff seat ina abiria wala hawahoji, nchi hii sijui tumeshindwa kujitawala? bora tumrudishe tu sultan za zanziber.

malalamiko yamekuwepo muda mrefu kuwa gari za mchina zina shida kwenye break system wala hatujali.
 
bodi za Quality Geregy na Guru Nanak mlango wa abiria ulikuwa seat ya tano kutoka mbele, sasa zimekuja hizi michina milango iko mbele kama howo, sijui latra na tbs hawalioni hili kuwa ni tatizo? matrafiki wanapokagua abiria na wana kuta staff seat ina abiria wala hawahoji, nchi hii sijui tumeshindwa kujitawala? bora tumrudishe tu sultan za zanziber.
Huenda maofisa wakati wapo mafunzoni walifundishwa kujali usalama wa abiria tu, na waka kariri na hawajiongezi kuona hilo tatizo la Makonda.

Mfano hawaruhusu abiria kukaa mbele ya bajaji, lakini wanaruhusu makonda kuweka sura zao mbele ya kioo cha gari.
 
Hiyo ina maana kwamba wamiliki wanajali maslahi yao binafsi, kwani wanashindwa kutenga siti mbili za mbele special kwa makonda?
kila bus huwa na stuff seat mbili, zinauzwa konda na dereva wa akiba wanatandika godoro kwenye bonnet, tunapita check point na trafik anaona kabisa dereva kalalia kigodoro ala hahoji. kisa tu kofia imeguswa kwa ndani
 
tunapita check point na trafik anaona kabisa dereva kalalia kigodoro ala hahoji. kisa tu kofia imeguswa kwa ndani
Mkuu kofia kuguswa kwa ndani ina maana gani? Hapo umeniacha
 
Makonda wawili wa nini? Mmoja tu anatosha. Kwanza inatakiwa tufanye kama majuu ambako gari linakuwa na dereva tu na ndiye anaweka na kutoa mizigo kwenye buti.
Madereva wetu muda wote wanawaza kukimbizana, hilo la wao kutoa mizigo itakuwa ngumu sana hapa kwetu.

Lakini Mamlaka zinapaswa kutizama upya swala hili.
 
Maboss wanaichukua, pale Dereva tyuuh ndo ana seat yake 7bu ni lazima.

Lakini wengine wanajiongeza wanakaa chini pembeni ya dereva kuna kisehemu huwa wanaweka foronya.
Niliwahi kuona wengine kama gari halina abiria wengi wanakaa kwenye siti, lakini gari ikijaa wanaweka roho mlangoni.
 
Ila wana moyo. Unakuta konda amekaa mazingira magumu kuanzia songea hadi mafinga kisa siti yake kauza.
Nawafananisha na wale wanaorithi nyumba halafu wanapangisha mpaka chumba anacholala halafu yeye analala anakesha nje.
 
Mpaka wanaamua kuuza siti inamaana maslahi yao ni madogo, sasa wanahatarisha maisha yao kwa kujaribu kuongeza maslahi yao.
 
Ndo maana ake, sasa bora hizo za kutoka Dar to mikoani.
Nenda mikoani, root za ndani ya wilaya, uone njegeka zake, sio abiria wala kondakta wote roho rehani.
Arusha niliona Haice hazina mlango na abiria wamejaa, chini zimetoboka barabara inaonekana 🙌🙌
 
Imekuwa kawaida kwa Makonda wa mabasi ya safari za mbali kukaa au kusimama pembezoni mwa kioo cha mbele, wana nin'giniza sura zao bila kuzingatia usalama wao.

Dereva pamoja na abiria ni lazima wafunge mikanda, je Makonda nao wanachukua tahadhari gani katika kuzingatia usalama wao wakati wa safari?

Gari ikielekea kugonga obviously dereva anaitoa upande wake na kuelekeza upande wa kushoto ambapo Makonda husimama, ajali ndogo ya kugonga inaweza kuondoka na maisha ya konda pekee.

View attachment 3168930

View attachment 3168932

Jana basi la Mallesas limegonga lori kwa nyuma, binti mrembo ambaye alikuwa ni konda akapoteza maisha papo hapo.

Apumzike kwa amani na Makonda wengine wachukue tahadhari kama sio kubadili utaratibu wa kukaa karibu na kioo cha gari.
Halafu traffic police wanakagua kila kituo kuona kama abiria wamekaa na wamefunga mikanda ya usalama
 
Back
Top Bottom