Makonda wa mabasi ya mikoani, kwanini mnahatarisha maisha yenu kwa kusimama karibu na kioo cha gari?

Makonda wa mabasi ya mikoani, kwanini mnahatarisha maisha yenu kwa kusimama karibu na kioo cha gari?

Imekuwa kawaida kwa Makonda wa mabasi ya safari za mbali kukaa au kusimama pembezoni mwa kioo cha mbele, wana nin'giniza sura zao bila kuzingatia usalama wao.

Dereva pamoja na abiria ni lazima wafunge mikanda, je Makonda nao wanachukua tahadhari gani katika kuzingatia usalama wao wakati wa safari?

Gari ikielekea kugonga obviously dereva anaitoa upande wake na kuelekeza upande wa kushoto ambapo Makonda husimama, ajali ndogo ya kugonga inaweza kuondoka na maisha ya konda pekee.

View attachment 3168930


View attachment 3168932

Jana basi la Mallesas limegonga lori kwa nyuma, binti mrembo ambaye alikuwa ni konda akapoteza maisha papo hapo.

Apumzike kwa amani na Makonda wengine wachukue tahadhari kama sio kubadili utaratibu wa kukaa karibu na kioo cha gari.
Njaa zinawaponza,basi karibu zote za kichina,kiti cha kwanza unapoingia upande wa kulia ni cha konda,lakini kwasababu ya njaa wanakiuza,halafu wanaamua kusimama pale mbele kitu ambacho ni hatari sana..
 
Kile
Maboss wanaichukua, pale Dereva tyuuh ndo ana seat yake 7bu ni lazima.

Lakini wengine wanajiongeza wanakaa chini pembeni ya dereva kuna kisehemu huwa wanaweka foronya.
Kisit makonda wengi wanauza ili wapate pesa pamoja na driver wake. Magari mengi sana hasa haya mapya ile seat huwa inaachwa kwa ajili ya konda na wala haingii kwenye mahesabu ya boss na hata kwenye chart haipo ila ndo ivyo makonda kujiongeza....
 
Hiyo ina maana kwamba wamiliki wanajali maslahi yao binafsi, kwani wanashindwa kutenga siti mbili za mbele special kwa makonda?
Siti ya konda ipo.. ila yeye ni nani hata aikalie asiiuze au asisimame pale mbele maana sometimes hata bus halijajaa ila utakuta kasimama pale mbele au kakaa juu ya engine. Wanafanana tu tabia, mazoea
 
Una piga story na mtu vzuri tu ila kwenye hatari ya kifo ana kupelekea wewe yeye a save 😂😂
😆😆😆 binadamu likija suala la ubinafsi hafikiri mara mbili anakubanika vizuri tu.

Ndo maana abiria wengi wanatakaga siti upande wa dereva.
 
Boss mbona unasagia kunguni nafasi za ajira ya watanzania wahitaji? Uwepo wa konda kwenye gari ni ajira kwa watanzania
kabisa, konda nirahisi kumtimua ukaweka mwingine dereva hasa wa long route sio rahisi kupata replacement, konda anaweza toka na bus dar akafika moro akashushwa wakala akaendelea na safari.
 
Siti zao mbona zipo ila huwa wanaziuza. Na kweli anawaambia fungeni mkanda na dereva wake anafunga mkanda ila yeye anasimama.
 
Maboss wanaichukua, pale Dereva tyuuh ndo ana seat yake 7bu ni lazima.

Lakini wengine wanajiongeza wanakaa chini pembeni ya dereva kuna kisehemu huwa wanaweka foronya.
Sio mabasi yote mkuu, zile mbili huwa ni zao , mizigo ya njiani wanakaba, basi nyingine zinapakia njiani pesa haifiki kwa boss.
 
maisha ya wadada yamewekwa rehani sana, kilasiku wanachimbwa biti na madereva nitakulengesha, sasa wamefanyakweli binti kalengeshwa kachomolewa roho

matajiri wengi wamekuwa wakiwahusudu makonda wa kike kwa kujituma kutoa huduma nzuri na uaminifu. unakuta binti tangu kigoma hadi dar yuko gado, na bado anafika saa nane mchana anaambiwa saa mbili usiku aamshe chuma kurudi,

kuna wengine akifika ameungua anaenda kujiweka rehani sheli apate mafuta bus igeuze atakazo okota njiani alipe deni la mafuta, bado mwisho wa mwezi boss anamwambia aisee rejesho la binki mwezi huu mawazo.

kuna konda mmoja nilikuwa naongea nae akanisimulia madhila yake, dereva anapewa posho elfu 30, njiani anamwambia binti ampe elfu 50, akigoma anazima bus anasingizia bovu, au anamchimba biti kuwa atamlengesha kwenye semi, wakifika safari amlipie dereva hela ya gesti na chakula. namuda mwingine akifika na uchovi ule dereva anataka ale mzigo tena wa bure

huku nyuma hesabu yote kaacha kwa tajiri akifika ndo aanze kusaka booking aweke mafuta ya kurudi hela isipotosha anajiweka rehani huku akitegemea abiria wa njiani alipe deni la mafuta, muda mwingine binti anarudi home hata elfu mbili hana.
 
Back
Top Bottom