Makonda: Wazururaji hawataenda gerezani bali watafanya kazi za kuzibua mitaro, kufyeka nyasi na kusafisha barabara

Makonda: Wazururaji hawataenda gerezani bali watafanya kazi za kuzibua mitaro, kufyeka nyasi na kusafisha barabara

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mkuu wa mkoa wa Dsm Paul Makonda amesema watu watakaokamatwa wakizurura jijini Dar watawajibishwa kwa kuzibua mifereji, kufyeka nyasi, kufagia barabara na kufanya kazi nyingine za usafi.

Makonda amesema hatawaweka mahabusu wazururaji kwa ajili ya kuepusha msongamano wakati huu wa Corona.

Hivyo RC amesisitiza kama mtu anatoka nyumbani kwake na kwenda mjini bila malengo ya msingi basi ajiandae kukutana na Rungu la Makonda.

Source Eatv habari!
 
Makonda akili zake anazijua mwenye sijui anatumika au anapenda tu mwenyewe kuwa headline kwenye media kila mara kwa sababu ya ujana wake kwa ufupi tuvumilie tu mdaa wake ukifika mwisho anaweza kuja mwingine na visa zaidi ya huyu kwa maono yangu jiji kubwa kama ili anatakiwa kiongozi mwenye umri kunzia miaka 40
 
Tofauti ya mwamri wa tabora na bashite ni kwamba mwamri anafwatilia mambo ya msingi ili apate sifa ila bashite anafwatilia mambo ya kipuuzi ili apate sifa (za kijinga).

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili jamaa Hakika ni shamba sana na halina hekma hata chembe! Kuna watu wa Lumumba wanamsifia kwa maagizo ya kijinga! Mtu amekataliwa na nchi kama Marekani kutokana na upuuzi wake halafu wajinga fulani wanamsifia!
 
Mkuu wa mkoa wa Dsm Paul Makonda amesema watu watakaokamatwa wakizurura jijini Dar watawajibishwa kwa kuzibua mifereji, kufyeka nyasi, kufagia barabara na kufanya kazi nyingine za usafi.

Makonda amesema hatawaweka mahabusu wazururaji kwa ajili ya kuepusha msongamano wakati huu wa Corona.

Hivyo RC amesisitiza kama mtu anatoka nyumbani kwake na kwenda mjini bila malengo ya msingi basi ajiandae kukutana na Rungu la Makonda.

Source Eatv habari!
Hakuna binadamu yeyote anapenda kuzurura hovyo...jua kali, joto la DSM namna hii eti uende kariakoo ama posta kuzurura bure hakuna kitu kama hicho...

Kila anayekwenda pahala ana sababu za msingi...

Hili zoezi navyowajua hawa police wetu majanga makubwa yatatokea..
Kumbukeni sekeseke la usafi lilivyoleta majanga...

Project za huyu jamaa huwa zinafeli kabla hata hazijaanza!!
 
Back
Top Bottom