Makonda: Wazururaji hawataenda gerezani bali watafanya kazi za kuzibua mitaro, kufyeka nyasi na kusafisha barabara

Makonda: Wazururaji hawataenda gerezani bali watafanya kazi za kuzibua mitaro, kufyeka nyasi na kusafisha barabara

Kuna wakati mtu unajikuta uanatamani kusema kitu lakini inakubidi tu unyamaze kwa sababu usalamu wako ni muhimu sana.
 
kwani mzurulaji ni yupi? ni zipi sifa a mzurulaji? nani anapaswa kuitwa mzurulaji na kwanini? utamtambuaje huyu mtu ni mzurulaji na huyu sio mzurulaji? vipi kama nimeenda kwa shughuli zangu kisha nikakumbana njiani na hao walioagizwa kukamata wazurulaji nami nitakamatwa kwa kua sina kielelezo chochote kinacho nitambulisha kwamba mimi so mzurulaji?
 
Tofauti ya mwamri wa tabora na bashite ni kwamba mwamri anafwatilia mambo ya msingi ili apate sifa ila bashite anafwatilia mambo ya kipuuzi ili apate sifa (za kijinga).

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwaambia watu wasizurure; watoke nyumbani kwenda kazini tu au kwenye shughuli inayoeleweka, ni jambo la kipuuzi? Kwa hiyo nchi zote zilizoanzisha lockdown zinafanya upuuzi tu? Ilichofanya Tanzania ni kutoanzisha lockdown kwa sababu ya msingi kwamba watu wengi wasipotoka nyumbani familia haitakula siku hiyo. Kuruhusiwa kutoka nyumbani isiwe ndiyo tikiti ya kuzurura. Nchi nyingine watu wanachapwa bakora kwa kuonekana mitaani badala ya kuwa nyumbani kwako.
 
Nchi gani hiyo hebu tutajie

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makonda akili zake anazijua mwenye sijui anatumika au anapenda tu mwenyewe kuwa headline kwenye media kila mara kwa sababu ya ujana wake kwa ufupi tuvumilie tu mdaa wake ukifika mwisho anaweza kuja mwingine na visa zaidi ya huyu kwa maono yangu jiji kubwa kama ili anatakiwa kiongozi mwenye umri kunzia miaka 40

Huyo mtu mwenye miaka zaidi ya 40 mfano awe Kange Lugola, Kigwangalla nk.
 
Anafeli sana..Naona tatizo ni elimu yake
 
Mkuu wa mkoa wa Dsm Paul Makonda amesema watu watakaokamatwa wakizurura jijini Dar watawajibishwa kwa kuzibua mifereji, kufyeka nyasi, kufagia barabara na kufanya kazi nyingine za usafi.

Makonda amesema hatawaweka mahabusu wazururaji kwa ajili ya kuepusha msongamano wakati huu wa Corona.

Hivyo RC amesisitiza kama mtu anatoka nyumbani kwake na kwenda mjini bila malengo ya msingi basi ajiandae kukutana na Rungu la Makonda.

Source Eatv habari!
Kwahiyo hatawapeleka mahakamani? Au yeye pia ni hakimu na jaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom