Makondeni, pepo ya dunia wengi wasiyoijua

Makondeni, pepo ya dunia wengi wasiyoijua

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Waliokulia vijijini mashambani wanalijua hili... Waliokulia mijini kwenye uchafuzi wa kila aina na vurugu zote hawaijui ladha yake
Ukisoma habari za peponi na vile kulivyo unaweza kukubalina nami kwamba makondeni ni pepo ya dunia
Hakuna vurugu za miziki
Hakuna honi
Hakuna fujo za bodaboda
Hakuna vurugrlumechi za daladala
Hakuna kelele za wahubiri feki wa kila imani
Hakuna makaka wala madala poa
Hakuna wezi wala vibaka
Hakuna gesti bubu
Hakuna aina yoyote ile ya uchafuzi wa hali ya hewa
Hakuna vyakula feki
Hakuna kuku mazezeta
Hakuna nyama kibudu
Hakuna upigaji wala utapeli wa aina yoyote ile
Hakuna ulaghai wa mapenzi , nyumba ndogo wala michepuko
Kilichopo huko ni amani, utulivu, u pendo, ukarimu, ucha Mungu, vyakula vizuri vitamu nknknk

Kama ukiweza unaweza kutengeneza pepo yako ya makondeni walau robo yake maokoto na muda vikikubariki...
Zifuatazo ni picha nyingi nyingi za mfano wa makondeni kulivyo
1739888884900.jpg
1739888892371.jpg
 
Mandhari ya kuvutia mno
1739888843075.jpg
1739888839516.jpg
hakuna kubanana wala hakuna ugomvi wa mipaka.. Wala huwezi kupita uchochoro na kutokea kwenye sebule wala choo cha mtu.. Huko hakuna kutapisha vyoo wakati wa mvua😪😆🤣
 
Back
Top Bottom