Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,557
- 8,673
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata msemeje ccm ni Chama dume
Hata Lowasa kwenye hotuba yake alisema alishiriki vita vya Kagera
Tofauti ya makongoro na hao ni :-
Alipigana vita vya Kagera Tena kwa kujitolea akiwa na Umri mdogo tu wa Karibu miaka 18
Ni afisa wa jeshi mwenye taaluma ya mizinga,usalama na mikakati
Ana shahada ya mikakati ya kimataifa na Diplomasia
Na amefanikwia kujenga Jina lake mwenyewe bila kutegemea kubebwa na Jina la baba yake ...Ndio Maana aligombea kwa tiketi ya upinzani pamoja na kuwa na uhakika wa kupitishwa kwa protocol za Jina Ndani ya ccm
Familia Yao imeishi maisha very humble na ya kuridhika sana ..Kama watanzania
Kassoro pekee inayoweza kumgharimu anayotakiwa kufanyia kazi ni kudhibitisha kuwa Ana uelewa wa UCHUMI wa soko na kuwa atakuwa rafik Kwa sekta binafsi ambayo inawajibika....ni lazima akutane na wafanyabiashara awahakikishie kuwa anaunga mkono Uchumi wa kisasa ...wasikir atafuata sera za UCHUMI za babake ...unaweza usipende utajiri Kama Obama lakini unaweza kusimama wakafaulu hawa watakuwa na uhakika kabisa ...mgombea pekee ambaye hatakuwa akiwaomba wafanyabiashara rushwa ni Makongoro
Mgombea pekee ambaye hatakuwa na genge la wafanyabiashara wa kuwalipa fadhila ni yeye ....Hadaiwi pesa na Nchi kuwadi Kama Iran ..na zingine ..akiwa na washauri wazuri anaweza kufanyia kazi kwa uhuru Zaidi
Katika watia nia wote waliojitokeza mpaka sasa, inashangaza kujenga hoja zao juu ya upungufu ya kimfumo na kiutawala wa serikali ya CCM ambayo na wao ni sehemu ya utawala huu. Wanaongea as if ni wageni au walifungwa vitambaa machoni sasa wamefunguliwa ndiyo wanajifanya kuona upungufu na uchovu wa CCM.
Tuwe wa kweli hakuna asiyejua Ccm ilipofika haiwez kutusogeza mbele hata kwa nusu hatua,,, wengi waliobaki ni watega mingo au opportunists..
Wako kwenye serikali ya ccm kwa miaka mingi mbona walikuwa kimya mambo yalivyokuwa yanakwenda kombo... Sasa hivi kila mtia nia wa ccm ndiyo anajifanya kuona mafisadi.. kila mtu ndiyo anaijua epa escrow nk. Wakati wapinzani wakipaza sauti juu ya ufisadi huu wanaccm hawa walijifanya hawaoni na as if hakuna kosa lililofanyika..
Mwanaccm anayetangza nia kwa kujenga hoja yake juu ya ufisadi leo.. hana sifa nyingine zaidi ya UNAFIKI
Walikuwa wapi siku zote..
Sasa hivi wanamwangushia lawama Kikwete.. nashangaa hata mawaziri nao eti ni wakosoaji wa mfumo uliopo..!??
Mtawezaje kujitoa na kuwa suluhisho la matatizo wakati ninyi wenyewe n sehemu ya tatizo..
zumbemkuu kwanza habar za asbh??Kweli sina hakika kama kushiriki vita vya kagera ndo sifa ya uongozi
Hapa sasa urais nchi hii ni kwa watoto wa marais tu. Kwan inavyoelekea wameshajipanga. Anaingia makongoro miaka kumi. Akitoka anaingia hussein mwinyi miaka kumi akitoka anaingia ridhiwan. Miaka kumi. Wengine cjui kama kwa mpango wa urais wa kuridhiana cjui itakuwaje.
Hapa sasa urais nchi hii ni kwa watoto wa marais tu. Kwan inavyoelekea wameshajipanga. Anaingia makongoro miaka kumi. Akitoka anaingia hussein mwinyi miaka kumi akitoka anaingia ridhiwan. Miaka kumi. Wengine cjui kama kwa mpango wa urais wa kuridhiana cjui itakuwaje.
huyo RIDHIWAN ataingia kwa sifa zipi? afadhali hussein MWINYI
Mkuu gfsonwin umenifanya nifikirishe kichwa changu zaidi, kuwa huenda awamu ijayo vionambali vimeonyesha kutakuwa na vita hivyo anahitajika mjeshi ikulu, nnachojiuliza Mwl. Nyerere alipigana vita gani kabla ya kuwa rais? Mwinyi, mkapa?? Hiki kigezo cha ujeshi kinanipa mashaka sana, sasa hiyo sifa ya kusoma diplomasia wakati huo huo kushiriki vita ya kagera ndo inaniumiza kichwa zaid, waliosoma hiyo diplomasia wanajua zaid, mie fundi mchundo ngoja
nijinyamazie tu niendelee kuona mazingaombwe hadi October 2015,
Swali la kizushi mkuu, umekata tiketi ya usafiri gani? Au na wewe utatangaza safari ya matumaini nije kukuunga mkono?
kwakweli hii nchi tunakazi sana
raia hatujui tunachotaka, hatuna vipaumbele vyetu sisi kama raia, hatujui hata tunaelekea wapi
napata picha kwamba kile kitu cha mie nikiamka naenda job jion narudi na mkate wa watt basi kimenitosha sihitaj kitu zaid ya hapo. hata hawa wanaharakat wetu hawajaweza kutuelimisha kuhusu nini ziwe sifa za rais tunayemtaka.......
swali lako la kizush jibu lake ni hili.............Mpaka sasa ata kadi ya kupiga kura sina wenzangu waende wakamchague manake sijui naenda kuchagua nini.
BTW hivi DSM inaandikisha lin wapiga kura?