Ulikuwa una hoja lakini umeshindwa kuisimami na ndio maana walio wengi wamekudis ...q. sio kuwa ndani ya CCM hakuna watu wema, wazarendo, wenye kuweza kuwatendea haki wenzao...ndio kusema yaliyokea kwa Zitto ndani ya CDM sio kusema CDM yote ina haiba ya Zitto, Samson Mwigamba na Kitla Mkumbo ..au yaliyotokea CUF sio kusema haiba ya Mzee Hamad Rashid ni sawa na Wanacuf wote.Kugeneralize mambo ni ufinyu wa kujituma kujua ukweli wa jambo..
Kuna watu makini ndani ya vyama vyetu vya siasa kuanzia CCM, CDM, CUF, navinginevyo wana uwezo thabiti wa kupambana na matatizo mazito yanayotusibu kama Rushwa, Wizi, Ufisadi, Maendeleo...lakini jinsi ya kuwaweka na kusimamia Taifa.Kwa kuwa tunao walalamika kuwa wanalitafuna Taifa wako ndani ya MFUMO [System] wa Taifa letu.Wengine ni viongozi, watendaji wakuu, watendaji wadogo na hata wananchi wa kawaida.Na popote penye ufisadi au wizi fahamu kuna mahusiano ya kimaslahi pia ...na jambo linapo husu maslahi tambua lina husu hatima ya VITA katika kutengua hatima hiyo.
Tunaposema Taifa liko kwenye Mtanziko wa UFISADI NA RUSHWA ndio kusema sio Viongozi tu hata sie wananchi wa kawaida tuna mchango wetu kwa kuwa mfumo pia uliojengwa HAKUNA RAIA wa kawaida anae weza kusimama na kusema jambo la UFISADI na RUSHWA bila kusukwa sukwa na mfumo wetu.Hivyo kuna tatizo la kitaifa la Ufisadi na Rushwa lakini si kweli kuwa kila RAIA wa Tanzania ni mla Rushwa na Fisadi kama ambavyo wewe unavyotaka kutuaminisha kuwa Wanccm wote ni tatizo.Jenga hoja kwa misingi ya kujenga FACTS.