Makontena 115 ya sukari iliyofichwa yakamatwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Makonda

Makontena 115 ya sukari iliyofichwa yakamatwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Makonda

Kama iko bandarini si manake bado haijatoka ili iingie godown?,
au anataka kusema ilipakiwa toka godown ikaenda kuficha bandarini?
 
Taarifa zinazotolewa kuhusu sukari hazina ukweli wala mtiririko unaoeleweka kwa akili ya kawaida. Serikali na jamii kwa ujumla imeingia kwenye mhemko ambao ni wa kupuuzwa kwa muda.
Jana walitoa taarifa kwamba serikali imeingiza sukari, hapo hapo wafanyabiashara wakaruhusiwa kutoa sukari iliyokuwa bandarini, sukari ya kwenye maghala haikufichwa n.k.
Haya yote ni kuwachanganya wananchi bila sababu yoyote. Kama kuna tatizo, viongozi na vyombo vya dola wafuatilie kwa utaratibu na ufanisi na taarifa za uhakika zitolewe badala ya kila mmoja kutoa matamko yasiyoeleweka kama mazuzu.
 
badala na kukaa na kutafakari jinsi ya kugundua viwanda vipya wanagundua makontena yaliyo nchi kavu,
 
Kina Makonda na Ally S Hapi msituletee usanii fanyeni kazi,msitoe statement kabla hamjajiridhisha 100%,sukari ipo kwenye kontena ICD/Bandarini mnasema imefichwa? ona Zakaria/TRA wamewaumbua kwamba kontena za bandarini zilikuwa zinasubiri taratibu za utoaji,huku napokaa sukari ni 2200-2500 na ipo bwelele sijui hiyo scarcity ni ya wapi? Tunataka tujadili LU-MI-GU na Device zake hizo 14 huku alilamba 99% ya malipo kabla hata hajafanya kazi.
 
U
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amebaini sukari zaidi ya makontena 115 iliyofichwa kwenye bandari kavu ya PMP, Mkuu wa Mkoa ametoa taarifa kuwa kuna zaidi ya Makontena 162 na sio 115 kama ilivyoripotiwa hivyo ameagiza zoezi la ukaguzi wa sukari liendelee kwenye Bandari kavu hiyo.
silolijua sawa na usiku wa giza.
majibu ya Sukari hiyo yanapatikana katika gazeti la mwanachi la tarehe 11/05/2016 pg 9 penye kichwa cha habari ''SAKATA LA SUKARI LACHUKUA SURA MPYA'' . Wanasema kuwa sukari hiyo iliuwa huko ili kumaliziwa kwa taratibu za ulipaji kodi za TRA. ''.....ilikuwa inasafirishwa kwenda Burundi, lakini tukaomba tuinunue na itumike hapa Nchini kutokana na sababu ya upungufu wa Sukari hapa kwetu...''
 
VItu vingine ni ujinga tu.
Eti amegundua,,,,He has discovered.. hahahahahaha

Haaa haaa kwahiyo unakataa hajagundua mbona vitabu vya history tuliambiwa Mzungu Rebman alikuwa mtu wa kwanza dunia kuona Mlima Kilimanjaro wakati wachagga walikuwa wakiota kuni,walikuwa wakiwinda wakiamka asubuhi wanaiona barafu hamkubisha 😳.Hakuna namna lazima tukubaliane Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar ni mchapaka kagndua sukari bandari kavu haaa haaaa.
 
Kina Makonda na Ally S Hapi msituletee usanii fanyeni kazi,msitoe statement kabla hamjajiridhisha 100%,sukari ipo kwenye kontena ICD/Bandarini mnasema imefichwa? ona Zakaria/TRA wamewaumbua kwamba kontena za bandarini zilikuwa zinasubiri taratibu za utoaji,huku napokaa sukari ni 2200-2500 na ipo bwelele sijui hiyo scarcity ni ya wapi? Tunataka tujadili LU-MI-GU na Device zake hizo 14 huku alilamba 99% ya malipo kabla hata hajafanya kazi.
Tujadili hapo kwenye nyekundu na sio usanii wa sukari
 
Serikali ya vyombo vya habari hii. Kuna mahali hawa watu wanadanganyana ili kuharibiana. Ni kuiga tu kila kitu bado sauti yake tu. Mh rais, kabla hujateua akuonyeshe kitu cha ubunifu alichobuni na kinachomwiingizia kipato. Hao uliowateua hawana sifa.
 
Hii mikuruko mingine mibaya sana mkiangukia pua mnajifuta kimykimya amsemi msije sema ipo kihalali to
 
Hivi nyumbani ukiwa na kilo 50 ni sahihi au ni kosa?
 
Hapo sasa.....makontena 162 yamefichwa....really?? kwenye bandari kavu??

MKUU kwañi ukiona kontena unawezaje kujua imesheheni kitu gani bilà ya kupewa tip off, walio toa taarifa wanajua kinacho endelea - Bandari kavu zunatumika kuficha vitu Vingi tu, hatutaki kuambiwa eti Sukari ilikuwa imehifadhiwa hapo jwa muda ikiwa kwenye transit kwenda nchi jirani. Usanii huu ni mbaya sana.
 
Eee boh! Kama kagundua aziite kwa jina lake kama walivyofanya wagunduzi waliopita, anasubiri mini sasa!
 
Watakamata hadi sukari inayoenda Zambia au Rwanda ,halafu watasema ilifichwa kumbe ilikuwa kwenye mchakato wa kusafirishwa.

Serikali iache kufanyia kazi kwa mizuka.
 
Hapo sasa.....makontena 162 yamefichwa....really?? kwenye bandari kavu??
Wandishi wetu ni shida sana. Unawezaje kuficha kontena 162? In fact zoezi zima la kamata kamata tumekurupuka sana, hatukujipanga kukabili upungufu wa sukari baada ya kuzuia imports.
 
Jana ITV walionyesha sukari nyingine ikiwa bandarini ya Zakaria ,ilikamatwa na Takukuru nayo ilifichwa!!!!

Maelezo ya Zakaria ni kuwa ilikuwa inaenda Burundi,sasa serikali kama inataka sukari ya nje si wamwambie Zakaria aagize kutoka nje.
 
Back
Top Bottom