Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nadhani TRA wanaweza kutoa maelezo mazuri kuhusu hili sakata.Kama yapo ICD ina maana yamehifadhiwa hayajafichwa!! Waache siasa! Hayo mengine yanaenda nje nchi na hata Ushuru hayajalipiwa! Utasemaje yamefichwa?? Unawezaje kufich kontena kwenye Bandari kavu??
Ufanyaji kazi wa serikali ya Magufuli unatia kichefuchefu....
Waache kukimbizana na sukari iliyozalishwa nchi za watu, waende kwa wakulima wa Miwa wakaulize kwa nini wameachana na Kilimo cha miwa
Mh Makonda, Sukari ina muda wake na ikipitiliza muda ule hakika lazima iharibiwe. Sasa kama walienda kuficha huko, waendelee. Suluhisho la kumaliza tatizo la sukari si kugundua zilizofichwa bali ni kuzalisha zaidi. Tuna ardhi nzuri, maji mengi (mito) ila zana za kuzalisha miwa hatuna. Sio kwamba hazipo duniani bali uwezo wa kuzinunua (mtu binafsi) Hatuna, Tunahitaji kuwezeshwa. Serekali iwasaidie wenye nia ya kulima miwa. Viwanda vya sukari vianzishwe kwa makusudi. Nendeni hapo chini hapo Madagaska mkajionee wenyewe kilimo cha miwa. Kwa nini tusichague kamkoa kamoja tu kakawa maarufu kwa kilimo cha miwa? Mfano Zanzibar?
Tatizo la uhaba waa sukari halikuanza mwaka huu au awamu hii ya JPM. Kama mnataka sifa za kweli, itafuteni dawa na dawa ni kuongeza uzalishaji.wa miwa na kuongeza viwanda vya sukari.
Mkuu itakayo expire itawekwa kwenye mifuko na itaonesha ina expire 2020