Makontena 115 ya sukari iliyofichwa yakamatwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Makonda

Makontena 115 ya sukari iliyofichwa yakamatwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Makonda

Kama yapo ICD ina maana yamehifadhiwa hayajafichwa!! Waache siasa! Hayo mengine yanaenda nje nchi na hata Ushuru hayajalipiwa! Utasemaje yamefichwa?? Unawezaje kufich kontena kwenye Bandari kavu??
Mbona hawauzi sasa?
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amebaini sukari zaidi ya makontena 115 iliyofichwa kwenye bandari kavu ya PMP, Mkuu wa Mkoa ametoa taarifa kuwa kuna zaidi ya Makontena 162 na sio 115 kama ilivyoripotiwa hivyo ameagiza zoezi la ukaguzi wa sukari liendelee kwenye Bandari kavu hiyo.
Lumumba a.k..a buku 7, hebu acheni miemko ya UVCCM, huwezi kununua bidhaa yako ya biashara usiwe na mahala pa kuiweka ambayo ni salama.
"Speed without brain is Zero", kwa mawazo finyu unataka asammbaze barabarani au?
Hebu tuwe na fikra chanya au Logic hasa tunapozungumzia masuala ya Msingi kwa Taifa kwa ujumla na kuacha kutumika na hisia za malipo.
 
Nafurahi kuona watu wakichukia ulaghai. Nimesema kila mara hiki cheo hakina ilani ya uchaguzi. Kipo kipo tu. Kazi yake ni kuzuia wapinzani kufanya mikutano na kutafutia misifa sifa tu!
 
U

silolijua sawa na usiku wa giza.
majibu ya Sukari hiyo yanapatikana katika gazeti la mwanachi la tarehe 11/05/2016 pg 9 penye kichwa cha habari ''SAKATA LA SUKARI LACHUKUA SURA MPYA'' . Wanasema kuwa sukari hiyo iliuwa huko ili kumaliziwa kwa taratibu za ulipaji kodi za TRA. ''.....ilikuwa inasafirishwa kwenda Burundi, lakini tukaomba tuinunue na itumike hapa Nchini kutokana na sababu ya upungufu wa Sukari hapa kwetu...''
mkuu,samahani!unaweza kuki upload kipisi cha gazeti chenye habari hio...?
 
MKUU kwañi ukiona kontena unawezaje kujua imesheheni kitu gani bilà ya kupewa tip off, walio toa taarifa wanajua kinacho endelea - Bandari kavu zunatumika kuficha vitu Vingi tu, hatutaki kuambiwa eti Sukari ilikuwa imehifadhiwa hapo jwa muda ikiwa kwenye transit kwenda nchi jirani. Usanii huu ni mbaya sana.
Mkuu

Bandari kavu zinamilikiwa na TRA pamoja na Operator. Hakuna kitu kinachoweza kuingia au kutoka bila TRA kujua.

Sasa kama kuna ishu ya kuficha sukari, basi TRA ndio vinara wa kuficha hiyo sukari.
 
he kama inasubiri clearance? Bado kidogo meli yenye sukari ikitia nanga bandarini tutaambiwa ' sukari imegundulika imefichwa kwenye meli'!

Kweli mkuu maana mimi nilivyocheck ile habari itv nilicheka sana yaani kontena linafichwa bandari kavu duu kweli hatupo serious na hii issue..Mzigo unasubiri vibari vya tfda ile utoke na pia ni watransit watu wanakuambia mzigo umefichwa tena eneo la customs area.
 
Je Wajua?
Je Wajua Mtu Wa Kwanza Duniani Kugundua Uwepo wa Makontena Ya Sukari Yaliyofichwa Katika Bandari Kavu?
Hapo Mnamo Tarehe 11/05/2016 Mhe Paul Makonda,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ameweka Historia ya Aina Yake Iliyo Ingizwa Katika Kitabu cha Guiness World Records Kwa Kugundua Uwepo wa Makontena 165 ya Sukari Katika Bandari Kavu ya P.M.P!
Tukio Hili Limeifanya Tanzania Kuingia Katika Orodha ya Nchi Maarufu na Pia Ugunduzi Umeöngezwa Katika Maajabu Kumi ya Dunia!
Hongera Tanzania,
Hongera Makonda!
 
Kwa sisi wananchi wa kawaida, we wouldn't care kama sukari ilikuwa inafichwa au la, provided bei ilibaki kuwa shs 1,800-2,000 kwa kilo. Haya yanayofanyika sasa ni siasa fulani ambazo mwisho wa siku wananchi wa kawaida ndio wanaoumia.
 
Yaani hivi ni vioja vya karne how come mwizi akafiche mzigo wake wa wizi kituo cha polisi? ICD au bandari kavu ni sehemu ambayo controlled by TRA or customs bonded. Kwa maana hiyo bado ipo kwenye hatua eidha za ulipaji wa kodi au kusafirishwa nje ya nchi.Huyu jamaa kwa siasa hajambo wacha tuongozane kwa MIZUKA tu.
 
makonda utampenda tu hata kama hupendi.
 
Ile movie ya tani 4 imeishaje?
Maana naona anazindua nyingine
Ile ishu Paul Makonda aliumbuka pale yule mzee wa ki Islam alipomjibu kuwa, "nimenunua hii sukari kwa ajili ya kwenda kutoa sadaka"

Paul Makonda ikabidi abadili kosa, sasa anamlaumu yule mzee wa ki Islam kwa kuweka sukari ghorofa ya 6 katika nyumba isiyoisha.

Jamani, tani 4 ni sawa na 4,000kg
4000kg * 2000 Tshs = 8,000,000 Tshs

Wakati mwingine watu wawe wanatumia akili, sio kutaka kick kwa 8mil. Waende huko kwenye migodi ya Barrick ambapo kuna upotevu wa mabilioni.
 
Back
Top Bottom