Mh Makonda, Sukari ina muda wake na ikipitiliza muda ule hakika lazima iharibiwe. Sasa kama walienda kuficha huko, waendelee. Suluhisho la kumaliza tatizo la sukari si kugundua zilizofichwa bali ni kuzalisha zaidi. Tuna ardhi nzuri, maji mengi (mito) ila zana za kuzalisha miwa hatuna. Sio kwamba hazipo duniani bali uwezo wa kuzinunua (mtu binafsi) Hatuna, Tunahitaji kuwezeshwa. Serekali iwasaidie wenye nia ya kulima miwa. Viwanda vya sukari vianzishwe kwa makusudi. Nendeni hapo chini hapo Madagaska mkajionee wenyewe kilimo cha miwa. Kwa nini tusichague kamkoa kamoja tu kakawa maarufu kwa kilimo cha miwa? Mfano Zanzibar?
Tatizo la uhaba waa sukari halikuanza mwaka huu au awamu hii ya JPM. Kama mnataka sifa za kweli, itafuteni dawa na dawa ni kuongeza uzalishaji.wa miwa na kuongeza viwanda vya sukari.