Makopo ya ARV yamezagaa mtaani kwangu

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2021
Posts
4,134
Reaction score
10,644
Hii ni ishara mbaya sana.

siku ya tano leo nakutana na makopo ya kubebea ARV kwenye haka kamtaa ninakoishi.

Yanatupwa tu yani hadi watoto wanayachezea kabisa.

leo ndio nimejua kuna kopo za vidonge 30, 90 hadi 100

Hii nchi kwa maeneo ya mjini kuna rate kubwa ya mambukizi ya UKIMWI.
 
Mi mwenyewe hii kitu ilinishangaza kuona makopo na yale makaratasi ya maelezo yakizagaa mitaani bila kudhibitiwa kama takataka, ilianza kunipa mtihani wa kubaini ni kina nani mtaani kwangu wanatumia hizi dawa
 
Km unakutana nayo mara kwa mara dizain unapewa ishara
 
Sioni sehemu ilipoandikwa ARV
 
Umejuaje kama ni makopo ya kubebea ARV?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…