Makopo ya ARV yamezagaa mtaani kwangu

Naona ugonjwa umeshazoeleka kiasi kwamba waathirika hawajali kujulikana, wanatupa kopo tu. Mwanzoni ilikuwa siri, aibu na fedheha!
kuna wengine wanakunywa hizo dawa waziwazi bila kificho kama zamani. Wapo pia wanaowapelekea moto waathirika bila hofu ya kuambukizwa
 
Shukuru Mungu unakutana nayo ili usijisahaulishe.
Hiyo inakukumbusha kuwa upo Tena karibu kabisa na wewe hivyo uchukue tahadhari.
 
Ili muanze kuwatenga, kuna JAMII nyingine wakisikia hivyo wataanza kunyoosheana vidole. Hata ww usingependa kuanza kujulikana iwapo ungepata ugonjwa kama huo
Kijana uwe unasoma na kuelewa kilichoandikwa Kabla ya kujibu
 
Inaonekana huo mtaa wenu watu hamzingatii usafi wa mazingira.
 
Hakuna, shida ni ishara njema watu wanatumia dawa. Mbaya yasingeeonekana, Mgeendelea kulowekeana mpaka basi.
 
Safi sana acha tupungue ugali utoshe
 
Watu wanaogopa gono na UTI sugu sio ukimwi mzee kua makini, hakikisha umevaa socks vizuri kabisa kabla ya kuvaa kiatu, haijalishi ni raba au buti
 
Unajuaje ni ARV? Mbona haijaandikwa hivyo?
 
Wengine tunatumia ARV kwa ajili ya kutibu Hepatitis.
 
Pedi zilizotumika, pampasi, condom zilizotumika zimechukua nafasi ya mifuko ya plastiki.. Kila mtaa zimetapakaa
 
Kweli dunia ina siri, na utu uzima wangu sikuwahi kuona kopo wala chochote kinachohusu ARV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…