Makosa ambayo wanaume tunakatazwa kuyafanya kwa wanawake wetu na kutugharimu

Makosa ambayo wanaume tunakatazwa kuyafanya kwa wanawake wetu na kutugharimu

Billie

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Posts
13,588
Reaction score
22,752
Kosa kubwa utakalofanya mwanaume kwenye mahusiano yoyote na mwanamke katika mapenzi

1.Kufanya kila njia hili kutimiza mahitaji yake na shida zake

2.Kusema ndio kwa kila kitu anachokihitaji.

3.Kumfanya kama nguzo yako katika mahusiano yenu

4.Kumuonesha kuwa unaogopa kumpoteza kwenye maisha yako.

5.Kumvumilia jeuri na dharau anazoonesha kwako

6. Kumpa kipaumbele sana yeye kuliko maisha yako wewe mwanaume kiujumla.

7.Kumpa uhuru wa kufanya kila kitu anachojisikia kwenye maisha yake bila kumsahihisha ,kumkosoa, na kumfanya awajibike kwenye makosa yake.

Ukweli ni kwamba ukiwa unafanya vitu hivi kwenye mahusiano yawe nje ya ndoa au ndani ya ndoa asilimia 95% wanawake lazima wawaangushe chini wanaume wanaowajali kwa namna hii.

Kuwa mpenzi na mwenye upendo kupitiliza hakuwezi kukusaidia mwanaume kufanya mahusiano yako yawe imara na mwanamke.

Mwanaume unatakiwa upende kama mwanaume usiige tabia za wazungu za kuwaabudu wanawake katika mahusiano .

Kuwa mwanaume wa shoka na siyo mwanaume mzuri kwa mwanamke wako .Kazi yako kubwa ni kutoa ,kulinda na kuhifadhi na kumuongoza mwanamke kufuata amri zako. Usizidishe zaidi ya hapa.

Nitawapa siri ndogo ambayo hamjui kuhusu wanawake.

1.Wanawake huwa hawaondoki kirahisi kwenye mahusiano waliyowekeza nguvu zao na muda .Mfano kaanza na mwanaume akiwa chini mpaka wameinuka wakiwa pamoja na kupata mafanikio ni ngumu kuondoka kirahisi katika haya mahusiano .

Atosalimu amri na hatokuwa tayari kuona mwanamke mwingine anakuja kula matunda ya jasho lake kutoka kwa mwanaume aliyepambana naye akiwa chini.

2.Wanawake huwa wanawataka na kuwapenda sana wanaume wanaowachukulia kama takataka hasa wakiwa na uhakika kuwa mwanaume huyo pesa anazo.

Watasimama kwenye mahusiano na kuvumilia shida na tabu zote ilimradi pesa kwao inaingia.

3.Kuwa mwema kwa mwanamke kupitiliza siyo silaha ya kufanya mahusiano yenu yawe bora. Ukiwa mwema kupitiliza kwa mwanamke wako atafikiria kwa asilimia kubwa haustahili penzi lake.

Ukiwa na upendo kupitiliza kwa wanawake, watakuchukulia kama mtumwa, wachukulie wanawake kwenye mahusiano kama mashabiki zako au washikaji zako wa kiume atakuheshimu na heshima itakuwepo ndani ya penzi lenu.

Mwisho ukifanya utafiti mzuri kwenye mahusiano utagundua kuwa wanaume wazuri wenye nia njema na mahusiano ya kimapenzi na wanawake ndio wanaongoza kuumizwa moyo na kusalitiwa vibaya.

Hii ni kwa sababu wanaume hawa wanawekeza sana kwenye mahusiano mbele ya mwanamke mmoja anayempenda na kumuelewa. Hawatengenezi mbadala pembeni endapo siku mambo yakienda mlama.

Ila kwa wale wanaume wazee wa chapa ilale huwezi ukawakuta wanaumia moyo kisa wanawake. Mwanamke akimzingua anapiga chini kwa sababu anakuwa na machaguo mengi ya wanawake kwenye listi yake.

Huwezi ukawakuta wanaume maplay boy wanapoteza muda na kuhangaika na mwanamke mmoja maana wanajua vizuri huu mchezo wa mahusiano unavyochezwa .

NB:Anyway neno langu siyo sheria ukitaka fuata na usipotaka usifuate akili kichwani mwako wanaume wenzangu hasa kwenye mahusiano yenu na wanawake.👊
 
'Hii ni kwa sababu wanaume hawa wanawekeza sana kwenye mahusiano mbele ya mwanamke mmoja anayempenda na kumuelewa. Hawatengenezi mbadala pembeni endapo siku mambo yakienda mrama'.

Mtoa mada, naomba kufahamu hiyo hapo juu kama ina apply hadi kwa jinsia Ke ama ni kwa Me pekee yao ndiyo mambo huenda mrama..?
 
20240821_143829.jpg
 
'Hii ni kwa sababu wanaume hawa wanawekeza sana kwenye mahusiano mbele ya mwanamke mmoja anayempenda na kumuelewa. Hawatengenezi mbadala pembeni endapo siku mambo yakienda mrama'.

Mtoa mada, naomba kufahamu hiyo hapo juu kama ina apply hadi kwa jinsia Ke ama ni kwa Me pekee yao ndiyo mambo huenda mrama..?
Hapa tunalinda afya ya akili ya mwanamme
 
Back
Top Bottom