Makosa kadhaa katika kutoa Pepo (Exorcism). Mapepo/Majini hayaombewi yanafukuzwa

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,420
Reaction score
17,735
Kumekuwa na sintofahamu katika namna ya kushughulikia Hawa vibaraka wa ibirisi. Mapepo Kwa aina zake.

Makosa ambayo nayaona.

1: Watu wanaomba na mapepo, Tena wanapiga na Magoti na kufumba macho.
Hakuna hiyo scene kwenye maandiko. Hatuombei mapepo tunayafukuza. Yakikomaa na sisi tunakomaa Hadi yatoke. Hayo sio maombi Wala Dua.

2: Shetani ni muongo na Baba wa Uongo. Usifanyie kazi maneno yake. Ni Ukosefu wa maarifa kumpa maiki Pepo au kumchukua maelezo ili uyafanyie kazi kama facts. Hata Yesu alipohojiana nayo aliyaamuru tu yaende hakufanyia kazi maneno yao. Hata hivyo yalimdanganya, Mwanzoni yaliongea Kwa Umoja baadae yakasema ni mengi region. Na region ilikuwa ni kikosi Cha kijeshi Cha kirumi sio Cha kipepo.

3: Pepo hutolewa Kwa Imani katika Damu ya Yesu tu. Mganga hatoi Pepo anayapoza Kwa kuongezea mengine au kulibembeleza litulie kiaina, asiyemuamini Yesu kuwa ni Mungu aliyeumba Hadi hao Majini/mapepo yakaasi hatoi Pepo Bali anawapoza tu. Nabii potoshi katika UKRISTO pia hatoi Pepo Bali anafanya sanaa ndio maana linapodai limetoka ukikuta a na aliyesimama Kiroho litalipuka Tena.

3: Aliyepewa mamlaka ya kutoa Pepo sio Mchungaji,Mwinjilisti,Kasisi au nabii tu Bali Kila anayemuamini Yesu anapaswa kuogopwa na kufukuza Pepo popote atakapokutana nalo. Nii mamlaka ukiamini unayo unakuwa na superiority complex dhidi ya vimamlaka vyote vya Ibirisi.

4: Mapepo na wachawi wanapenda makanisa,familia au watu wanaoyatajataja na kuyapa airtime. Haya makanisa na familia tunayaita Satan conscious churches/Families. Kanisani au Familia ni Mahali pa kumsifu Mungu, kutaja uwezo wake, ikiwezekana Shetani asimbuliwe kabisa. Hilo kanisa/familia hailiwezi kusumbuliwa mara Kwa mara na nguvu za Giza maana hazijapewa nafasi. Mungu hukaa katikati ya sifa. Mahali ambapo Mungu anasifiwa na kutukuzwa Sana Shetani hakai. Ni suala la Muda tu atachikichia automatically bila kujua siku, saa Wala dakika atatafuta anakopendwa na kutajwatajwa.

5: Hakuna kitu Kinaitwa Territorial spirits. Kwamba Kuna kitengo maalumu Cha Majini au mapepo kinatawala eneo flani tuu. Mapepo ni universal. Sio watu Hadi useme wamefungwa kufanyia kazi sehemu flani tu. Hiyo elimu chanzo chake ni mapepo yenyewe ili kuteka fahamu za watu.

6: Huwezi kumuua Pepo/jini. Hizo elimu chanzo chake ni mapepo yenyewe. Shetani na Malaika wake watauliwa na Yesu siku ya mwisho. Kazi yetu ni kuyafukuza kwenye miili ya watu yasiwatese lakini yatabaki tu yanavizia nafasi hapo au Kwa mwingine.

Leo tuishie hapo.
Mafungu yatakuja Kwa watakaotaka fafanuzi.

Muebrania
Mitale na Midimu.
 
Binafsi naona wapo wateule maalum wa Mungu mwenyewe ambao huwaleta kwa ajili ya kuwakomboa watu wake kwenye vita ya kiroho.

Ukiangalia sasa hivi Makanisa ni mengi lakini waumini wake wamepigika kila aina ya majanga.
Zaid wanaendlea kukamuliwa sadaka na michango mbalimbali bila msaada.
 
Ni kweli, tunatatizo mahala
 
Pepo aka shetani hawezi kutoka kwa imani ya damu ya Yesu hata siku moja kama ndio hivyo imani yako inavyokwambia Pepo haogopi Damu ya Yesu .Pepo anatolewa kwa dawa maalum za kumfukuza pepo mchafu na ukipewa na kuzitumia atatoka pepo mchafu akitaka asitake. Kuna utaalam maalum wa kuweza kumtoa pepo ndani ya mwili wa mtu au ndani ya nyumba unapoishi sio kutumia imani yako ya damu ya Yesu eti pepo mchafu ataweza kutoka sio rahisi. Mimi ninakataa unavyosema.
 
Pepo aka shetani hawezi kutoka kw aimani ya damu ya Yesu hata siku moja kama ndio hivyo imani yako inavyokwambia Pepo haogopi Damu ya Yesu .Pepo anatolewa kwa dawa maalum za kumfukuza pepo mchafu na ukipewa na kuzitumia atatoka pepo mchafu akitaka asitake. Kuna utaalam maalum wakuwezakumtoa pepo ndani ya mwili wamtu au ndani ya nyumba unapoishi sio kutumia imani yako ya damu ay Yesu eti pepo mchafu ataweza kutoka sio rahisi. Mimi ninakataa unavyosema.
Asante Kwa kutumia uhuru wako wa kuchagua kukataa au kukubali.
Ila unabaki hauko sahihi Kwa Mujibu wa Imani kuhusu Mungu.

Kijadi hata Kwa kumcharaza fimbo mwenye Pepo Huwa wanaamini yanatoka. Naheshimu maoni yako ila hayako sahihi Kwa Mujibu wa maelezo ya bandiko hapo juu.
 
Mapepo uwakumba zaidi wanawake kwa sababu wanatumia vitu vyao mfano mawigi, vipodozi, make up, kucha kope bandia, suruari na mavazi ya kuzimu yanayoshawishi ngono. Huwezi kuta mwanamke asiyetumia vitu hivyo au anaevaa mavazi ya heshima akaanguka pepo. Bali waliovaa vitu vyao.
 
Usipige maombi ya kuondoa au kuvunja sijui kuharibu wachawi, mapepo nk ukivunja atarudi tena kesho. Piga maombi ya kuuwa kukata kichwa kuchoma mishale ya moto na kuteketeza kabisa kwa damu ya YESU, ayarudi tena na hata wenzake awawekukuchezea wanajua pale watakufa kama wenzao. Maombi utenda Kazi kabisa katika ulimwengu wa ROHO.
Mchawi atakiwi kuchekewa anatakiwa kuuliwa. Hukumu ya mchawi ni kifo Ili asiwadhuru wengine.
 
Out of faith (Me muumini Mzuri tu)
Nna swali hasa kwako mitale na midimu hiyo namba mbili wakristo wengi huwa wanaisema sana kuwa shetani alikuwa ni muongo na baba wa uongo hebu nipe aya yoyote ikimuonyesha shetani akisema uongo...

NB: Tafsiri ya uongo= kusemakitu kisichokuwa na ukweli
Mwanzo 2,3
Sentensi ya kwanza ya Shetani kurekodiwa katika maandiko ilikuwa ni uongo, na kutilia mashaka intergity ya Mungu.

Mungu. Hakika mtakufa, Shetani: Hamtakufa hakika.
 
Nashukuru Kwa response yako mkuu mitale na midimu ,
Bhasi ngoja nijaribu na mimi kujibu kwa ki "jielimu" changu kidogo nilichopataga cha theolojia ya maandiko matukufu.

Cha Kwanza Hautakuja kukuta kwenye Maandiko ya kale (Agano la kale) yoyote ushahidi wa kuonyesha hasa kosa la shetani ila utakuta shetani akitajwa kwenye vitabu vya agano jipya kama baba wa uongo na baba wa kila maovu
Sasa turejee Shida zote zilipoanzia (Kwa mujibu wa Biblia)

Nitarejea aya ulizotoa Mwanzo 2 na mwanzo 3 na nitazitumia hizohzo

Kipindi M/Mungu anawakabidhi Bustani ya Edeni aliwaambia nitanukuu Mwanzo 2:16,17

......Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika........

Mungu alimwambia Adam na Mkewe pindi atakapokula bhasi atakufa Ngoja niache lugha za kiswahili na kiinglishi nilichunguze neno la MUNGU kwa lugha Mama iliyoandkiwa Kihebrew
kauli inasema ..........
......בְּי֛וֹם אֲכָלְךָ֥ מִמֶּ֖נּוּ מ֥וֹת תָּמֽוּת......

Matamshi;
....Ba yo wm (Ba yaumi) mim men nu Mawt (mowt) Tamut....

Sasa tuone
maneno yaliyotumika... ba yawm ....Mawt tamut...
maneno haya yanamaanisha Siku hiyo hyo mtakayokula ndiyo siku mtakayokufa..... Ni onyo kali sana yani kwa mfano umwambie mtu ukinywa sumu tu umekufa asipokufa bhasi sumu haikuwa sumu...

turudi kwa shetani aliwaambia Adam na Eve
soma kwenye Mwanzo 3:4
........לֹֽא־מ֖וֹת תְּמֻתֽוּן.......

matamshi;
.........La mawt tamutun......

maana yake Hamtafikwa na Umauti au kifo siku hiyo.....
Na pia akawaambia kuwa mtakavyokula hamtakufa ila "mtafumbuliwa macho na mtakuwa na ufahamu nanyi mtakuwa kama mungu Kwa kujua mema na mabaya"

Yaliyotokea baada ya kula tunda

1.Ni kweli hawakufa siku hiyo kama alivyowaambia ila waliishi zaidi ya miaka 900 baada ya siku hiyo

2.Mungu alithibitisha kuwa kwa kula Tunda walikuwa Na ufahamu kama mmoja wao...Soma mwanzo 3:22....
....."Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya".....

biblia bado inamtaja shetani kama ni advocate wa Upande wa malalamiko yaani anashitaki watu kwa mwenyezi Mungu soma 1 petro 5:8, ufunuo 12:10
Neno mshitaki kwa asili linatokana na neno la Kiyunani “Kategoros” au “Kategor”ambalo kwa kiingereza ni “An accuiser”

pia shetani anatajwa kama Ni mtu anayeishi mbinguni au mtu anayehudhuria vikao vya mara kwa mara vya mbinguni.
soma Ayubu 1:6-11 pia soma Ayubu 2:1-5 Bilia inasema hivi “Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe?..........

Kitendo cha Mungu kumuuliza ulikwa wapi wewe ni kuonyesha ni mtu aliyetokea kuwepo hapo lakini hakuwepo......

Bado nasubiri jibu langu Mkuu
simtetei shetani ila najenga hoja juu ya Kitabu cha Biblia kuwa kimya juu ya Dhambi hasa ya shetan........

Mimi ni Muumini mzuri tu.....
 
M
Mapepo uwakumba zaidi wanawake kwa sababu wanatumia vitu vyao mfano mawigi, vipodozi, make up, kucha kope bandia, suruari na mavazi ya kuzimu yanayoshawishi ngono. Huwezi kuta mwanamke asiyetumia vitu hivyo au anaevaa mavazi ya heshima akaanguka pepo. Bali waliovaa vitu vyao.
mh, mbona kuna wanawake wanajifunika mpaka macho, lakini ndio wanaongoza kuwa na mapepo
 
Nashukuru Kwa response yako mkuu mitale na midimu ,
Bhasi ngoja nijaribu na mimi kujibu kwa ki "jielimu" changu kidogo nilichopataga cha theolojia ya maandiko matukufu.

Cha Kwanza Hautakuja kukuta kwenye Maandiko ya kale (Agano la kale) yoyote ushahidi wa kuonyesha hasa kosa la shetani ila utakuta shetani akitajwa kwenye vitabu vya agano jipya kama baba wa uongo na baba wa kila maovu
Sasa turejee Shida zote zilipoanzia (Kwa mujibu wa Biblia)

Nitarejea aya ulizotoa Mwanzo 2 na mwanzo 3 na nitazitumia hizohzo

Kipindi M/Mungu anawakabidhi Bustani ya Edeni aliwaambia nitanukuu Mwanzo 2:16,17

......Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika........

Mungu alimwambia Adam na Mkewe pindi atakapokula bhasi atakufa Ngoja niache lugha za kiswahili na kiinglishi nilichunguze neno la MUNGU kwa lugha Mama iliyoandkiwa Kihebrew
kauli inasema ..........
......בְּי֛וֹם אֲכָלְךָ֥ מִמֶּ֖נּוּ מ֥וֹת תָּמֽוּת......

Matamshi;
....Ba yo wm (Ba yaumi) mim men nu Mawt (mowt) Tamut....

Sasa tuone
maneno yaliyotumika... ba yawm ....Mawt tamut...
maneno haya yanamaanisha Siku hiyo hyo mtakayokula ndiyo siku mtakayokufa..... Ni onyo kali sana yani kwa mfano umwambie mtu ukinywa sumu tu umekufa asipokufa bhasi sumu haikuwa sumu...

turudi kwa shetani aliwaambia Adam na Eve
soma kwenye Mwanzo 3:4
........לֹֽא־מ֖וֹת תְּמֻתֽוּן.......

matamshi;
.........La mawt tamutun......

maana yake Hamtafikwa na Umauti au kifo siku hiyo.....
Na pia akawaambia kuwa mtakavyokula hamtakufa ila "mtafumbuliwa macho na mtakuwa na ufahamu nanyi mtakuwa kama mungu Kwa kujua mema na mabaya"

Yaliyotokea baada ya kula tunda

1.Ni kweli hawakufa siku hiyo kama alivyowaambia ila waliishi zaidi ya miaka 900 baada ya siku hiyo

2.Mungu alithibitisha kuwa kwa kula Tunda walikuwa Na ufahamu kama mmoja wao...Soma mwanzo 3:22....
....."Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya".....

biblia bado inamtaja shetani kama ni advocate wa Upande wa malalamiko yaani anashitaki watu kwa mwenyezi Mungu soma 1 petro 5:8, ufunuo 12:10
Neno mshitaki kwa asili linatokana na neno la Kiyunani “Kategoros” au “Kategor”ambalo kwa kiingereza ni “An accuiser”

pia shetani anatajwa kama Ni mtu anayeishi mbinguni au mtu anayehudhuria vikao vya mara kwa mara vya mbinguni.
soma Ayubu 1:6-11 pia soma Ayubu 2:1-5 Bilia inasema hivi “Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe?..........

Kitendo cha Mungu kumuuliza ulikwa wapi wewe ni kuonyesha ni mtu aliyetokea kuwepo hapo lakini hakuwepo......

Bado nasubiri jibu langu Mkuu
simtetei shetani ila najenga hoja juu ya Kitabu cha Biblia kuwa kimya juu ya Dhambi hasa ya shetan........

Mimi ni Muumini mzuri tu.....
Hv jamaa alikimbia ili mi nikujibu
 
Kumekuwa na sintofahamu katika namna ya kushughulikia Hawa vibaraka wa ibirisi. Mapepo Kwa aina zake.

Makosa ambayo nayaona.

1: Watu wanaomba na mapepo, Tena wanapiga na Magoti na kufumba macho.
Hakuna hiyo scene kwenye maandiko. Hatuombei mapepo tunayafukuza. Yakikomaa na sisi tunakomaa Hadi yatoke. Hayo sio maombi Wala Dua.

2: Shetani ni muongo na Baba wa Uongo. Usifanyie kazi maneno yake. Ni Ukosefu wa maarifa kumpa maiki Pepo au kumchukua maelezo ili uyafanyie kazi kama facts. Hata Yesu alipohojiana nayo aliyaamuru tu yaende hakufanyia kazi maneno yao. Hata hivyo yalimdanganya, Mwanzoni yaliongea Kwa Umoja baadae yakasema ni mengi region. Na region ilikuwa ni kikosi Cha kijeshi Cha kirumi sio Cha kipepo.

3: Pepo hutolewa Kwa Imani katika Damu ya Yesu tu. Mganga hatoi Pepo anayapoza Kwa kuongezea mengine au kulibembeleza litulie kiaina, asiyemuamini Yesu kuwa ni Mungu aliyeumba Hadi hao Majini/mapepo yakaasi hatoi Pepo Bali anawapoza tu. Nabii potoshi katika UKRISTO pia hatoi Pepo Bali anafanya sanaa ndio maana linapodai limetoka ukikuta a na aliyesimama Kiroho litalipuka Tena.

3: Aliyepewa mamlaka ya kutoa Pepo sio Mchungaji,Mwinjilisti,Kasisi au nabii tu Bali Kila anayemuamini Yesu anapaswa kuogopwa na kufukuza Pepo popote atakapokutana nalo. Nii mamlaka ukiamini unayo unakuwa na superiority complex dhidi ya vimamlaka vyote vya Ibirisi.

4: Mapepo na wachawi wanapenda makanisa,familia au watu wanaoyatajataja na kuyapa airtime. Haya makanisa na familia tunayaita Satan conscious churches/Families. Kanisani au Familia ni Mahali pa kumsifu Mungu, kutaja uwezo wake, ikiwezekana Shetani asimbuliwe kabisa. Hilo kanisa/familia hailiwezi kusumbuliwa mara Kwa mara na nguvu za Giza maana hazijapewa nafasi. Mungu hukaa katikati ya sifa. Mahali ambapo Mungu anasifiwa na kutukuzwa Sana Shetani hakai. Ni suala la Muda tu atachikichia automatically bila kujua siku, saa Wala dakika atatafuta anakopendwa na kutajwatajwa.

5: Hakuna kitu Kinaitwa Territorial spirits. Kwamba Kuna kitengo maalumu Cha Majini au mapepo kinatawala eneo flani tuu. Mapepo ni universal. Sio watu Hadi useme wamefungwa kufanyia kazi sehemu flani tu. Hiyo elimu chanzo chake ni mapepo yenyewe ili kuteka fahamu za watu.

6: Huwezi kumuua Pepo/jini. Hizo elimu chanzo chake ni mapepo yenyewe. Shetani na Malaika wake watauliwa na Yesu siku ya mwisho. Kazi yetu ni kuyafukuza kwenye miili ya watu yasiwatese lakini yatabaki tu yanavizia nafasi hapo au Kwa mwingine.

Leo tuishie hapo.
Mafungu yatakuja Kwa watakaotaka fafanuzi.

Muebrania
Mitale na Midimu.
Mkuu wewe umeongelea Exorcism ambayo ni tofauti na Deliverance.

Exorcism ni kumfukuza pepo toka kwa mtu, kitu au mahala, wakati Deliverance ni kitendo cha kumweka mtu huru.

Kwenye nguvu ama uwezo unaotumika kufukuza pepo unatoka kwenye vitu au vifaa vya dunia hii wakati kwenye deliverance, nguvu ama uwexo unatoka kwa Mungu.

Wanaofanya Exorcism wanaweza wakawa waamini au wasio waamini wa Yesu kristo wakati waamini wa Yesu Kristo pekee ndio hufanya deliverance.

Exorcism si sehemu ya agano jipya kwani Deliverance ndio theme kubwa ya agano jipya.

Exorcism hufanywa zaidi nje ya Ukristo na wale watu wa agano la kale. Katika ukristo hufanywa zaidi na Wakatoliki.

Ninaamini katika kuonesha mamlaka unapofukuza pepo. Ninaamini hupaswi kupiga goti unapofanya deliverance au exorcism. Ninaamini hupaswi kuomba kufukuza pepo bali kutumia mamlaka uliyonayo au uliyopewa;lakini kwa deliverance hata ukipiga goti; uwezo wa kumtoa pepo unatokana na mamlaka ya KiMungu uliyopewa kama mwamini, haijalishi umepiga goti au umesimama.
 
Sikupata jibu mkuu hebu nipe jibu
Zaburi 90:4 na 2Petr 3:8 Adamu alikufa ndani ya siku moja machoni pa Mungu. wapo aliofikisha miaka 1000 lakini Si Adam wala mkewe waliofikisha hio miaka.

1)kuhusu mwanzo 2:16,17 shetani alikua sahh kusema akila tunda atajua mema na mabaya ila hakua sahh kusema "Hakika hamtakufa" "Ye shall not surely Die". So kitendo cha shetani kukanusha kwamba hawatakufa tayari ni uwongo huo.
2)Kumbuka kwamba Mungu kama baba mwenye nyumba ana haki ya kuweka mipaka ndani ya nyumba yake. Mungu alipowaumba adam na hawa aliwaonyesha mpaka wake kwa kutowaruhusu kula yale matunda just to show loyalty to him lakini aliwapa kila kitu na uhuru wa kutosha. kitendo cha shetani kwenda kumshawishi Hawa then Adam ni kama alisema Mungu ni mbinafsi. lakini matokeo ya dhambi yao mpk leo wazao wake tunapambana nayo. what if wasingemsikiliza shetan? hapo ndipo tunasema shetani ni mwongo
3) Kuhusu kisa cha Ayubu kwenye masimulizi ya ayubu 1,2 lina uhusiano wa moja kwa moja na 1petr 5:8 na Ufunuo 12:10. katika hvyo visa chunguza vzuri ni kama shetani anamshtaki Ayubu kwa Mungu like Mungu anamlinda Ayubu na kumbariki bure tu ila akiruhusu ajaribiwe atamwacha Mungu. na wengi hapa hua wanachanganya mana katika kisa hicho aliyekua akijaribu utii wa Ayubu kwa Mungu ni shetani sio Mungu. hata aliposema bwana ametoa bwana ametwaa yeye pia hakujua kwamba ni shetani aliyekua akimjaribu na baadae alikuja kutubu dhambi yake soma Ayubu 42:3-6. ni kisa kizito na kirefu sana na kina mada nyingi mno nitachoka kuandika.. karibu
 
Sijui kitu, ila kwa jinsi ulivoandika nimeipenda.
Ni kama njia ya kumuelekea mungu ipo ndani ya himaya ya shetani!
 
But napo kwenye hili shetani alidhihirika kua mwongo coz Ayubu alivumilia majaribu mpaka mwisho na Mungu alirudisha mali na kumbariki mara dufu Ayubu tofauti na mwanzo. Kingine now shetani hana nafasi tena ya kwenda mbingunu coz alishatupwa duniani soma ufunuo 12:12
 
Back
Top Bottom