Nashukuru Kwa response yako mkuu
mitale na midimu ,
Bhasi ngoja nijaribu na mimi kujibu kwa ki "jielimu" changu kidogo nilichopataga cha theolojia ya maandiko matukufu.
Cha Kwanza Hautakuja kukuta kwenye Maandiko ya kale (Agano la kale) yoyote ushahidi wa kuonyesha hasa kosa la shetani ila utakuta shetani akitajwa kwenye vitabu vya agano jipya kama baba wa uongo na baba wa kila maovu
Sasa turejee Shida zote zilipoanzia (
Kwa mujibu wa Biblia)
Nitarejea aya ulizotoa Mwanzo 2 na mwanzo 3 na nitazitumia hizohzo
Kipindi M/Mungu anawakabidhi Bustani ya Edeni aliwaambia nitanukuu
Mwanzo 2:16,17
......
Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika........
Mungu alimwambia Adam na Mkewe pindi atakapokula bhasi atakufa Ngoja niache lugha za kiswahili na kiinglishi nilichunguze neno la MUNGU kwa lugha Mama iliyoandkiwa Kihebrew
kauli inasema ..........
......
בְּי֛וֹם אֲכָלְךָ֥ מִמֶּ֖נּוּ מ֥וֹת תָּמֽוּת......
Matamshi;
....
Ba yo wm (Ba yaumi) mim men nu Mawt (mowt) Tamut....
Sasa tuone
maneno yaliyotumika...
ba yawm ....Mawt tamut...
maneno haya yanamaanisha
Siku hiyo hyo mtakayokula ndiyo siku mtakayokufa..... Ni onyo kali sana yani kwa mfano umwambie mtu ukinywa sumu tu umekufa asipokufa bhasi sumu haikuwa sumu...
turudi kwa shetani aliwaambia Adam na Eve
soma kwenye Mwanzo 3:4
........לֹֽא־מ֖וֹת תְּמֻתֽוּן.......
matamshi;
.........
La mawt tamutun......
maana yake Hamtafikwa na Umauti au kifo siku hiyo.....
Na pia akawaambia kuwa mtakavyokula hamtakufa ila "
mtafumbuliwa macho na mtakuwa na ufahamu nanyi mtakuwa kama mungu Kwa kujua mema na mabaya"
Yaliyotokea baada ya kula tunda
1.
Ni kweli hawakufa siku hiyo kama alivyowaambia ila waliishi zaidi ya miaka 900 baada ya siku hiyo
2.Mungu alithibitisha kuwa kwa kula Tunda walikuwa Na ufahamu kama mmoja wao...Soma mwanzo 3:22....
....."
Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya".....
biblia bado inamtaja shetani kama ni advocate wa Upande wa malalamiko yaani anashitaki watu kwa mwenyezi Mungu soma 1 petro 5:8, ufunuo 12:10
Neno mshitaki kwa asili linatokana na neno la Kiyunani “Kategoros” au “Kategor”ambalo kwa kiingereza ni “An accuiser”
pia shetani anatajwa kama Ni mtu anayeishi mbinguni au mtu anayehudhuria vikao vya mara kwa mara vya mbinguni.
soma Ayubu 1:6-11 pia soma Ayubu 2:1-5 Bilia inasema hivi “Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe?..........
Kitendo cha Mungu kumuuliza ulikwa wapi wewe ni kuonyesha ni mtu aliyetokea kuwepo hapo lakini hakuwepo......
Bado nasubiri jibu langu Mkuu
simtetei shetani ila najenga hoja juu ya Kitabu cha Biblia kuwa kimya juu ya Dhambi hasa ya shetan........
Mimi ni Muumini mzuri tu.....