Makosa kadhaa katika kutoa Pepo (Exorcism). Mapepo/Majini hayaombewi yanafukuzwa

Makosa kadhaa katika kutoa Pepo (Exorcism). Mapepo/Majini hayaombewi yanafukuzwa

Usipige maombi ya kuondoa au kuvunja sijui kuharibu wachawi, mapepo nk ukivunja atarudi tena kesho. Piga maombi ya kuuwa kukata kichwa kuchoma mishale ya moto na kuteketeza kabisa kwa damu ya YESU, ayarudi tena na hata wenzake awawekukuchezea wanajua pale watakufa kama wenzao. Maombi utenda Kazi kabisa katika ulimwengu wa ROHO.
Mchawi atakiwi kuchekewa anatakiwa kuuliwa. Hukumu ya mchawi ni kifo Ili asiwadhuru wengine.
Haelewi anachoongea. Unajua hii tabia ya kuwasifia sifia waganga wa kienyeji waliomo humu jukwaani imewafanya baadhi ya watu wakawa wajinga.
 
Kumekuwa na sintofahamu katika namna ya kushughulikia Hawa vibaraka wa ibirisi. Mapepo Kwa aina zake.

Makosa ambayo nayaona.

1: Watu wanaomba na mapepo, Tena wanapiga na Magoti na kufumba macho.
Hakuna hiyo scene kwenye maandiko. Hatuombei mapepo tunayafukuza. Yakikomaa na sisi tunakomaa Hadi yatoke. Hayo sio maombi Wala Dua.

2: Shetani ni muongo na Baba wa Uongo. Usifanyie kazi maneno yake. Ni Ukosefu wa maarifa kumpa maiki Pepo au kumchukua maelezo ili uyafanyie kazi kama facts. Hata Yesu alipohojiana nayo aliyaamuru tu yaende hakufanyia kazi maneno yao. Hata hivyo yalimdanganya, Mwanzoni yaliongea Kwa Umoja baadae yakasema ni mengi region. Na region ilikuwa ni kikosi Cha kijeshi Cha kirumi sio Cha kipepo.

3: Pepo hutolewa Kwa Imani katika Damu ya Yesu tu. Mganga hatoi Pepo anayapoza Kwa kuongezea mengine au kulibembeleza litulie kiaina, asiyemuamini Yesu kuwa ni Mungu aliyeumba Hadi hao Majini/mapepo yakaasi hatoi Pepo Bali anawapoza tu. Nabii potoshi katika UKRISTO pia hatoi Pepo Bali anafanya sanaa ndio maana linapodai limetoka ukikuta a na aliyesimama Kiroho litalipuka Tena.

3: Aliyepewa mamlaka ya kutoa Pepo sio Mchungaji,Mwinjilisti,Kasisi au nabii tu Bali Kila anayemuamini Yesu anapaswa kuogopwa na kufukuza Pepo popote atakapokutana nalo. Nii mamlaka ukiamini unayo unakuwa na superiority complex dhidi ya vimamlaka vyote vya Ibirisi.

4: Mapepo na wachawi wanapenda makanisa,familia au watu wanaoyatajataja na kuyapa airtime. Haya makanisa na familia tunayaita Satan conscious churches/Families. Kanisani au Familia ni Mahali pa kumsifu Mungu, kutaja uwezo wake, ikiwezekana Shetani asimbuliwe kabisa. Hilo kanisa/familia hailiwezi kusumbuliwa mara Kwa mara na nguvu za Giza maana hazijapewa nafasi. Mungu hukaa katikati ya sifa. Mahali ambapo Mungu anasifiwa na kutukuzwa Sana Shetani hakai. Ni suala la Muda tu atachikichia automatically bila kujua siku, saa Wala dakika atatafuta anakopendwa na kutajwatajwa.


5: Hakuna kitu Kinaitwa Territorial spirits. Kwamba Kuna kitengo maalumu Cha Majini au mapepo kinatawala eneo flani tuu. Mapepo ni universal. Sio watu Hadi useme wamefungwa kufanyia kazi sehemu flani tu. Hiyo elimu chanzo chake ni mapepo yenyewe ili kuteka fahamu za watu.

6: Huwezi kumuua Pepo/jini. Hizo elimu chanzo chake ni mapepo yenyewe. Shetani na Malaika wake watauliwa na Yesu siku ya mwisho. Kazi yetu ni kuyafukuza kwenye miili ya watu yasiwatese lakini yatabaki tu yanavizia nafasi hapo au Kwa mwingine.


Leo tuishie hapo.
Mafungu yatakuja Kwa watakaotaka fafanuzi.

Muebrania
Mitale na Midimu.
Exactly
 
Pepo aka shetani hawezi kutoka kwa imani ya damu ya Yesu hata siku moja kama ndio hivyo imani yako inavyokwambia Pepo haogopi Damu ya Yesu .Pepo anatolewa kwa dawa maalum za kumfukuza pepo mchafu na ukipewa na kuzitumia atatoka pepo mchafu akitaka asitake. Kuna utaalam maalum wa kuweza kumtoa pepo ndani ya mwili wa mtu au ndani ya nyumba unapoishi sio kutumia imani yako ya damu ya Yesu eti pepo mchafu ataweza kutoka sio rahisi. Mimi ninakataa unavyosema.
Kama upo dar njoo ujionee ninavyoyafurumusha Kwa jina la Yesu iwe pepo,mini,au mzimu yaani ni chap Kwa haraka

Usipende kujifungia kwenye kibubu tembea uone na ujifunze Mengi mkuu
 
Uto
Mapepo uwakumba zaidi wanawake kwa sababu wanatumia vitu vyao mfano mawigi, vipodozi, make up, kucha kope bandia, suruari na mavazi ya kuzimu yanayoshawishi ngono. Huwezi kuta mwanamke asiyetumia vitu hivyo au anaevaa mavazi ya heshima akaanguka pepo. Bali waliovaa vitu vyao.
Utoto raha sana .mawigi hata ww waweza yatengeneza ni aidha nyuzi za kijijini kwenu za miti unazitreat .au unayeyusha hii mikospoya plastic unatengeneza.vipodozi ni matunda na magamba ya miti unaya choma kitaalamu .kuzimu panahusikaje???
 
Back
Top Bottom