Uchaguzi 2020 Makosa ya Lissu yanaweza kutumiwa na CCM kumzidi kete kisiasa


Umeongelea jambo la maana sana hapa. Lisu awe makini maana mapingamizi yapo na hakika hawatamuacha salama wakipata mwanya maadui zake.
 
Uchumi wako uko je
Maana unaweza kuta hata wewe kwenye familia yako ndo tatizo
Mkuu kwani wewe unaposikia kitu kinaitwa uchumi wa nchi huwa unaelewa nini?Ile USD 1080.00 iliyoifanya Tanzania iingie uchumi wa kati si makusanyo ya Kodi au pesa iliyotumika kutenga SGR bali wastani wa kipato changu na chako.Kwa hiyo kabla ya kuanza kushabikia na kuonesha ujinga wako,tafuta maarifa Kwanza ili ujue connection Kati ya serikali na mlo unaoweka mezani kwako Kila siku
 

Anapenda media sasa ni.lazima ajibu hoja, akigoma basi atakuwa anadharau vyombo vya habali, kinachotakiwa ni kuwajibu kama waalivyouliza kwani yeye si ni nimsomi bhana?
 
Ninekuuliza wewe binafisi mimi mipango yangu ya maisha nizaidi ya hiyo 1080 uliyo taja. Na maanisha mkuu anza kwenye familia yako ukiwa baba fara huwezi kuja kuwa kiongozi bora lazima uwe fara tu na kuona mapungufu ya wenzako tu.
 
CCM ni taasisi kubwa, hata hayo masuala ya katiba na haki za binadamu wapo wengi tu wenye kuweza kumzidi maarifa Lissu.

Ile hali ya u-taasisi inawazuia wataalam hao wasiongee bila ya kupata maelekezo kutoka kwa wakubwa wao.
Wale wanayopeleka nje yanakuwa tayari yamejadiliwa kwa kina ndani. Hawaropoki ovyo kufurahisha mashabiki bali ndio uelekeo wao.
 

aiseee..

sasa itakuwaje na wabongo wamezoea kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.!?

BTW kama anautaka urais afate huo ushauri...aweke chujio kwenye kauli
 
Sio makosa au mapungufu ya Lisu ni viongozi wana mkakati wa Chadema walitakiwa kujiandaa mapema tena ni rahisi sana kukosoa kuongozi alie madarakani lakini bado muda unatosha Chadema strategists warudi katika drawing board wafanye SWORT analysis na kutengeneza mkakati wa maeneo muhimu ya kuzingatiwa na mgombea wao jukwaani sio petty issues kama JPM ametoa rushwa ya laki 5 wakati umma unamjua JPM amepambana na grand corruption vizuri ingawa kunaweza kuwa na mapungufu, sio kusema TZ kuna Corona sana wakati sote tunajua katika vita ya Corona JPM aliipatia kiasi kikubwa ingawa kuna mapungufu kidogo pia
 
Wale wanayopeleka nje yanakuwa tayari yamejadiliwa kwa kina ndani. Hawaropoki ovyo kufurahisha mashabiki bali ndio uelekeo wao.
CCM wanaweza kudumu kwa miaka na miaka wakiongozwa na nidhamu. Wanajitahidi sana kupambana na zile 'ego' binafsi, wanautunza ule muundo mzima wa Chama, ambao wameurithi tangu enzi zile za kina Nyerere, Sozigwa na wanasiasa wengine wakongwe.
 
kutakuwa na mdahalo?
 
Mimi binafsi ninakuheshimu sana kwa michango yako pia na umri.
Katika hili umewahi sana kutoa hitimisho.
Nafikiri wakati sahihi wa kumwaga sera, mikakati nk bado muda wake...kama ni mvua hata mawingu bado kabisa.
Hii ya sasa ni amsha smsha tu.
 
Ninekuuliza wewe binafisi mimi mipango yangu ya maisha nizaidi ya hiyo 1080 uliyo taja. Na maanisha mkuu anza kwenye familia yako ukiwa baba fara huwezi kuja kuwa kiongozi bora lazima uwe fara tu na kuona mapungufu ya wenzako tu.
Kwa hiyo Kama wewe si fara huwezi kuona mapungufu wa wenzako? Wewe mipango yako ya maisha ni zaidi ya 1080 USD au kipato chako kwa sasa zaidi ya USD 1080.00? Fafanua kidogo.mimi Cha kwangu ni USD 57,000.00 kwa mwaka na hali yangu mbaya sana
 
Siko tofauti na mleta mada ninachokisema hapa ni kwamba hakuna mtu aliyekamilika hapa duniani kwa kuwa wote ni binadamu,isipokuwa tunakamilishwa kwa kushauriana na kupokea ushauri wa mwenzako aliyekamilika katika lile ambalo unamapungufu nalo.

Hata wale ambao hatuko tayari kumpa kura zetu Magufuli hatuna maana kuwa Magufuli hajafanya kitu chochote,amefanya mengi mazuri na amefanya mengi mabaya kama binadamu,tatizo linakuja ni pale ambapo kuna watu wanajifanya ni kama malaika ambao hawakosei wakati ni wanadamu wanaokosea kama wengine.

Kitu ambacho Lissu anatakiwa aepukane nacho kwa kupokea ushauri mzuri unaotolewa kwake na wenzake kama ushauri wa mleta mada.
 
Ushauri murua kabisa, pia kitengo cha habari chadema kiamuke. Rafiki yangu na classmate wangu Tumaini Makene hili linakuhusu. Nilishangaa mkutano mkuu wa chadema kuturushwa full kwenye online chadema media TV, badala yake tukawa tunapata kupitia Dar mpya na mwananchi online, ambayo ili kuwa censored.
 
Una akili sana
Kama atapita atajifunza kitu hasa kujenga hoja ili watanzania wamuelewe
 
Kwa hiyo Kama wewe si fara huwezi kuona mapungufu wa wenzako? Wewe mipango yako ya maisha ni zaidi ya 1080 USD au kipato chako kwa sasa zaidi ya USD 1080.00? Fafanua kidogo.mimi Cha kwangu ni USD 57,000.00 kwa mwaka na hali yangu mbaya sana
Hahaha pambana sana ufiki USD 100000.
 
Umate mate muhimu sana kipindi cha kampeni. Lissu hajafanya kazi tangu avamiwe kule Dodoma hana mpunga.
 
Nakupa 'A top for Good thinking' breaking is very important before change down 'unapotaka kushusha abiria tumia breki kabla huja badili gia ili abiria wasije wakadondoka'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…