Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Humu jf kuna bifu kati ya mashabiki wa Freeman Mbowe na Tundu Lissu na machawa wa pande zote. Wengi ima hawajui mchezo wa siasa au hawana hata chembe juu ya demokrasia. Chadema, tofauti na CCM ni chama cha kila mmoja. Hivyo, wawili hawa wanapopambana kugombea uenyekiti si tatizo. Siyo sawa na maccm ambayo mwenyekiti wao hajawahi kupigiwa kura popote zaidi ya kutegemea mkono wa Mungu. Hivyo, wanaoona kuwa kuna uhasama kati ya Mbowe na lissu waache siasa na demokrasia vichukue mkondo wake.