Wala hainikeri..
Nadhani wenyewe wakifufuka watashangaa sana hizi habari zako wao walipambana na wakoloni kama watanganyika.. hainalishi alikuwa shekhe au nani?
Walichotanguliza kikubwa ni uzalendo wao kwa nchi/ardhi yao ya MAMA Tanganyika.
Inside...
Unazungumza na Mohamed Said.
Mimi ni mjukuu wa Salum Abdallah Popo muasisi wa TANU 1954 na Tanganyika Railways African Union (TRAU) 1955.
Babu yangu kapigania uhuru wa Tanganyika kwa hali na mali.
Kaongoza General Strike mwaka wa 1947, 1949 na 1960.
Aliwekwa kizuizini mwaka wa 1964 baada ya maasi ya Tanganyika Rifles.
Unazungumza na Mohamed Said.
Naijua vizuri historia ya uhuru kwa kuwa ni sehemu ya maisha ya wazee wangu.
Mimi nimesoma Nyaraza za Sykes nilizokabidhiwa na Ally Sykes na nimeandika kitabu kilichosahihisha historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Ally Sykes kadi yake ya TANU ni No. 2.
Abdul Sykes kaka yake kadi yake ya TANU ni No. 3.
Kadi ya TANU ya Julius Nyerere ni No. 1.
Kadi ya Nyerere imetolewa na Ally Sykes na ina sahihi yake.
Abdul Sykes, Ally Sykes na Julius Nyerere ndiyo waliosajili chama cha TANU na wanachama wa mwanzo walitoka Rufiji na walipewa kadi zao na Mzee Said Chamwenyewe.
Hawa wanachama walikuwa muridi wa Qadiriyya na Khalifa wao alikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir.
Hawa kama kushangaa watakushagaa wewe kwani hawakujui huwajui.
Na Ally Sykes Muthaiga Club, Nairobi 1989