Makubaliano Kati ya Tanzania na Dubai ni Batili kwenye sheria za kimataifa

Makubaliano Kati ya Tanzania na Dubai ni Batili kwenye sheria za kimataifa

Uzumbukuku Kwa Sisi watanzania Kwa sababu hatuna kampuni kama hiyo?
Mbona kampuni hiyo IPO USA, UK, ujerumani na China?
Hizo nchi nazo mazumbukuku au unaongea kitu hukijui??
Missunderstand!


Sisi tunapambana kuuza nchi/ tena sector nyeti kabisa, badala ya kua na vyombo/kampuni kama hizo ili na sisi tufanye uharamia kama huo kwingine
 
Umechelewa. Hakuna awezaye kuhoji tena huo mkataba baada ya bunge letu tukufu kuridhia.
Bunge limeridhia mkataba au makubaliano?. Kasome Geneva Convention on the Law of Treaties uone grounds za kuinvalidate mkataba wa kimataifa. Moja wapo ni error.

Kwa mujibu wa ibara ya pili ya Montevideo Convention ya mwaka 1933, nchi ikiwa shirikisho Basi kinachotambulika Kama legal person ni ile shirikisho sio washirika wa shirikisho. Hivyo ground yangu ya kwanza ni hiyo.
 
Mkataba Kati ya serikali ya Tanzania na Dubai ni batili kwenye sheria za kimataifa. Maana ya kwamba Dubai sio sovereign state Kama jamhuri ya muungano wa Tanzania, hivyo haiwezi kuingia mikataba ya kimataifa.

Mikataba ya kimataifa inaingiwa na Falme ya Kiarabu inayotambulika kwenye sheria za kimataifa na sio Dubai ambayo ni sehemu ya UAE.

Hivyo naenda mahakamani kupinga mkataba huo au makubaliano hayo.
Nakusapoti kwa 100% ukihitaji mchango nipo tayari kutembeza bakuli nchi nzima
 
Umesoma Katiba ya U.A.E.?
Icheki Google uisome uone powers za Emirates zikoje.

Mtahangaika mpaka mtage wallahi!
 
Wanaoingia Ubia ni DP World na TPA.

Siyo nchi ya Dubai. Ni kampuni inayomilikiwa na serikali yake.

Usijisumbue.
Yuko sahihi Kuna mkataba wa mashirikiano ambao ulisainiwa na waziri wa ujenzi na viongozi wa Dubai. Kike kilichokuwa kinajadiliwa bungeni Leo ni MOU" Yani hati ya maridhiano

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Kisheria lazima uingie mkataba na competent party, ndio maana sheria ya mikataba inakataza kuingia mkataba na mto au mtu mwenye shida ya akili. Sasa kwenye sheria ya kimataifa unaingia mikataba wa kimataifa baina ya sovereign states, Sasa Dubai sio sovereign state kama Kenya ama Uganda, hapo tunafanyaje.
 
Sisi tupo huku bukene tabora hata hatujui kinachoendelea
 
Umesoma Katiba ya U.A.E.?
Icheki Google uisome uone powers za Emirates zikoje.

Mtahangaika mpaka mtage wallahi!
Hiyo ni katiba ya united Arab Emirates na siyo ya Dubai... Dubai sio nchi ni capital city (Hapa nisahishwe kama nimekosea). Dubai ni tofauti kabisa na Vatican ambayo ni nchi ndani ya nchi.

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Hapana, kwa sheria mama ya mikataba ya kimataifa ya Geneva Convention on the Law of Treaties ya mwaka 1969, bado naruhusiwa kuchallenge huo mkataba maana ni batili.
Tunakutakia mafanikio msomi Keyboard lawyer
 
Back
Top Bottom