DOKEZO Makumbusho: Polisi wadaiwa kuvamia Ofisi za "Reachout Tanzania", wakidai kumtafuta Wakili Lusako Alphonce, ambaye hakuwa ofisini

DOKEZO Makumbusho: Polisi wadaiwa kuvamia Ofisi za "Reachout Tanzania", wakidai kumtafuta Wakili Lusako Alphonce, ambaye hakuwa ofisini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ni ukweli unaousema sasa wao hao Chama A kwanini wanaogopa kuambiwa ukweli huo kuhusu suala la ajira? Of course yes majority vijana wengi hawana ajira sasa wao wakiambiwa hivyo si inabidi watafute ufumbuzi kwanini waogope kuambiwa ukweli?
🤣 ccm hawana suluhisho la ukosefu wa ajira kwa vijana. Suluhisho walionalo ni kuwashughulikia watu wenye mdomo mdomo kuhusu ukosefu wa ajira 🤣 yaani wanahofu juu ya umaarufu na ushawishi wa hao watu usije ukatumika kuchochea watu kuitoa ccm madarakani kwenye uchaguzi 🤣 au kwa maandamano makubwa mpaka ikulu 🤣🤣
 
Hiki kitu kikiendelea ,kuna siku hao askari watachomwa moto na wananchi mimi nashauri mkuu wa polisi au Usalama ambako hao vijana wanatoka wawe makini kwa kuwa wanafanya vitu mchana kweupe kama vile uhai wa wananchi wanaweza kuufanyia kitu chochote wakati wowote hasa ukiwa upinzani.Ila namshauri RAIS Kama Mama "UCHUNGU WA KUZAA TUNAUJUA SISI" Iko siku itampata mtu wake wa karibu ndio tumbo la uzazi litamwuma zaidi.KIROO sasa ,damu za watu lazima zilete laana juu ya utawala na nchi .Magufuli azingekufa mapema na kwa mateso yale kama asingemwaga damu hebu mwone JK anavyuishi kwa raha au Mwinyi (RIP).Mimi nimeomba sana Mungu mtoto wangu asiingie kwenye kitu kinaitwa askari au usalama ,please sitaki laana kwa kizazi changu aisee.Na kwa sasa sina mtu anafanya kazi serikalini kwenye blood line yangu -asante Mungu kwa hilo
 
Video ya watu waliojitambulisha kuwa ni Askari Polisi wakivamia ofisi za Taasisi ya Reachout Tanzania zilizopo eneo la Makumbusho jijini Dar es Salaam, wakimtafuta Mwanasheria wa taasisi hiyo, Lusako Alphonce

Inaelezwa watu hao walifika wakiwa katika kundi kubwa ambapo wenye mitutu ya bunduki walibaki nje kwenye gari (hawaonekani kwenye CCTV), na wawili wenye bastola waliingia ndani kumsaka Lusako, kama walivyonaswa kwenye camera.!

Pia, Soma: Polisi wadaiwa kuvamia Ofisi za Reachout Tanzania Makumbusho, wakidai kumtafuta Lusako Alphonce, ambaye hakuwa ofisini
Screenshot 2024-12-05 131522.png

Polisi hawakufuati tu bila tatizo,kuna kitu lusako kafanya
Utakua unaota wewe, au hujawahi kuishi Tanzania. Soma chini hapo uone maafisa wa polisi tena wakiwa na vyeo vikubwa walipoenda kumkamata na kumuua mfanyabiashara na kuchukua pesa zake.
Sasa hivi wote wapo jela
 
Mbona habari haieleweki? Kamilisha taarifa
 
Kuna Video nimekutana nayo ya Mtu anayedaiwa kuwa ni Advocate Alphonce Lusako Akiwa ankimbizwa na watu ambao inasemekana na Watekaji wengine.Mwenye Taarifa Atujuze
 
Video ya watu waliojitambulisha kuwa ni Askari Polisi wakivamia ofisi za Taasisi ya Reachout Tanzania zilizopo eneo la Makumbusho jijini Dar es Salaam, wakimtafuta Mwanasheria wa taasisi hiyo, Lusako Alphonce

Inaelezwa watu hao walifika wakiwa katika kundi kubwa ambapo wenye mitutu ya bunduki walibaki nje kwenye gari (hawaonekani kwenye CCTV), na wawili wenye bastola waliingia ndani kumsaka Lusako, kama walivyonaswa kwenye camera.!

Pia, Soma: Polisi wadaiwa kuvamia Ofisi za Reachout Tanzania Makumbusho, wakidai kumtafuta Lusako Alphonce, ambaye hakuwa ofisini
Anayewafahamu hawa awataje kwa majina ili Wazazi wao wafahamu kwamba walizaa Watekaji
 
Nafikiri sasa ni wasaa serikali iidhinishe kutokuwa mwaccm, mkosoaji, na mtoa maoni tofauti na utawala ni kosa.

Ili watu wale sahani moja na polisi tuone kama kukosekana kwa order ndio njia sahihi ya kuendesha nchi.
 
Back
Top Bottom