DOKEZO Makumbusho: Polisi wadaiwa kuvamia Ofisi za "Reachout Tanzania", wakidai kumtafuta Wakili Lusako Alphonce, ambaye hakuwa ofisini

DOKEZO Makumbusho: Polisi wadaiwa kuvamia Ofisi za "Reachout Tanzania", wakidai kumtafuta Wakili Lusako Alphonce, ambaye hakuwa ofisini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Utakua unaota wewe, au hujawahi kuishi Tanzania. Soma chini hapo uone maafisa wa polisi tena wakiwa na vyeo vikubwa walipoenda kumkamata na kumuua mfanyabiashara na kuchukua pesa zake.
Sasa hivi wote wapo jela
Tofauti hiyo,najua utaniletea ya zombe pia, polisi na uniform kukufuata ofisini ni very official,kuna kitu
 
Sawa kuna kitu kafanya sasa ndiyo wamfuate na zana za kivita? Kwamba Lusako atawashambulia kwa zana kama hizo? Kwamba wangemuita aripoti kituo cha polisi angekimbia?
Kawaida polisi kufuata wahalifu na mijegeje na kupigwa jeki,
 
ila hii nchi ingekuwa Ina fata Sheria, hao askari wange koma Sana.

hivi ujasiri wa kuvamia ofisi ya mtu na silaha una utoa wapi???.
Kuna wengine wana presha, mtu afe kisa kihoro sijui wata sema nini.
Wanatupeleka kuwa kama Mexico hawa

Ova
 
Watanzania ndiyo hawana nguvu msikimbilie kusema hakuna upinzani wenye nguvu.

Juzi Nondo katekwa hadharani nani alipambana kuzuia asitekwe?
Wahuni wamehodhi vyama vyote vya siasa. Wote ni CCM.

Unafikiri ungetokea upinzani wa ukweli kama Mtikila, Chadema ya Dr Slaa kabla ya 2015. Upinzani ungechukua nchi.

Wananchi wanajua CCM sio wazuri ila hakuna alternative.
 
Kutukana sio kukosoa.Kutukana ni kosa la jinai.Unapojifanya mwamba unapotukana ukijiwa ili uwekwe mbaroni endelea na umwamba wacha kulia kulia kama kigoli.
Lusako ametukana kumbe!
 
Utakua unaota wewe, au hujawahi kuishi Tanzania. Soma chini hapo uone maafisa wa polisi tena wakiwa na vyeo vikubwa walipoenda kumkamata na kumuua mfanyabiashara na kuchukua pesa zake.
Sasa hivi wote wapo jela
Huyo ni mpuuzi kama sio mpumb.
 
Hahaha. Umenikumbusha kisa cha coplo Abdul yule wa oysterbay aliyewahi kufyatua risasi 3 mbele ya ADAM MALIMA.alijinasibu kwamba amevaa mkanda wenye rangi za bendera ya taifa. Sirro akasema ni sahihi kwa afande kufanya vile.
Malima akafikishwa mahakamani wakati kesi inaendelea malima akateuliwa na JPM kuwa RC mara.
Yule afande akiwa bado anakula vumbi kwenye lindo na doria
HaHaha
 
Polisi wenye silaha wadaiwa kuvamia ofisi za Taasisi ya Reachout Tanzania zilizopo maeneo ya Makumbusho jijini Dar es Salaam, wakidai kumtafuta Mwanasheria wao Lusako Alphonce, ambaye hakuwa ofisini. Polisi hao, wakiwa na sare na wengine hawana sare, walitishia kuvunja milango licha ya kuambiwa kuwa Lusako hayupo. CCTV camera za taasisi hiyo zimenasa tukio hilo.
View attachment 3169416
View attachment 3169418
Hii ni sauti inayosambaa mitandaoni inayodaiwa kuwa ni ya Lusako Alphonce, akiota taarifa za kuhofia kutekwa
View attachment 3169417
View attachment 3169538
Mzee Warioba kuyakemea jana leo wanataka kuonyesha kuwa wao hawajali mtu yeyote zaidi ya Samia
 
Naona utaratibu wa maisha umebadilika sana ......protocols zipo..kwa nini hazifuatwi....kama huyu kijana inaonekana ana ofisi hapo..hiyo ni adress tosha...kwa nini usitumiwe wito rasmi na ukizingatia ni mwanasheria?...kwa nini unataka kumchukua kwa staili hiyo?...kwa kifupi unataka kumfanya kitu kibaya.
Nchi ina utaratibu tena mzuri tu, lakini niwakumbushe tu wenye mamlaka
Kuna kitu kinajengeka kupitia staili hii..
Hawa wananchi wanawatazama tu..walioweka hizo protocols walikuwa very smart kuliko watu wanavyofikiria.
Muda ni mwalimu mzuri sana.
 
Back
Top Bottom