Makundi 4 ya Watanzania waliobaki Njiapanda baada ya Hotuba ya Rais Samia ya Aprili 22, 2021

Makundi 4 ya Watanzania waliobaki Njiapanda baada ya Hotuba ya Rais Samia ya Aprili 22, 2021

Mkaruka

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
19,629
Reaction score
34,199
Hotuba ya Rais Samia hapo jana imeacha watu wengi nija panda. Binafsi naona kama ililenga zaidi kuyapooza makundi yaliyokuwa yanapiga kelele kama:
  • Vyama vya upinzani
  • Team Magufuli
  • Wafanyabiashara
Wananchi wengine kiukweli tumebaki njiapanda, maana hatujui ni upi uelekeo wa Rais hasa unapohusisha makundi yafuatayo:

( Ifahamike kuwa watanzania wengi hawana vyama na siyo wafuasi wa vyama vya siasa)

1- Waliodhulumiwa, kuteswa, kutekwa, kupotea na kuumizwa na awamu ya 5

Je, waliopoteza ndugu zao wakubali matokeo, wazike migomba tu mambo yaishe??

2- Vijana wasio na ajira (Jobless)

Hapa sina maana serikali inaweza kuajiri kila mtu, ila unaposhindwa kuajiri kabisa na wakati huo huo unataka kila kitu kifanywe na serikali hilo ni janga kubwa.

3- Wazee wa mafao na kikokotoo.

Hapa mwelekeo ni upi maana sheria ya kikotoo bado ipo?

Fao la kujitoa vipi?

4- Watanzania waliokimbia nchi ( exiled ).

Hawa hawana uhakika na usalama wao, maana waliowaumiza mpaka leo bado wapo wanadunda na hakuna jipya lolote.

Je, waendelee kubaki huko waliko au warudi nyumbani?

Ni nini mtazamo wako?
 
Hotuba ya Jana, Kwangu mimi haikuwa na mambo yanayotuhusu wananchi moja kwa moja bali mambo ya Kitaifa zaid yaani Kuzungumzia miradi mikubwa bila kuzungumzia mqmbo yanayowagusa wananchi moja kwa moja
Exactly, hotuba ya jana nadhani ililenga zaidi kutafuta mwafaka na wanasiasa wanapiga kelele kuhusu legacy ya Magu, vyama vya upinzani pamoja na wafanyabiashara.

Haikuwa na jipya kwa Mtanzania wa kawaida.
 
Pigeni kazi wazee mama yupo Safi tu , hutuba ya Jan ya kiungwana snaa
 
Nimekuelewa kote kasoro hapo kwenye timu Magufuli, hao watu ni wakina nani haswa? binafsi siamini kama wana exist.

Wanachama wa CCM wengi ni bendera fuata upepo, leo wote watacheza ngoma ya Samia kwasababu wanachotaka wao ni matumbo yao yajae, so yeyote atakayekuwa juu regardless ya tabia zake watamsapoti tu.

Next time akitokea Magufuli mwingine huko mbele ya safari nae atapata mashabiki wake vilevile, mwenyekiti wa chama chao ndie anashikilia hatma ya wengi wao hasa uwepo wao kule bungeni, lazima wajipendekeze kwake tu.
 
Kuhusu 1. Hiyo ni system ambayo ni mwendelezo ili CCM iwepo madarakani, sioni kwa nini aongelee wakati naye najua wazi kuwa baada ya hii miaka mitano, atataka miaka 10 mingine ambayo ni yake, lazima ajizatiti aendeleze system ili CCM and the gang iendelee kutawala.
Atafanyaje hatujui.

Kuhusu 2. Private sector kaongelea kirefu sana pamoja na kilimo, mining, nk, lakini yote uongelewa, mambo yapo palepale, anayeongea ni CCM, Na CCM wanajulikana kwa nadharia, empty talk.
 
Tusubiri keshokutwa Siku ya Muungano na May Mosi. Huenda tukaona kwa vitendo. Je ataweza kuwaleta Watz pamoja kwenye shughuli za Kitaifa?? Je Wafanyakazi watatabasamu??
 
Back
Top Bottom