Kinuju
JF-Expert Member
- Mar 20, 2021
- 2,386
- 5,325
Tangu lini Nyumbu wakamtakia mema rais Samia hadi wampangie cha kufanya?Hotuba ya Rais Samia hapo jana imeacha watu wengi nija panda. Binafsi naona kama ililenga zaidi kuyapooza makundi yaliyokuwa yanapiga kelele kama:
Wananchi wengine kiukweli tumebaki njiapanda, maana hatujui ni upi uelekeo wa Rais hasa unapohusisha makundi yafuatayo:
- Vyama vya upinzani
- Team Magufuli
- Wafanyabiashara
( Ifahamike kuwa watanzania wengi hawana vyama na siyo wafuasi wa vyama vya siasa)
1- Waliodhulumiwa, kuteswa, kutekwa, kupotea na kuumizwa na awamu ya 5
Je, waliopoteza ndugu zao wakubali matokeo, wazike migomba tu mambo yaishe??
2- Vijana wasio na ajira (Jobless)
Hapa sina maana serikali inaweza kuajiri kila mtu, ila unaposhindwa kuajiri kabisa na wakati huo huo unataka kila kitu kifanywe na serikali hilo ni janga kubwa.
3- Wazee wa mafao na kikokotoo.
Hapa mwelekeo ni upi maana sheria ya kikotoo bado ipo?
Fao la kujitoa vipi?
4- Watanzania waliokimbia nchi ( exiled ).
Hawa hawana uhakika na usalama wao, maana waliowaumiza mpaka leo bado wapo wanadunda na hakuna jipya lolote.
Je, waendelee kubaki huko waliko au warudi nyumbani?
Ni nini mtazamo wako?
Hangaikeni na mzee wa MIGA mtetezi wa mashoga.