Makundi 4 ya Watanzania waliobaki Njiapanda baada ya Hotuba ya Rais Samia ya Aprili 22, 2021

Team Magufuli wapo! Na bado wana nguvu sana kiasi cha mama kutumia dk za kutosha tu kwenye hotuba yake kuwaonesha yuko pamoja nao.

Kiongozi wao ni yule mtu muongo waliyempigia sana makofi ile jana.
 
4- Watanzania waliokimbia nchi ( exiled ).
hivi unaweza kusema lema kakimbia nchi kwa kuogopa nini alikuwa na impact gani kwa taifa mpaka akimbie huyo ni mhuni anataka sifa za kuitwa et mkimbizi wa kisiasa aseme alichokikimbia ni nini anamwogopa nani
 
hivi unaweza kusema lema kakimbia nchi kwa kuogopa nini alikuwa na impact gani kwa taifa mpaka akimbie huyo ni mhuni anataka sifa za kuitwa et mkimbizi wa kisiasa aseme alichokikimbia ni nini anamwogopa nani
Ukiachana na Lema, kuna matukio ya kutisha sana yametokea ndani ya taifa hili.

  • Azory Gwanda
  • Tundu Lissu
  • Ben Saanane
  • Lwajabe
  • Kanguye

Na waliokuwa wanawatishia maisha na kuwafanyia unyama mpaka leo wapo, na wana madaraka vile vile!
 
Fuatilia bunge ndio utajua.

Kuna wanasiasa wanahisi legacy ( hapa wana maana yale mazuri ya Magufuli ) inahujumiwa.

Na hili limekolezwa baada ya report ya CAG kutoka.
🤣 🤣 🤣 🤣 ni shida kubwa kuwabadili mawazo
 
CHADEMA wamejipinga kuunga mkono uzi,uzi wenyewe ni upupu tu! Ahahahahaha.
 
Lakini hotuba yake bungeni ndio huo uekekeo wa serikali yake.

Kwahiyo hakuna hotuba kubwa kuzidi hiyo.
Hivyo ndio inavyopaswa kuwa, lakini kwenye uhalisia ni tofauti kabisa. Hapa kwetu rais hutekeleza mambo yake kutokana na upepo, ukibadili tu mwelekeo, na yeye anabadilika.
 
Yeye alijua lazima atapitishwa tu, huyu hajiamini ndio maana kila wakati anaongelea swala la kuaminiwa

Kimsingi Magufuli hakuwa anategemea kura toka kwa yoyote, ili mradi ana madaraka basi. Kwake yeye madaraka ilikuwa kila kitu, tena kwa katiba mbovu kama hii, alikuwa anaweza kupanga atakacho bila kujali utaratibu ukoje.
 
Hotuba ninzuri tu, imejikita kuwahakikishia wananchi kwamba uchumi wa nchi utaendelea kukua hasa kwa kuhakikisha miradi yote mikubwa kama umeme, reli, usafiri wa anga, nk,nk,
Pia swala la amani nautulivu pia vitalindwa ipasavyo.

Binafsi naona hayoyote yatawezekana.

Wanao sema ccm niileile wakituliza vichwa wakaangalia utendaji wa Hayati Magu watagundua aliacha fundisho kwamba unaweza kuwa ndani ya ccm na bado unaweza ukafanya vizuri kwa kupambana na wahujumu uchumi hatakama ni makada vigogo.

Na Mama amesema maono na mipango aliokuwanayo Magu hajaendanayo imebakihapa na inafanyiwa kazi kasema moto niule ule.
Binafsi nimefurahi alipo toa onyo kwa wahujumu uchumi maana hawa miakayote ndio walikuwa wana turudisha nyuma.

Lat's keep on wait and see.
 
Fuatilia bunge ndio utajua.

Kuna wanasiasa wanahisi legacy ( hapa wana maana yale mazuri ya Magufuli ) inahujumiwa.

Na hili limekolezwa baada ya report ya CAG kutoka.
Wanapima upepo ili watege vizuri
 
ni mpuuzi wa maisha tu ndie atakaye tegemea la maana kutoka CCM
 
Jambo la muhimu ni kwamba hofu na giza la awamu iliyopita havitakuwepo ila CCM ni ile ile
 
Binafsi yangu,,niko njia panda,,,ila ngoja tuone.
 
Hotuba ya Jana, Kwangu mimi haikuwa na mambo yanayotuhusu wananchi moja kwa moja bali mambo ya Kitaifa zaid yaani Kuzungumzia miradi mikubwa bila kuzungumzia mqmbo yanayowagusa wananchi moja kwa moja
Kwa akili yako miradi mikubwa kama bwawa la umeme halikugusi!!!?
au nyie ndio lile kundi ambalo mnaamini uongozi ukibadilika mtakuwa mnaokota pesa barabarani!!??
 
Moto unabaki uleule. Mgawanyiko, hasira na chuki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…