Makundi ya haki za Binadamu ya Israel yatoa ripoti kuilaani serikali yao kwa Mauaji ya Kimbari(Genocide) huko Gaza

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
17,047
Reaction score
63,206
Baada ya taatifa ya taasisi ya haki za binadamu ya Amnesty ya miezi michache iliyopita, taasisi ya haki za binadamu ya nchini Israel ya B'Tselem nayo imetoa taarifa kuwa wamejiridhisha vya kutosha kuwa serikali ya nchi yao inafanya mauaji ya Kimbari huko Gaza.
Wakihojiwa na mwandishi wa habari nguli Christine Amanpour wa CNN, wamesema kuwa wanasikitishwa sana kuona kuwa wamefika katika hatua ambayo ni dhahiri hawawezi kuukataa ukweli kuwa yanayoendelea Gaza ni mauaji ya Kimbari.

Unaweza kupata Interview yao kamili hapa:


View: https://youtu.be/kNJbNCCejvg?si=ZGi1w5zr-3vKPOO4
 
Hamas si waachie mateka wa Israel vita iishie sasa bado wanawashikilia huku wanauliwa ndo nini
 
Hamas si waachie mateka wa Israel vita iishie sasa bado wanawashikilia huku wanauliwa ndo nini

Israel ina mateka wa Kipalestina wengi zaidi kuliko hao Mateka ambao HAMAS imewashikilia.

By the way, Serikali ya Netanyahu inakataa kila dili ambalo HAMAS wako tayari kuachia mateka, lengo ni Israel iendelee kuwatumia msteka kama excuse ya kukamilisha agenda yao ya kuwafukuza wapalestina Gaza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…