Makundi ya vijana wa Kitanzania ambao hujihisi wameyapatia maisha


Hilo la followers wa twitter linatesa wengi sana,

Acc yangu ya twitter ina miaka kama nane sasa na nina-followers kama 50 and I don’t give a dammm

Sio faida ya kuwa na followers kibao halafu hata chenji hainipi.

Kama nafanya biashara sawa otherwise ni upuuzi tu.
 
.................Mkuu bora umeanzisha huu uzi hapa.

Juzi jumamosi nikiwa natoka home na mvua hizi maji yametuama hovyo naelekea stand za huku mitaani maeneo ya Mbezi Kimara bwana mdogo mmoja yupo na gari yake Mazda model siikumbuki ila ni hizi saloons za 9.7/10.5mill mimi napita pembeni mwa barabara huku nazungumza na simu sina hili wala lile mara pwaa!

Mimaji michafu suruali yote mpaka raba nilizokuwa nimevaa zimebadilika rangi zimekuwa tope na nilivaa cadet ya khaki simple nyeusi na nyeupe,wala hakujali na sababu barabara ina mashimo alikuwa anaenda speed ndogo sana but alishindwa hata kushusha kioo kuniambia samahani nachokumbuka aligeuka kidharau akanitazama kisha huyoo akenda zake huku seat ya kushoto amekaa mwanamke wake ameweka miguu kwenye dushboard wala hawakujali.

Sehemu yenyewe ni karibu na CCM wanakolaza magari sasa jamaa waliokuwa wamekaa pale picha waliiona wakaniambia bwana huyu jamaa gari yake huwa inalalaga hapa yeye kapanga kwenye nyumba ile palee!nikajisemea kimoyo moyo hakika Tanzania ukiwa na gari wewe ndo tajiri yaani amepanga chumba na sebule ananimwagia mimi maji machafu hata haonyeshi ubinaadam?any way niliacha likapita ila siyo vizuri tusidharauliane sana tunapohisi tuna mafanikio fulani wakati mwengine unaemdharau anaweza kuwa amekuacha mbali sana wanojua wakakucheka.
 
Piga Kaz tafuta pesa tu kila mtu Ni tajiri kwa nafas yake na jamii inayomzunguka nyiny Ni Aina ya watu wanaokaaa vijiweni kujadiri maisha ya watu kuliko kujadili maisha yako halisi unayoish wew
 
pole sana kwa masahibu hayo ndg yangu. sisi watembelea kwa miguu huwa tunadharauliwa sana na wenye magari.
 
Piga Kaz tafuta pesa tu kila mtu Ni tajiri kwa nafas yake na jamii inayomzunguka nyiny Ni Aina ya watu wanaokaaa vijiweni kujadiri maisha ya watu kuliko kujadili maisha yako halisi unayoish wew
asante sana. [emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Soon Twitter inakua kama Instagram na facebook. Zamani twitter ilikua inachukuliwa kama platform ya elites kujadili mambo ya kitaifa na mambo magumu, leo kule twitter ni umalaya, ukahaba, ushoga, ujinga. Watu wanajadili mambo ya hovyo.

Nadhani platform pekee iliyobaki ya kuchangia mambo ya maana ni JF kwa sababu imetutengea majukwaa, kila mtu anachangia jukwa ambalo akili yake inaweza kujadili.
 
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…