Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sizungumzii wale ambao bado wanaendelea kuishi huko.
nazungumzia wale ambao walishawahi kuishi huko ila sasa wamerudi bongo mazima wakipambana na ugumu wa maisha ya huku. ile mentality ya maisha ya kimarekani huwa haiwatoki haraka.
Hapo kwa wanasheria.. you nailed it 😄😄Wahudumu wa ndege
Wanasheria ndani ya slim navy blue suit
wale wanaoandika post zao kwa maandishi makubwa wakidhani kwa kufanya hivyo ndio ujumbe wao utafika kwa haraka.UKISOMA HII TOPIC NA MICHANGO YAKE NDIO UTAJUA AKILI ZA WATANZANI WENGI.
UTAONA JINSI WATU WALIVYO BUSY KUCHUNGUZA MAISHA YA WATU NA KUANZA KUWA-JUDGE.
WATANZANIA WENGI WAMEJAA WIVU, MAJUNGU NA UCHUNGUU MWINGI NDANI YA MIOYO YAO.
MFANO, MTU AKINUNUA VITZ AU IST WEWE ANAKUKERA NINI?
Tunakwama wapi kama taifa? Niliamini tukiwa na watu wanaofanya tafiti itasaidia sana watoa maamuzi kupanga na kutekeleza mipango sahihi yenye tija.
Hii kazi yote iliyofanyika hapa sio ndogo!!!
Ila sipo kwenye kundi hata moja hapo juu, kwa mbaaali nilisoma mchepuo wa sayansi ila ndio ikawa elimu yangu ya juu kabisa sekondari.
Ukishakuwa masikini utaanza kumhukumu kila.mtu na 'lifestyle' yake.
Just mind your own business and work harder to get rid of poverty in your family.
ulichukua mchepuko wa sayansi au sanaa?. maana waliopata B au A kwenye somo la hisabati katika mitahani yao ya mwisho ya sekondari huwa wanahisi wapo vizuri sana kimaisha. [emoji23][emoji23][emoji23]Walau wewe elimu yako ya sekondari.
Mi niliyeishia fom tuu nisemeje sasa?
Nilifeli mtihani wa fom tuu na ndo ikawa mara yangu y mwisho kukanyaga ardhi ya shule!
*MCHEPUKO = MCHEPUO (wa masomo ya sayansi).- Wanaojua kuzungumza Kiingereza hata kama wanazungumza Kiingereza "broken". Wote ni mashahidi, hawa hata hapa JF wapo. Siku zote hujihisi wao ni bora na maisha wameyapatia.
- Wanaomiliki matoleo mbalimbali ya simu za iPhone. Siongezi neno kuhusu kundi hili.
- Waliochukua mchepuko wa masomo ya sayansi walipokuwa sekondari na baadaye wakaenda vyuo vikuu kusomea kozi mbalimbali za uhandisi. Hawa hata ukiwakuta mtaani bila ajira, by default wanajihisi tayari wameyapatia maisha.
- Wenye followers kuanzia elfu 20, 30, 40 au zaidi kwenye mtandao wa Instagram. Hili ni kundi ambalo linajihisi limeyapatia sana maisha kwa kuwa na followers wengi. Wanafollow mastaa tu. kma wewe sio star usitegemee kama atakufollow back.
- Wahitimu vijana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Siongezi neno kuhusu kundi hili.
- Vijana wa kitanzania ambao kwa wakati fulani waliwahi kuishi Marekani au Uingereza halafu kwa sasa wamerudi bongo kupambana na msoto wa maisha.
- Wanaomiliki gari jamii ya Vitz, IST na Altezza. Jeuri na mikwara yao barabarani inatupa picha halisi.
- Wanajeshi vijana miezi yao kwanza kwenye ajira jeshini halafu uwakute uraiani wamevaa zile gwanda zao.
Ongezea wengine unaowajua.
Karibuni.
MKUU,
Hebu tutajie ID yako ya awali kwanza mkuu,Magu na mdogo wake makonda
Sielewi kwa nini watu wanajali hivyo maisha ya wengine...
Nafuatilia kwa ukaribu kuona tunaangukia kundi gani hapa kwenye huu "utafiti" mkuu.
Lakini mwenzangu wewe unatisha, umelamba Urais wa kudumu. Au ulishang'atuka?
Hii nchi ina vipaji kumbe, hii kazi imefanyika hapa sio ya kitoto bingwa.
Haina hajaHebu tutajie ID yako ya awali kwanza mkuu,
Maana'ke hii umefungua leo hii.
ulichukua mchepuko wa sayansi au sanaa?. maana waliopata B au A kwenye somo la hisabati katika mitahani yao ya mwisho ya sekondari huwa wanahisi wapo vizuri sana kimaisha. [emoji23][emoji23][emoji23]
ni mchepuo, kuna mtu kanisahihisha.Na hii elimu yangu ya fom tu sijaelewa....ni mchepuko au mchepuo?
Vyovyote vile, mi nakumbuka nilisomaga masomo ya Jografia, Hesabu, Sayansi Kimu, Siasa, Kiswahili, Kizungu, na Michezo.
Somo la Michezo ndo nilikuwa nalipenda zaidi kuliko yote.