Makundi ya vijana wa Kitanzania ambao hujihisi wameyapatia maisha

Makundi ya vijana wa Kitanzania ambao hujihisi wameyapatia maisha

Unaizungumzia JF ipi mkuu?

JF hii ambayo topic ya kula mademu kimasihara inapata page 50 kwa siku mbili tu?

Unazingumzia JF ipi ambayo hakuna mashoga na makahaba

Jf ipi ambayo ni tofauti na fb,instagram na twitter?

Sikiliza mzee labda tofauti huku hatutupii picha zetu

Ila ujinga wa social media ni ule ule
Kwani JF umekatazwa kujitupia selfie yako? Tupia picha tu mzeya
 
Soo Twitter inakua kama Instagram na facebook. Zamani twitter ilikua inachukuliwa kama platform ya elites kujadili mambo ya kitaifa na mambo magumu, leo kule twitter ni umalaya, ukahaba, ushoga, ujinga. Watu wanajadili mambo ya hovyo.

Nadhani platform pekee iliyobaki ya kuchangia mambo ya maana ni JF kwa sababu imetutengea majukwaa, kila mtu anachangia jukwa ambalo akili yake inaweza kujadili.
sure
 
Vijana wanaofanya kazi benki wanajionaga sana maisha yamo mkononi tayari!

Hawa wapanda mlima wanajifanyaga wako serius sana na maisha, yan wao ndy wanajua maisha ni nini..akipita mtaani haongei na mtu, ni yeye na kula karanga, kuvaa mabuti na kuhadithia ananvyopambana...nimeona wengi
 
Amesema huku kuna majukwaa tofauti kwahiyo unachagua mwenyewe jukwaa linalokufaa

Hebu nenda jukwaa la siasa halafu fuatilia uchangiaji ndo ujue pakoje

Watu wanaropoka na kutukanana hovyo hovyo tu kifupi jf haina tofauti na social medai zote.
 
Sio madreva wetu tu. Hata sisi tuliopata nafasi ya kuendeshwa kwenye hayo magari huwa tunajisikia sana. Binafsi huwa naona Bara Bara yote ni kwa ajili yangu tu
 
.................Mkuu bora umeanzisha huu uzi hapa.

Juzi jumamosi nikiwa natoka home na mvua hizi maji yametuama hovyo naelekea stand za huku mitaani maeneo ya Mbezi Kimara bwana mdogo mmoja yupo na gari yake Mazda model siikumbuki ila ni hizi saloons za 9.7/10.5mill mimi napita pembeni mwa barabara huku nazungumza na simu sina hili wala lile mara pwaa!

Mimaji michafu suruali yote mpaka raba nilizokuwa nimevaa zimebadilika rangi zimekuwa tope na nilivaa cadet ya khaki simple nyeusi na nyeupe,wala hakujali na sababu barabara ina mashimo alikuwa anaenda speed ndogo sana but alishindwa hata kushusha kioo kuniambia samahani nachokumbuka aligeuka kidharau akanitazama kisha huyoo akenda zake huku seat ya kushoto amekaa mwanamke wake ameweka miguu kwenye dushboard wala hawakujali.

Sehemu yenyewe ni karibu na CCM wanakolaza magari sasa jamaa waliokuwa wamekaa pale picha waliiona wakaniambia bwana huyu jamaa gari yake huwa inalalaga hapa yeye kapanga kwenye nyumba ile palee!nikajisemea kimoyo moyo hakika Tanzania ukiwa na gari wewe ndo tajiri yaani amepanga chumba na sebule ananimwagia mimi maji machafu hata haonyeshi ubinaadam?any way niliacha likapita ila siyo vizuri tusidharauliane sana tunapohisi tuna mafanikio fulani wakati mwengine unaemdharau anaweza kuwa amekuacha mbali sana wanojua wakakucheka.
Aisee, mtafute huyo demu wake aliyeweka miguu juu umpige miti mkuu.
😁
 
Vijana wanaofanya benki wanaona wamewin life...fani ambayo haina majivuno ni udaktari tu kidogo na wahandisi
 
Haka kauzi kamekaa kimajungu majungu hivi, kimipasho mipasho mixer na kiwivu wivu, anyway, vipi wanafunzi wa chuo hasa UDSM.
 
Hakuna vijana wanaojiona wametoboa maisha kama hawa wa am global alliance
Madem hawa wanaofany besidei za kumwagiana maji
 
Back
Top Bottom