Makundi ya vijana wa Kitanzania ambao hujihisi wameyapatia maisha

sizungumzii wale ambao bado wanaendelea kuishi huko.

nazungumzia wale ambao walishawahi kuishi huko ila sasa wamerudi bongo mazima wakipambana na ugumu wa maisha ya huku. ile mentality ya maisha ya kimarekani huwa haiwatoki haraka.

Kwanza wewe kutokujua au kuthamini kwamba alishawahi kuwa US anakuona kama mhujumu uchumi anaetakiwa kunyongwa bila kupewa nafasi ya kuomba msamaha wa kutubu kwa DPP.
 
Wavaa kaunda suti na superblack kichwani vinajiona wazalendo kuliko watz wengine.
hahahaha....vijana wa dizaini hiyo wamejaa sana uvccm. huwa wanajifanya wanauchungu sana na chama kuliko waasisi.
 
wale wanaoandika post zao kwa maandishi makubwa wakidhani kwa kufanya hivyo ndio ujumbe wao utafika kwa haraka.

NB: niliyoyaandika kwenye mada yangu kwa lugha ya kimakonde inaitwa "social experience".

kila nchi ina aina ya social experience zake na sio dhambi kujadili. so take it easy bro.
 
Walau wewe elimu yako ya sekondari.

Mi niliyeishia fom tuu nisemeje sasa?

Nilifeli mtihani wa fom tuu na ndo ikawa mara yangu y mwisho kukanyaga ardhi ya shule!
 
Walau wewe elimu yako ya sekondari.

Mi niliyeishia fom tuu nisemeje sasa?

Nilifeli mtihani wa fom tuu na ndo ikawa mara yangu y mwisho kukanyaga ardhi ya shule!
ulichukua mchepuko wa sayansi au sanaa?. maana waliopata B au A kwenye somo la hisabati katika mitahani yao ya mwisho ya sekondari huwa wanahisi wapo vizuri sana kimaisha. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
*MCHEPUKO = MCHEPUO (wa masomo ya sayansi).
 
Kuna wale wanaoweka whatsapp status za hela,unakuta kashikilia minoti kibao anajikuta ameyapatia maisha. Sasa mimi niko hivi,najifanya mchimba chumvi afu siku nikiamua kujionesha rangi zangu watatafuta pa kujificha[emoji41]
 
Nafuatilia kwa ukaribu kuona tunaangukia kundi gani hapa kwenye huu "utafiti" mkuu.

Lakini mwenzangu wewe unatisha, umelamba Urais wa kudumu. Au ulishang'atuka?

Hii nchi ina vipaji kumbe, hii kazi imefanyika hapa sio ya kitoto bingwa.

Hahaaa urais wangu ni wa kudumu kaka.

Labda hapo baadaye maadui wa mafanikio wanipindue.
 
ulichukua mchepuko wa sayansi au sanaa?. maana waliopata B au A kwenye somo la hisabati katika mitahani yao ya mwisho ya sekondari huwa wanahisi wapo vizuri sana kimaisha. [emoji23][emoji23][emoji23]

Na hii elimu yangu ya fom tu sijaelewa....ni mchepuko au mchepuo?

Vyovyote vile, mi nakumbuka nilisomaga masomo ya Jografia, Hesabu, Sayansi Kimu, Siasa, Kiswahili, Kizungu, na Michezo.

Somo la Michezo ndo nilikuwa nalipenda zaidi kuliko yote.
 
ni mchepuo, kuna mtu kanisahihisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…