Makundi ya vijana wa Kitanzania ambao hujihisi wameyapatia maisha

Makundi ya vijana wa Kitanzania ambao hujihisi wameyapatia maisha

Kuna jamaa ameiandika huko Twitter.

HAKUNA WATU WANAJIONAGA WAMEYAPATIA MAISHA KAMA WALE JAMAA WANAOSIMAMIA MITIHANI YA UTUMISHI/AJIRA PORTAL.
 
- Wanaojua kuzungumza Kiingereza hata kama wanazungumza Kiingereza "broken". Wote ni mashahidi, hawa hata hapa JF wapo. Siku zote hujihisi wao ni bora na maisha wameyapatia.

- Wanaomiliki gari jamii ya Vitz, IST na Altezza. Jeuri na mikwara yao barabarani inatupa picha halisi.

- Wanajeshi vijana miezi yao kwanza kwenye ajira Jeshini halafu uwakute Uraiani wamevaa zile sare zao zenye mabaka mabaka.

Ongezea wengine unaowajua.

Karibuni.
Waliochaguliwa kwenda chuo kikuu

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
 
Wale wenye rasta waliooa vibibi vya kizungu 60yrs plus. Unawakuta wanatembea jioni wanaongozana huku wanasindikizwa na mbwa wao. Wapo sana mbezi beach, masaki na Arusha. Yaani wanajiona wameyapatia maisha balaa
 
Macustomer care, receptionist na mahr asee Hawa wanazingua sana
Nlienda Kwny interview Moja yule HR alikazia Kwny swal ambalo ni gumu sana mpk mahr wenzie wakawa wanamuangalia jinsi anavyolirudia swal nkataman kumwambia Mbn kama unataka sifa kaka

-wale maservice man/girl wa jkt asee wale maboya wanajiona kama Navy Seal vile jinsi wanavyonyanyasa kurutiz utaskia "kuruta hatujapiga kozi pamoja ntakuharibu" yaan wajiona kama Mabeyo vile
 
Wanaishi dar, wanajiona wamepatia sana maisha na wako juu zaidi kulko wamikoani!

Madem wenye tako,Wafanyakazi bank hasa CRDB,.
Wanaoishi dar yan naamin wanahisi ndio Ulaya

Makundi mengineyo;
1. Watu wanaoishi Dar/ wale ambao wamewahi kufika Dar, wanawaona walio mikoani ni maboya,
2. Watu wa Kilimanjaro, wanajiona ndio wajanja na wameelimika kuzidi waTanzania waliobakia
3. Wadada wenye matako makubwa, wanajiona wao wana undugu na Mungu
5. Wamiliki wa nyumba zenye geti, wanatuona wengine tunaishi vichakani
Wanaoish dar co tu binadamu hata kuku asa jogoo lilitangulia kukaa dar siku akija jogoo wa shamba hapati tunda labda ampige kwnza jogoo la dar au avizie kimtetea kinachojipitisha karib yake Lakin wee akionwa na jogoo la dar yaan hata kama hajapiz kimoko anatolewa baru inshot dar kama kuna kalaana fulan hv ndo maana unaweza shangaa jua kali lakn dalila tu bonge la mvua linanyesha...
 
[emoji1787][emoji1787]
 
Wadada wale wa "kituo kinachofuata ni manzese argentina" nao wanajiskia tu kwnn siku hz hawatangaz😁
 
- Wanaojua kuzungumza Kiingereza hata kama wanazungumza Kiingereza "broken". Wote ni mashahidi, hawa hata hapa JF wapo. Siku zote hujihisi wao ni bora na maisha wameyapatia.

- Wanaomiliki matoleo mbalimbali ya simu za iPhone. Siongezi neno kuhusu kundi hili.

- Waliochukua mkondo wa masomo ya sayansi walipokuwa sekondari na baadaye wakaenda vyuo vikuu kusomea kozi mbalimbali za uhandisi. Hawa hata ukiwakuta mtaani bila ajira, by default wanajihisi tayari wameyapatia maisha.

- Wenye followers kuanzia 20K, 30K, 40K au zaidi kwenye mtandao ya kijamii. Hili ni kundi ambalo linajihisi limeyapatia sana maisha kwa kuwa na followers wengi. Wanafollow mastaa tu. kama wewe sio star usitegemee ukurasa wako kupata followback au like kutoka kwenye kundi hili.

- Wahitimu vijana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Siongezi neno kuhusu kundi hili.

- Vijana wa Kitanzania ambao kwa wakati fulani waliwahi kuishi Marekani au Uingereza halafu kwa sasa wamerudi Bongo kupambana na msoto wa maisha.

- Wanaomiliki gari jamii ya Vitz, IST na Altezza. Jeuri na mikwara yao barabarani inatupa picha halisi.

- Wanajeshi vijana miezi yao kwanza kwenye ajira Jeshini halafu uwakute Uraiani wamevaa zile sare zao zenye mabaka mabaka.

Ongezea wengine unaowajua.

Karibuni.
Hivi ina nawezekanaje uishi usa au UK uko halafu unarudi bongo? Aise utakuwa umelogwa aise..
 
1. Wanaotumwa kuclamp matairi ya magari kwa 'wrong parking'. Heri kupambana na ibilisi gizani kuliko hawa jamaa.

2. Watoto wa miaka 5+ walionunuliwa na kuvaa nguo mpya za siku kuu.

3. Watoto wa kiume shuleni wanaobalehe walioanza kuota vindevu kabla ya wenzao darasani. Kila saa wakiongea wanazikuna kuna na kuhakikisha wenzao wanawaona wanavyovikunakuna. Wanawaona wenzao kama bado wananyonya kwa mama zao.

4. Watoto wa kiume darasani walionza kupata sauti nzito. Kila swali anainua mkono ajibu ili darasa lisikie bezi lake.
 
Back
Top Bottom