Malaika anayetajwa katika Ufunuo wa Yohana 9:11, ni nani haswa? Je kupatwa kwa jua Aprili 2024 kunahusiana na malaika huyu?

Malaika anayetajwa katika Ufunuo wa Yohana 9:11, ni nani haswa? Je kupatwa kwa jua Aprili 2024 kunahusiana na malaika huyu?

Wana JF, umofia kwenu.

Sisi ambao tumeishi kwenye kupokea imani katika umoja na utofauti wa itikadi zetu, tunaelewa uwepo wa viumbe wa kipekee ambao waliumbwa kwa upepo na moto. Baadhi ya viumbe hao waliasi na kutuletea sintifahamu kubwa kwenye mahusiano yetu na aliyetuumba (kwa imani tunavyoamini sisi).



View attachment 2948716
Majina ya Malaika wanaotajwa mara nyingi kwenye kitabu cha Biblia ni Mikaeli, Gabriel na Lusifa ambaye baadaye aligeuka kuwa shetani. Lakini kwenye kitabu cha Ufunuo wa Yohana ametajwa malaika mwingine ambaye anaonekana na jukumu tofauti la kuogofya zaidi. Wahubiri wengi wamekuwa wakihubiri safari ya Mbinguni na funuo mbalimbali zinazotarajiwa kutokea kabla ya siku kubwa ya Big Bang itakayoumaliza ulimwengu huu na kuanza maisha mapya nje ya realm hii tunayoishi.
View attachment 2948713
Ufunuo 9:11 Juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.

Malaika huyu ana special segment kwenye moja ya battalion ya lusifa kama inavyoelezwa kwenye Ufunuo 9: 2 - 10. Ukichunguza maandiko unaweza kupata nukta kadhaa za kuunganisha ili kupata usahihi ama ukaribiano wa matukio yaliyotabiriwa. Hivi sasa mamlaka za kimataifa za Hali ya Hewa wametoa tahadhari uwezekano wa kupatwa kwa jua mnamo tarehe 4 April 2024 ambapo jua litatiwa giza kwa muda mrefu zaidi kulingana na historia ya kupatwa kwa jua.
View attachment 2948715

Nini kitatokea kwenye tukio hilo na uwezekano wa historia ya dunia kubadilika baada ya jua kupatwa unaweza kuthibitisha kuwa Abadon atakuwa ameshapanda baada ya shimo la kuzimu kufunguliwa? Pia kumekuwa na matukio yakiripotiwa ya kuonekana kwa nzige waharibifu mahala mahala, ambapo miaka ya hivi karibuni kumeripotiwa nzige kuzingira eneo la Hijja la Maka hususan ule msikiti mkubwa. Jambo hili limewaibua watu wengi kujaribu kuongelea uwezekano wa dalili zilizotajwa kwenye kitabu cha Ufunuo; ambapo ukichimba taarifa za nzige hao hawahusiani hata kidogo na Nzige wanaotajwa kwenye Ufunuo 9: 3, 7-9.
View attachment 2948718


Lengo la uzi huu ni kutafuta elimu zaidi kuhusu malaika hususan huyu aliyetajwa kwenye kitabu hiko. Kwa kuwa analo jina la Kiyunani, inaleta picha kwamba Apolioni anaweza kuwepo kwenye majina ya miungu inayotajwa kwenye taarifa za kale za Wayunani (Wagiriki). Wenye kufahamu haya mambo watushirikishe elimu zaidi kwenye hili jambo.

Karibuni tuelimishane
DR Mambo Jambo zitto junior Eli Cohen Mathanzua Rabbon pitieni hapa.

Hao nzige wa kuzimu wana Sifa za kipekee na ni kwa ajili ya kuwaadhibu wanadamu wasio na mihuri ya Mungu watakapokuwepo wakati huo (hao sio nzige wa kawaida, hao ni watesaji tu).......

nzige tulionao Sasa wanaosumbua ni wale wa jangwani (Desert Locust) hawa wameongezeka sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa sidhani kama wana uhusiano wa moja kwa moja.

Ila huenda mabadiliko ya hali ya hewa yakawa dalili za kuelekea kwenye ule mwisho ila bado sio mwisho wenyewe.
 
Kwenye maandiko wanasema malaika wa tano akipiga baragumu, atapewa funguo kufungua shimo la kuzimu...... Huyu malaika Abadoni atachomoza na hao nzige hatari... Kuna uhusiano wowote na wale malaika wanne hatari waliofungwa chini ya mto?

Abadon au Apolioni (Apollyon), ni shetani ama jemedari kwenye jeshi lake?
Wale wanne wa mto fiati ni masensri tu, yani wajuba, wachenetaji watauwa watu karibu 2 ya dunia, huyo apoloni ni nzige lord, Pia kuna malaika waasi waalio na nguvu kuliko shetani mmoja wapo ni huyo mwamba
 
Ndio, katika muktadha wa Ufunuo 9:11, malaika huyu anayejulikana kama Abadoni au Apolioni anaunganishwa na tukio la malaika wa tano akitoa tarumbeta na kupewa funguo za shimo la kuzimu. Kisha, nzige hatari wanaoongozwa na huyu malaika huachiwa kutoka kwenye shimo hilo. Kuhusu uhusiano na malaika wanne waliofungwa chini ya mto, kuna mjadala kuhusu hilo katika tafsiri mbalimbali za maandiko.

Katika tafsiri za kidini, kuna tofauti za maoni kuhusu utambulisho na asili ya malaika huyu. Baadhi wanafikiria kuwa Abadoni au Apolioni ni jemedari katika jeshi la Shetani, wakati wengine wanaweza kuona malaika huyu kama uhusiano wa nguvu za uovu au mfano wa kishetani. Hata hivyo, maandiko hayatoi maelezo ya kutosha kuhusu utambulisho halisi wa malaika huyu, hivyo suala hilo bado linabaki kama mada ya tafsiri na majadiliano katika muktadha wa imani na teolojia.
Katika sura za mwanzoni za kitabu cha Ufunuo wa Yohana kuna barua aliandika kwa makanisa huku akitaja malaika... wapo waalimu wa Biblia kama Kakobe wanatafsiri kwenye mafundisho yao kuwa hao malaika wanaotajwa ni viongozi waangalizi wa hayo makanisa....

Hapa kwenye Ufunuo 9:11 huyu Apolioni au Abadon anatajwa kama mfalme kiongozi wa hao nzige waliobeba features za kutisha zenye madhara kwa binadamu. Je inawezekana tafsiri ya fallen angel isiwe sahihi kwake kwa sababu ya nafasi yake kama mfalme au kiongozi wa hao nzige? Kama ilivyo jamii ya wadudu lazima iwe na mfalme au malkia
 
Kimsingi mimi ukishatumia scriptures kama mtetezi wa hoja yako siwezi elewana na wewe sababu hizo sasa ni imani sawa kabisa na hisia/mapenzi binafs.
Mkuu
Unaweza kujadili kila neno kwa muktadha wa maono yako. Ukijibagua kuwa Quran, Biblia na vitabu vilivyohifadhi maandiko ya imani hizo haileti mantiki.

Ni scriptures pekee ambamo kumehifadhi taarifa lukuki zinazojenga udadisi na facts kadhaa muhimu
 
Unapodadisi nguvu za kuzimu isiwe kama kitisho kwa wanadamu kwa maana sisi wanadamu mlinzi wetu ni YESU KRISTO jamii wa SIMBA WA YUDA JEMEDARI WA VITA. huyo pekee ndio tungewekeza nguvu kubwa kumsoma, kumuelewa na kumfuata maana alipo yeye hao apoliyon hawaingii.
 
Mkuu
Unaweza kujadili kila neno kwa muktadha wa maono yako. Ukijibagua kuwa Quran, Biblia na vitabu vilivyohifadhi maandiko ya imani hizo haileti mantiki.

Ni scriptures pekee ambamo kumehifadhi taarifa lukuki zinazojenga udadisi na facts kadhaa muhimu
Ahya sawa Mkuu.
 
Huyo ni mfalme wa nzige ambao ni battalion ya kuzimu.
Inawezekana makamanda wa jeshi la shetani wana vyeo vya ufalme
Hakuna kitu kama hiyo, mfalme ndani ya mfalme, HAPANA.

Waulize waganga, wenye level za juu watakwambia.
 
DR Mambo Jambo zitto junior Eli Cohen Mathanzua Rabbon pitieni hapa.

Hao nzige wa kuzimu wana Sifa za kipekee na ni kwa ajili ya kuwaadhibu wanadamu wasio na mihuri ya Mungu watakapokuwepo wakati huo (hao sio nzige wa kawaida, hao ni watesaji tu).......

nzige tulionao Sasa wanaosumbua ni wale wa jangwani (Desert Locust) hawa wameongezeka sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa sidhani kama wana uhusiano wa moja kwa moja.

Ila huenda mabadiliko ya hali ya hewa yakawa dalili za kuelekea kwenye ule mwisho ila bado sio mwisho wenyewe.
Hayo yatatokea baada ya UNYAKUO, ni pale 666 itakapoanza Rasmi,

Mabadiliko tunayopitia sasa ni nusu shari,

Watakaoachwa wasinyakuliwe, waliomkataa Yesu wataucheza muziki huo.

Kuzimu na Majeshi yote yatapanda duniani kushughulikia na wanadamu Walio hai.
 
Back
Top Bottom