Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 32,639
- 42,908
DR Mambo Jambo zitto junior Eli Cohen Mathanzua Rabbon pitieni hapa.Wana JF, umofia kwenu.
Sisi ambao tumeishi kwenye kupokea imani katika umoja na utofauti wa itikadi zetu, tunaelewa uwepo wa viumbe wa kipekee ambao waliumbwa kwa upepo na moto. Baadhi ya viumbe hao waliasi na kutuletea sintifahamu kubwa kwenye mahusiano yetu na aliyetuumba (kwa imani tunavyoamini sisi).
View attachment 2948716
Majina ya Malaika wanaotajwa mara nyingi kwenye kitabu cha Biblia ni Mikaeli, Gabriel na Lusifa ambaye baadaye aligeuka kuwa shetani. Lakini kwenye kitabu cha Ufunuo wa Yohana ametajwa malaika mwingine ambaye anaonekana na jukumu tofauti la kuogofya zaidi. Wahubiri wengi wamekuwa wakihubiri safari ya Mbinguni na funuo mbalimbali zinazotarajiwa kutokea kabla ya siku kubwa ya Big Bang itakayoumaliza ulimwengu huu na kuanza maisha mapya nje ya realm hii tunayoishi.
View attachment 2948713
Ufunuo 9:11 Juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.
Malaika huyu ana special segment kwenye moja ya battalion ya lusifa kama inavyoelezwa kwenye Ufunuo 9: 2 - 10. Ukichunguza maandiko unaweza kupata nukta kadhaa za kuunganisha ili kupata usahihi ama ukaribiano wa matukio yaliyotabiriwa. Hivi sasa mamlaka za kimataifa za Hali ya Hewa wametoa tahadhari uwezekano wa kupatwa kwa jua mnamo tarehe 4 April 2024 ambapo jua litatiwa giza kwa muda mrefu zaidi kulingana na historia ya kupatwa kwa jua.
View attachment 2948715
Nini kitatokea kwenye tukio hilo na uwezekano wa historia ya dunia kubadilika baada ya jua kupatwa unaweza kuthibitisha kuwa Abadon atakuwa ameshapanda baada ya shimo la kuzimu kufunguliwa? Pia kumekuwa na matukio yakiripotiwa ya kuonekana kwa nzige waharibifu mahala mahala, ambapo miaka ya hivi karibuni kumeripotiwa nzige kuzingira eneo la Hijja la Maka hususan ule msikiti mkubwa. Jambo hili limewaibua watu wengi kujaribu kuongelea uwezekano wa dalili zilizotajwa kwenye kitabu cha Ufunuo; ambapo ukichimba taarifa za nzige hao hawahusiani hata kidogo na Nzige wanaotajwa kwenye Ufunuo 9: 3, 7-9.
View attachment 2948718
Lengo la uzi huu ni kutafuta elimu zaidi kuhusu malaika hususan huyu aliyetajwa kwenye kitabu hiko. Kwa kuwa analo jina la Kiyunani, inaleta picha kwamba Apolioni anaweza kuwepo kwenye majina ya miungu inayotajwa kwenye taarifa za kale za Wayunani (Wagiriki). Wenye kufahamu haya mambo watushirikishe elimu zaidi kwenye hili jambo.
Karibuni tuelimishane
Hao nzige wa kuzimu wana Sifa za kipekee na ni kwa ajili ya kuwaadhibu wanadamu wasio na mihuri ya Mungu watakapokuwepo wakati huo (hao sio nzige wa kawaida, hao ni watesaji tu).......
nzige tulionao Sasa wanaosumbua ni wale wa jangwani (Desert Locust) hawa wameongezeka sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa sidhani kama wana uhusiano wa moja kwa moja.
Ila huenda mabadiliko ya hali ya hewa yakawa dalili za kuelekea kwenye ule mwisho ila bado sio mwisho wenyewe.