Malaika anayetajwa katika Ufunuo wa Yohana 9:11, ni nani haswa? Je kupatwa kwa jua Aprili 2024 kunahusiana na malaika huyu?

DR Mambo Jambo zitto junior Eli Cohen Mathanzua Rabbon pitieni hapa.

Hao nzige wa kuzimu wana Sifa za kipekee na ni kwa ajili ya kuwaadhibu wanadamu wasio na mihuri ya Mungu watakapokuwepo wakati huo (hao sio nzige wa kawaida, hao ni watesaji tu).......

nzige tulionao Sasa wanaosumbua ni wale wa jangwani (Desert Locust) hawa wameongezeka sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa sidhani kama wana uhusiano wa moja kwa moja.

Ila huenda mabadiliko ya hali ya hewa yakawa dalili za kuelekea kwenye ule mwisho ila bado sio mwisho wenyewe.
 
Wale wanne wa mto fiati ni masensri tu, yani wajuba, wachenetaji watauwa watu karibu 2 ya dunia, huyo apoloni ni nzige lord, Pia kuna malaika waasi waalio na nguvu kuliko shetani mmoja wapo ni huyo mwamba
 
Katika sura za mwanzoni za kitabu cha Ufunuo wa Yohana kuna barua aliandika kwa makanisa huku akitaja malaika... wapo waalimu wa Biblia kama Kakobe wanatafsiri kwenye mafundisho yao kuwa hao malaika wanaotajwa ni viongozi waangalizi wa hayo makanisa....

Hapa kwenye Ufunuo 9:11 huyu Apolioni au Abadon anatajwa kama mfalme kiongozi wa hao nzige waliobeba features za kutisha zenye madhara kwa binadamu. Je inawezekana tafsiri ya fallen angel isiwe sahihi kwake kwa sababu ya nafasi yake kama mfalme au kiongozi wa hao nzige? Kama ilivyo jamii ya wadudu lazima iwe na mfalme au malkia
 
Kimsingi mimi ukishatumia scriptures kama mtetezi wa hoja yako siwezi elewana na wewe sababu hizo sasa ni imani sawa kabisa na hisia/mapenzi binafs.
Mkuu
Unaweza kujadili kila neno kwa muktadha wa maono yako. Ukijibagua kuwa Quran, Biblia na vitabu vilivyohifadhi maandiko ya imani hizo haileti mantiki.

Ni scriptures pekee ambamo kumehifadhi taarifa lukuki zinazojenga udadisi na facts kadhaa muhimu
 
Unapodadisi nguvu za kuzimu isiwe kama kitisho kwa wanadamu kwa maana sisi wanadamu mlinzi wetu ni YESU KRISTO jamii wa SIMBA WA YUDA JEMEDARI WA VITA. huyo pekee ndio tungewekeza nguvu kubwa kumsoma, kumuelewa na kumfuata maana alipo yeye hao apoliyon hawaingii.
 
Ahya sawa Mkuu.
 
Huyo ni mfalme wa nzige ambao ni battalion ya kuzimu.
Inawezekana makamanda wa jeshi la shetani wana vyeo vya ufalme
Hakuna kitu kama hiyo, mfalme ndani ya mfalme, HAPANA.

Waulize waganga, wenye level za juu watakwambia.
 
Hayo yatatokea baada ya UNYAKUO, ni pale 666 itakapoanza Rasmi,

Mabadiliko tunayopitia sasa ni nusu shari,

Watakaoachwa wasinyakuliwe, waliomkataa Yesu wataucheza muziki huo.

Kuzimu na Majeshi yote yatapanda duniani kushughulikia na wanadamu Walio hai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…