KERO Malalamiko kuhusu malipo yasiyo na usawa kwa wataalamu wa maabara mkoani Mwanza, wakati wa mitihani ya NECTA

KERO Malalamiko kuhusu malipo yasiyo na usawa kwa wataalamu wa maabara mkoani Mwanza, wakati wa mitihani ya NECTA

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu malipo ya wataalamu wa maabara (Laboratory Technicians) wanaohusika na maandalizi ya mitihani ya vitendo kwa watahiniwa wa Kidato cha Nne na Sita wakati wa mitihani ya kuhitimu inayoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).

Changamoto kubwa ni kwamba wataalamu tunalipwa kiwango sawa cha posho bila kuzingatia idadi ya mitihani tunayoandaa na uzito wa majukumu yetu. Kwa mfano, mtaalamu anayeandaa mtihani wa 2A pekee hulipwa sawa na mwenzake anayeandaa mitihani ya 2A, 2B na 2C kwa Kidato cha Nne. Hali hiyo pia inajitokeza kwa Kidato cha Sita katika masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia, ambapo mtaalamu anayeandaa mtihani wa 3A pekee hulipwa sawa na anayeandaa mitihani ya 3A, 3B na 3C.

Hali hii inaleta malalamiko miongoni mwa wataalamu kwa sababu malipo hayazingatii tofauti ya majukumu na kiasi cha kazi wanazofanya. Inafika hatua mtaalamu anayehudumia watahiniwa 600 analipwa posho sawa na mwenzake anayehudumia watahiniwa 45, licha ya tofauti kubwa ya mzigo wa kazi.

Aidha, wataalamu wa maabara tunafanya kazi zinazohitaji umakini mkubwa na wakati mwingine tunakabiliwa na hatari zinazotokana na matumizi ya kemikali mbalimbali. Pamoja na changamoto hizo, bado tunakabiliwa na suala la malipo ambayo hayaendani na uzito na wingi wa majukumu yetu.

Kwa msingi huo, tunaiomba NECTA pamoja na mamlaka nyingine zinazohusika kupitia upya utaratibu wa malipo haya ili kuhakikisha kuwa posho zinazingatia idadi ya mitihani, wingi wa watahiniwa na uzito wa kazi inayofanyika.

NECTA, tafadhali lichukulieni suala hili kwa uzito na mtoe ufafanuzi kuhusu utaratibu unaotumika kupanga malipo haya. Ni muhimu kuhakikisha kuwa wataalamu wa maabara tunatendewa haki na kulipwa kwa kuzingatia majukumu tunayotekeleza. Usawa katika malipo ni muhimu katika kuongeza morali na kutambua mchango wao katika kufanikisha mitihani ya kitaifa.
 
Poleni sana

Mnastahili posho ya vihatarishi mnavyokutana navyo i.e. risk allowance. Wizara husika iliangalie hili
 
Inafika hatua mtaalamu anayehudumia watahiniwa 600 analipwa posho sawa na mwenzake anayehudumia watahiniwa 45, licha ya tofauti kubwa ya mzigo wa kazi.
Hapa pamenishtua sana kwa hio anaehudumia mtu mmoja tu km analipwa 1,000,000 basi na anaehudumia watu 1,000 nae analipwa 1,000,000? Waangalie namna ya kufanya ila kiuhalisia hii sio haki
 
Kwanini posho iwe moja wakati mitihani hiyo inafanywa siku tofauti?
 
Sisi ayo hayatuhusu ukiona huelewi acha kazi uje tushinde wote mtaani uku.
 
Mimi ninachojua msingi wa malipo ni idadi ya siku na cheo cha mfanyakazi ndivyo huamua malipo yawe kiasi gani. Pengine hilo ndio walilolizingatia
 
Mimi ninachojua msingi wa malipo ni idadi ya siku na cheo cha mfanyakazi ndivyo huamua malipo yawe kiasi gani. Pengine hilo ndio walilolizingatia

Huko local governemnt kuna kona kona nyingi sana nikuhakikishie tu. Hapo unakuta viongozi wa ngazi husika wanalazimisha wawalipe "flat rate" lakini kwenye dokezo la kuomba fedha wamewawekea siku nyingi na hela nyingi. Zinazobaki wanazibonda.​
 
Back
Top Bottom