Malalamiko kuhusu pesa za kujikimu kwa waajiriwa wapya Halmashauri ya wilaya ileje

Malalamiko kuhusu pesa za kujikimu kwa waajiriwa wapya Halmashauri ya wilaya ileje

The atlantic

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2023
Posts
390
Reaction score
670
Habari za leo wakuu,

Moja kwa moja kwenye mada, pesa za kujikimu kwa waajiriwa wapya zimefika wilayani ileje yapata wiki mbili Sasa, hili lilithibitishwa na katibu ofisini ya DMO kupitia kundi lao la WhatsApp (idara afya).

Lakini hadi leo pesa hizo hazijalipwa kwa wahusika na kila wakihoji wanaambiwa 'soon watalipwa'.

Za chini chini ni kwamba fungu hilo limedokolewa kwa ajili ya kuukarimu mwenge unaotarajiwa kuja wilayani humo wiki ijayo.

Kwako mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Ileje, kama unavyojua jiografia ya wilaya yako ilivyokaa ni mbaya, uchumi wa wilaya yako uko chini. Huduma hazipatikani kwa wanakoishi vijijini, wenyeji wanaogopwa kutokana na sifa zao, wasaidie hawa watumishi wapate hela zao.
 
Vijana msidanganywe sijui pesa zipo hamtaki kulipwa kitu kilichochelewesha msilipwe ni mifumo ya malipo serikalini kutoanza kufanya kazi baada ya mwaka wa fedha 2022 to 2023 kuisha

Kwaiyo mwezi huu haki yenu mtapatiwa kwani mifumo ishafunguka acheni sikia porojo za sijui group la WhatsApp nk

Nililipoti kutoka hapa HAZINA YA JF miye ni George maratu wa...........
 
Mkuu mwezi ndo unaishilizia ivooo
 
Alafu mbona nasikia mifumo inafungwa Tena tare 30 mwezi huu Ni kweli au
 
Mara nyingi pesa za kujikimu bila kutumia nguvu za ziada huishia mifukoni mwa wakubwa. Hapa cha msingi, orodhesheni halmashauri zote ambazo hazijafanya malipo ili hatua zingine ziweze kuchukuliwa vinginevyo mtadhulumika
 
Mkuu mwezi ndo unaishilizia ivooo
Pale unapona haki yako upewi usibembeleze chukua kwa nguvu sasa kama mnategemea mkuu wa wilaya, sijui mkurugenzi nk atakuja wasemea endeleeni hapo nikutaka haki yenu kwa nguvu wenzenu walishawafungia wakurugenzi ofisini wakitaka haki yao so fanyeni jambo mpewe chenu

Nikupe wazo tafuta idadi ya watu mnao dai hizo pesa tafuta mawasiliano yao ukiyapata tuma meseji tarehe ...... unatakiwa kufika ofisi ya mkurugenzi kuchukua malipo yako ya kujikimu fika bila kukosa taja na mda pia mwamnie kama ana swali akupigie akikupigia tu unampanga bwana uje hiyo siku omba ruhusa kituo chako,cha kazi sema unafika hospital mala moja kisha njoo uku tudai chetu chetu

Hakikisha unaruhusa usiondoke bila ruhusa utaonekana mtoro kazini hiyo kesi tena so buni uongo wowote upate ruhusa mkifika pale ita wenzako hoja moja wote nendeni kwa afisa utumishi mwambieni shida yenu kama hana majibu ombeni muonane na mkurugenzi, mkurugenzi akikosa majibu nyokeni kwa afisa tawala akikosa majibu nendeni kwa mkuuu wa wilaya hapo mnakiamsha mnachukua na picha video mnasambaza kwenye magroup ya mitandao ya jamii

Angalizo ushauri huu unaitaji ujasiri sana kama huna ujasiri acha
 
Hela za serikali hazitolewi hovyo,zinapitia mifumo na wakuu wengi ili kuidhinishwa,endeleeni kupaza sauti mtalipwa.
 
Poleni sana, mambo ya serikali ndivyo yalivyo...
 
Back
Top Bottom