Supu ya kokoto
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 4,194
- 7,602
Serikaliiiiiii.......tunakufa huku ILEJE,Songwe.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mmeshalipwaHabari za leo wakuu,
Moja kwa moja kwenye mada, pesa za kujikimu kwa waajiriwa wapya zimefika wilayani ileje yapata wiki mbili Sasa, hili lilithibitishwa na katibu ofisini ya DMO kupitia kundi lao la WhatsApp (idara afya).
Lakini hadi leo pesa hizo hazijalipwa kwa wahusika na kila wakihoji wanaambiwa 'soon watalipwa'.
Za chini chini ni kwamba fungu hilo limedokolewa kwa ajili ya kuukarimu mwenge unaotarajiwa kuja wilayani humo wiki ijayo.
Kwako mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Ileje, kama unavyojua jiografia ya wilaya yako ilivyokaa ni mbaya, uchumi wa wilaya yako uko chini. Huduma hazipatikani kwa wanakoishi vijijini, wenyeji wanaogopwa kutokana na sifa zao, wasaidie hawa watumishi wapate hela zao.