DOKEZO Malalamiko kwa NHIF: Nashindwa kupata huduma za Afya pamoja na kulipia kifurushi cha Tsh. Milioni 1.4

DOKEZO Malalamiko kwa NHIF: Nashindwa kupata huduma za Afya pamoja na kulipia kifurushi cha Tsh. Milioni 1.4

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mimi pia nawashangaa hawa NHIF. Mtu binafsi anaweza kulipa pesa nyingi kwa mwaka kuishinda muajiriwa, lakini wanapewa huduma za ovyo. Wanawanyanyasa wachangiaji wakati hujuma inafanywa hospitalini kwa kuandika pesa nyingi wakati mgonjwa ametibiwa kwa gharama ndogo. Wafanye utafiti watagundua ukweli huo
 
Mimi siwaelewi watoa maamuzi wa shirika hili kwa hatua yao ya kubariki ubaguzi kinyume cha katiba, sheria na pengine misingi ya utatibu wanayodai kuiwekea bima.

Iweje watu wanaochangia kapu moja, wengine waruhusiwe kupata huduma hospitali yoyote, ilihali wale wenzangu na mimi wakitakiwa kuanzia hospitali ya chini na kisha upewe rufaa, ndio utapata matibabu.

Nimemshuhudia mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji BMC na kutakiwa kurudi klinik wiki mbili baadaye, huyu mgonjwa alikataliwa kupokelrwa BMC akitakiwa kuwa na rufaa kutoka hpspitali ya mkoa.
Binafsi najiuliza kwanini kuna ubaguzi baina ya wanachama? Kosa la hawa wengine ni kuchangia wenyewe badala ya mwajiri? Je kuna upigaji katika hospitali kupitia bima? Hii ndio njia ya kupunguza? Au nni namna ya kuzibeba hospitali za ummy?

Naomba kuwakumbusha yaliyotokea wakati wa mwalimu; alitaka serikali iwe na maduka yake ili yashindane na yale binafsi lakini kina kawawa na wenzake sawa na akina ummy na wenzake wakataka kuua maduka binafsi. Kilichotokea kwa maduka ya ujamaa leo ni historia.
 
Kuona vitu ambavyo vipo katika astal plane,unahitaji clairvoyant sight.
Kwa hiyo unawezausali malaika aje mbele yako. Lakinu kama huna clairvoyant vision huwezi kumuona.
Likewise,unaweza kuwaita mashetani,kama Mfalme Suleiman,lakini ili kuwaona lazima uwe na special powers of vision.
Halafu,your Father in Heaven knows what you want even before you ask Him? Well,that may be a true statement,lakini,kama unataka msaada wa Yesu lazima usali umwombe Yesu.
Likewise,Shetani. Shetani hamvizii mtu yoyote,hamshawishi mtu yoyote. If you wany help from Satan, you must pray to Satan. Kama unataka msaada wa Shetani,lazima umuombe,umbembeleze. Hiyo ndiyo dini ya Shetani.
Waumini wa dini ya Shetani,utawatambua kwa jinsi wanavyooongea. Utawasikia mara kwa mara,"Yule mtu anajisahau sana." Yaani,yeye ndiye boss,lakini wewe unajisahau.
Ndio sala yao kila siku,."Shetani,wewe ndiyo
bosi,lakini siku hizi mambo hayaendi vizuri,kwa ajili hawa mapadre wako wanakusaliti. Ndio inatokea hii hali watu wanahisahau sana. Mapadre wako ni wavivu, wanasakusaliti. Mapadre wako ni wavivu na waumini wako wote wamesambaratika,wanakosa msaada. Lakini ipo siku,siku inakaribia,ambapo utaionesha hii Dunia kwamba wewe ndiye bosi."
Hii ndiyo wala yao ya kila siku jioni,na wakimkaribisha mgeni,wakisali naye hii sala,mara baada ya kuisali hii sala,kwa kuisali huu sala,anakuwa mfuasi wa Shetani.
 
Kuna sababu gani isiyo ya kitapeli, kulazimisha wanandoa wote wawili wenye mtoto mmoja tu (hawana mtegemezi mwingine) wakatwe michango ya bima ya afya kutoka kwenye mishahara yao? Au wanaadhibiwa kwa kuwa wao ni waajiriwa wa serikali?
 
Madaktari naomba niwaulize, kwani miwani sio matibabu ya macho? Kama uono wako unategemea miwani na usipovaa sio tu kwamba huoni bali unaumwa sana na kichwa, kwanini sasa NHIF wanagoma kulipia huduma ya miwani katika vifurushi vyao?

Wiki mbili hizi nimepata mitihani ya kuuguza mzazi wangu na watoto, kwa mpigo na nimekuwa nikilalamikia sana kuhusu NHIF bahati mbaya kila ninayemlalamikia ananishanga kuwa ilikuwaje nikaenda kukata bima hiyo? Yani ni kama watu wamekubali kuwa hii inatakiwa kuwa last option.

Nikiri, naongea kutoka kwenye tabaka la kati. Kwa kipindi hiki ambacho sina muajiri nikaona ni busara nikate bima binafsi. Nilipoenda NHIF niliulizia package ya juu kabisa, nikaambiwa ni TIMIZA, nikalipa 1.4m nikijua yakinikuta makubwa bima itaniokoa - ndio dhana kuu ya bima.

Mara ya kwanza naenda hospital, naambiwa ahaa, bima za makampuni tu ndio zinaweza kutumika hospital hii, bima za vifurushi lazima ukaanzie hosp ndogo umepewa rufaa ndio uje huku. Nikajiuliza kwa nini matabaka ya walioajiriwa na wasioajiriwa yanaendelezwa? wangapi wameajiriwa?

Kwanini hatumpi mtu ambaye hayuko kwenye kampuni options za kuwa na bima yenye faida kama walio kwenye makampuni? Kwanini watu binafsi wanaonekana wote ni walala hoi? Mimi nilidhani, NHIF itafaidika zaidi kama watu wengi watajiunga na mfuko na si kutegemea tu watumishi.

Nikakung'uta dira nikaenda kwenye kituo, baada kumuona daktari akaniomba niende kwa dr mwengine specialist, nikaamua kumsubiri mana alikaribia kuanza clinic yake, nikaambiwa bima inalipa 1 consultation kwa siku hivyo nije kesho. Nikaona hizo hela za wese na time bora nilipe tu.

Mara Bi mkubwa akaumwa, nae ana bima yake ya kifurushi, tukaambiwa tulipie MRI na baadae operation, nikauliza NHIF inatusaidiaje, naambiwa inalipa kitanda, dawa na kumuona dr? I was like seriously? kwanini bima wanachukua majukumu madogo makubwa wanamuachia mgonjwa?

Wakati bado napambana na bi mkubwa yuko wodini, bint karudishwa kutoka shule hoi. Dr kaandika kipimo, nikaambiwa nilipe cash kwa kuwa ni gharama na hakiko kwenye bima, chozi lilinidondoka. Nikajikung'uta nikalipa mtoto akapata matibabu.

Tumeenda kwenye macho, tunaambiwa hapa unalipiwa tu kumuona Dr ila miwani hakuna. Nikamuuliza Dr kwa hiyo kwa taaluma yako hapa tunywe dawa gani ili tuone vizuri? kati yenu na NHIF nani anatakiwa aseme macho yangu yanatibiwaje? Nikaambiwa huduma hiyo inapatikana kwa kampuni.

Anyways to make long story short, NHIF naweza kurudishiwa tushilingi kwangu kaliko baki nikamnunulie kijana miwani? kama huduma zenyewe naishia kuingia mfukoni hiyo chenji itanisaidia sana. Pili natamani viongozi wawe wanajaribu kutumia hizi huduma ili wajue ufanisi wake.

Tatu, bado naamini kuna potential kubwa kwa NHIF kutoa universal coverage kwa watanzania, ila kwanza muondoe hili tabaka la watumishi/kampuni na binafsi. Muwe na huduma kwa segment mbalimbali, kama mtu binafsi anaweza kuafford the best cover, let it be.

Hii dhana ya kama una hela kanunue bima kwenye kampuni binafsi haisaidii sana, mana ili mfuko uimarike mnahitaji watu wengi wachangie, na ili watu wachangie inabidi wapate huduma stahiki, kwa ubora. Sio una bima unaanza kwenda kukopa. Haisadii mchangiaji wala mfuko wenyewe.

Ukweli ni kwamba watanzania sisi wa tabaka hili wengi tunatibiwa na wafamasia, unajisikia ndivyo sivyo unaibuka phamacy unapewa dawa siku inaenda sasa kama coverage ni kumuona Daktari na dawa mnakuwa hamjasaidia sana. Ni vizuri mkafanya tena ethnographic study ya kundi hili letu.

Mwisho mkiona hayo yote hayafai, basi anzisheni bima za viungo, kama bima ya macho miguu, mgongo, kichwa, nk ili niwe na uhakiki kuwa kiungo changu hiki kikipata mushkeli kitatibiwa in full. Tutaongea na viungo vingine visiume na magonjwa ambayo hayako kwenye coverage yasije.
@Wizara ya Afya
 
Kiufupi kama unajali familia yako hyo 1.4m ungeiweka kwenye hifadhi yako binafsi ukawa unatumia kulingana na huduma uitakayo. Mm sikati bima hata siku moja kwakua najua hakuna hospitali inayokataa cash ikalazimisha uwe na bima kwahyo uamuzi ni wako kulingana na ustaarabu wako wa matumizi.
Unaropoka tu ila siku yakikukuta ndo utaelewa umuhimu wake
 
Mimi sijawahi kuelewa hii logic hasa kwa bima ya NHIF, majuzi nimeenda kufanya vipimo, tena Hospital kubwa ya serikali, nikaambiwa kipimo cha homa ya ini, ambacho ni sh 30,000 hakipo kwenye bima, ila vipimo vingine mpaka vya sh 125,000 vipo kwenye bima!!
Magonjwa ya Moyo, Kansa, Ini, Figo bima wamejitoa
 
Mi naona bora waweke na vifurushi vya exwcutive ili wanaoweza walipie
 
Unaropoka tu ila siku yakikukuta ndo utaelewa umuhimu wake
Hebu tusiandikie mate jamaa katoa 1.4m na yamemkuta kaingia tena mfukoni haya hayo ambayo yatanikuta mm nisiekata bima ni yapi wakati waliokata yanawakuta na 1.4m sio bima ndogo kwa usawa wa mtanzania. Muda mwingine usiwe muoga sana wa maisha na nimesema kama ustaarabu wako wa pesa ni mzuri bora uweke hiyo hela kwenye ac utumie pale unapopata majanga. Bima kwa bongo ni utapeli fulani ukiona watu zaidi ya 10 wanalalamikia bima inamaana wote wanaonewa mfumo wa bima ni wakitapeli tu
 
Ukiwa na bima ya NHIF ya mwajiri huduma hizo unazipata.

Ila kama una bima ya NHIF ya vifurushi huduma hizo huzipati
Sasa mfano bima ya muajiri gharama yake ni 800k na bima binafsi nimekata 1.4m kama jamaa iweje nikose huduma wakati nimeweka mpunga mrefu zaidi ya wale wa muajiri ukiskia upigaji ndio mambo kama haya. Ajira zenyewe chenga alafu kipaumbele wakapewe walioajiriwa hili kundi la wataftaji binafsi wakatibiwe na bima ipi sasa
 
Sasa mfano bima ya muajiri gharama yake ni 800k na bima binafsi nimekata 1.4m kama jamaa iweje nikose huduma wakati nimeweka mpunga mrefu zaidi ya wale wa muajiri ukiskia upigaji ndio mambo kama haya. Ajira zenyewe chenga alafu kipaumbele wakapewe walioajiriwa hili kundi la wataftaji binafsi wakatibiwe na bima ipi sasa

Mfuko wa bima unaeendeshwa kwa mfumo wa pool la kuchangiana.

Miaka ya nyuma NHIF waliweka pool moja lenye michango ya waajiriwa wanaokatwa kila mwezi na watu walio nje ya ajira ambao wanalipia bima binafsi kila mwaka.

Mbeleni NHIF wakagundua watu wanaokata bima binafsi asilimia kubwa ni wagonjwa tofauti na waajiriwa wao wanalipia bima kwa kulazimishwa na waajiri wao kwa kukatwa hivyo wengi waajiriwa ni wazima ki afya. Hivyo hawatumii pesa za mfuko sana tofauti na watu binafsi wakiwa wazima hawakati bima wakianza kuumwa ndio wanakata bima na kuanza kufilisi mfuko kwa kutumia kingi kuliko walichochangia.


NHIF imeweka pool mbili sasa.. watu wenye bima binafsi kapu lao peke yao.

Na watu waajiriwa wanaokatwa kwenye mishahara yao kapu lao peke yao


Kwenye haya makapu wamegundua kapu la watu binafsi lina matumizi makubwa kuliko michango wanayochangia. Hivyo wamewakatalia magonjwa makubwa yote maana kapu lao lina pesa kiasi kidogo halimudu kuwatibia hayo magonjwa.


Waajiriwa wao kapu lao ni kubwa lina mapesa mengi yanaingia kila mwezi huku wanaooumwa ni wachache sana hivyo kapu lao halifilisiki. Ndio maana wamewaruhusu watibiwe mpaka magonjwa makubwa

NHIF WANAAMINI KAMA MTU BINAFSI UNAONA BIMA YA NHIF INAKUNYONYA HELA ZAKO UNAZOLIPIA KILA MWAKA. ACHANA NA NHIF NENDA KAKATE BIMA YA KAMPUNI ZINGINE MAANA HAWAKULAZIMISHI
 
Back
Top Bottom