Darkhorse001
JF-Expert Member
- Dec 19, 2020
- 306
- 538
[emoji16][emoji16]Wao wanajipa bima za tofauti wanaweza kutibiwa magonjwa makubwa na mahospitali makubwa yenye gharama. Ndio wao wanafilisi mfuko
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji16][emoji16]Wao wanajipa bima za tofauti wanaweza kutibiwa magonjwa makubwa na mahospitali makubwa yenye gharama. Ndio wao wanafilisi mfuko
@Wizara ya AfyaMadaktari naomba niwaulize, kwani miwani sio matibabu ya macho? Kama uono wako unategemea miwani na usipovaa sio tu kwamba huoni bali unaumwa sana na kichwa, kwanini sasa NHIF wanagoma kulipia huduma ya miwani katika vifurushi vyao?
Wiki mbili hizi nimepata mitihani ya kuuguza mzazi wangu na watoto, kwa mpigo na nimekuwa nikilalamikia sana kuhusu NHIF bahati mbaya kila ninayemlalamikia ananishanga kuwa ilikuwaje nikaenda kukata bima hiyo? Yani ni kama watu wamekubali kuwa hii inatakiwa kuwa last option.
Nikiri, naongea kutoka kwenye tabaka la kati. Kwa kipindi hiki ambacho sina muajiri nikaona ni busara nikate bima binafsi. Nilipoenda NHIF niliulizia package ya juu kabisa, nikaambiwa ni TIMIZA, nikalipa 1.4m nikijua yakinikuta makubwa bima itaniokoa - ndio dhana kuu ya bima.
Mara ya kwanza naenda hospital, naambiwa ahaa, bima za makampuni tu ndio zinaweza kutumika hospital hii, bima za vifurushi lazima ukaanzie hosp ndogo umepewa rufaa ndio uje huku. Nikajiuliza kwa nini matabaka ya walioajiriwa na wasioajiriwa yanaendelezwa? wangapi wameajiriwa?
Kwanini hatumpi mtu ambaye hayuko kwenye kampuni options za kuwa na bima yenye faida kama walio kwenye makampuni? Kwanini watu binafsi wanaonekana wote ni walala hoi? Mimi nilidhani, NHIF itafaidika zaidi kama watu wengi watajiunga na mfuko na si kutegemea tu watumishi.
Nikakung'uta dira nikaenda kwenye kituo, baada kumuona daktari akaniomba niende kwa dr mwengine specialist, nikaamua kumsubiri mana alikaribia kuanza clinic yake, nikaambiwa bima inalipa 1 consultation kwa siku hivyo nije kesho. Nikaona hizo hela za wese na time bora nilipe tu.
Mara Bi mkubwa akaumwa, nae ana bima yake ya kifurushi, tukaambiwa tulipie MRI na baadae operation, nikauliza NHIF inatusaidiaje, naambiwa inalipa kitanda, dawa na kumuona dr? I was like seriously? kwanini bima wanachukua majukumu madogo makubwa wanamuachia mgonjwa?
Wakati bado napambana na bi mkubwa yuko wodini, bint karudishwa kutoka shule hoi. Dr kaandika kipimo, nikaambiwa nilipe cash kwa kuwa ni gharama na hakiko kwenye bima, chozi lilinidondoka. Nikajikung'uta nikalipa mtoto akapata matibabu.
Tumeenda kwenye macho, tunaambiwa hapa unalipiwa tu kumuona Dr ila miwani hakuna. Nikamuuliza Dr kwa hiyo kwa taaluma yako hapa tunywe dawa gani ili tuone vizuri? kati yenu na NHIF nani anatakiwa aseme macho yangu yanatibiwaje? Nikaambiwa huduma hiyo inapatikana kwa kampuni.
Anyways to make long story short, NHIF naweza kurudishiwa tushilingi kwangu kaliko baki nikamnunulie kijana miwani? kama huduma zenyewe naishia kuingia mfukoni hiyo chenji itanisaidia sana. Pili natamani viongozi wawe wanajaribu kutumia hizi huduma ili wajue ufanisi wake.
Tatu, bado naamini kuna potential kubwa kwa NHIF kutoa universal coverage kwa watanzania, ila kwanza muondoe hili tabaka la watumishi/kampuni na binafsi. Muwe na huduma kwa segment mbalimbali, kama mtu binafsi anaweza kuafford the best cover, let it be.
Hii dhana ya kama una hela kanunue bima kwenye kampuni binafsi haisaidii sana, mana ili mfuko uimarike mnahitaji watu wengi wachangie, na ili watu wachangie inabidi wapate huduma stahiki, kwa ubora. Sio una bima unaanza kwenda kukopa. Haisadii mchangiaji wala mfuko wenyewe.
Ukweli ni kwamba watanzania sisi wa tabaka hili wengi tunatibiwa na wafamasia, unajisikia ndivyo sivyo unaibuka phamacy unapewa dawa siku inaenda sasa kama coverage ni kumuona Daktari na dawa mnakuwa hamjasaidia sana. Ni vizuri mkafanya tena ethnographic study ya kundi hili letu.
Mwisho mkiona hayo yote hayafai, basi anzisheni bima za viungo, kama bima ya macho miguu, mgongo, kichwa, nk ili niwe na uhakiki kuwa kiungo changu hiki kikipata mushkeli kitatibiwa in full. Tutaongea na viungo vingine visiume na magonjwa ambayo hayako kwenye coverage yasije.
Unaropoka tu ila siku yakikukuta ndo utaelewa umuhimu wakeKiufupi kama unajali familia yako hyo 1.4m ungeiweka kwenye hifadhi yako binafsi ukawa unatumia kulingana na huduma uitakayo. Mm sikati bima hata siku moja kwakua najua hakuna hospitali inayokataa cash ikalazimisha uwe na bima kwahyo uamuzi ni wako kulingana na ustaarabu wako wa matumizi.
Magonjwa ya Moyo, Kansa, Ini, Figo bima wamejitoaMimi sijawahi kuelewa hii logic hasa kwa bima ya NHIF, majuzi nimeenda kufanya vipimo, tena Hospital kubwa ya serikali, nikaambiwa kipimo cha homa ya ini, ambacho ni sh 30,000 hakipo kwenye bima, ila vipimo vingine mpaka vya sh 125,000 vipo kwenye bima!!
Magonjwa ya Moyo, Kansa, Ini, Figo bima wamejitoa
Hebu tusiandikie mate jamaa katoa 1.4m na yamemkuta kaingia tena mfukoni haya hayo ambayo yatanikuta mm nisiekata bima ni yapi wakati waliokata yanawakuta na 1.4m sio bima ndogo kwa usawa wa mtanzania. Muda mwingine usiwe muoga sana wa maisha na nimesema kama ustaarabu wako wa pesa ni mzuri bora uweke hiyo hela kwenye ac utumie pale unapopata majanga. Bima kwa bongo ni utapeli fulani ukiona watu zaidi ya 10 wanalalamikia bima inamaana wote wanaonewa mfumo wa bima ni wakitapeli tuUnaropoka tu ila siku yakikukuta ndo utaelewa umuhimu wake
Sasa mfano bima ya muajiri gharama yake ni 800k na bima binafsi nimekata 1.4m kama jamaa iweje nikose huduma wakati nimeweka mpunga mrefu zaidi ya wale wa muajiri ukiskia upigaji ndio mambo kama haya. Ajira zenyewe chenga alafu kipaumbele wakapewe walioajiriwa hili kundi la wataftaji binafsi wakatibiwe na bima ipi sasaUkiwa na bima ya NHIF ya mwajiri huduma hizo unazipata.
Ila kama una bima ya NHIF ya vifurushi huduma hizo huzipati
Sasa mfano bima ya muajiri gharama yake ni 800k na bima binafsi nimekata 1.4m kama jamaa iweje nikose huduma wakati nimeweka mpunga mrefu zaidi ya wale wa muajiri ukiskia upigaji ndio mambo kama haya. Ajira zenyewe chenga alafu kipaumbele wakapewe walioajiriwa hili kundi la wataftaji binafsi wakatibiwe na bima ipi sasa