Ni kawaida kampuni kuzaliwa, kuishi na kufa katika ulimwengu wa biashara hivyo Tigo ni sehemu ya hayo automatically.
Ninachojiuliza ni kweli kuwa kampuni ya Tigo imekubali Kufa kirahisi hivyo baada ya jitihada Zooote za kukupambana sokoni.
Bila shaka Tigo wanajua jinsi kampuni zao nyingine Africa zilivyoshindwa kufanya vizuri isipokuwa ya Tanzania imekuwa tofauti. Hapa Kuna watu wa masoko wanastahili pongezi kubwa. Mfano ni kina Kelvin Twisa, hongera kwao maana walifanya kazi nzuri kipindi chao.
Nije kwenye suala la msingi la kwa nini Tigo inaenda kufa:
Kwanza ieleweke, mpaka kufikia maamuzi ya kubadili vifurushi mchakato huo utakuwa na sababu zilizokubalika na menejimenti na kwa kuwa wao ni key players yawezekana wameona mbali na wana taarifa za kutosha.
Pamoja na hayo, haituzuii kutoa maoni yetu.
Sasa basi kwa maoni yangu kitendo cha Tigo kubadili vifurushi vyao itasababisha wateja wao wakimbie.
Tigo itakimbiwa na wateja sababu ya msingi wa ukuaji wake ulijengwa kwa vijana hasa wanafunzi na watu wenye kipato kidogo ambao kimsingi ni wengi. Ilifikia kipindi karibu wanafunzi 'wote' ama wengi wana laini za tigo. Hapo ndipo likatokea Jina kuwa ni mtandao wa wanafunzi. Wanafunzi hao walipomaliza waliendelea na sasa wapo vijana wa kutosha ni watumiaji wa mtandao huu.
Shida kubwa ni msingi uliotumika kuikuza tigo na kushikilia wateja wake ambao ni vijana kwa kuwapa ofa kubwa za muda wa maongezi na internet. Sasa unapoondoa vitu hivi vijana hawa ni rahisi kuhama na kuhamia mitandao mingine yenye huduma nafuu kwa sababu wanazo alternatives.
Vijana ni risk takers, hawana vya kupoteza wanapohama hama. Ni tofauti na wazee ama watu wa umri wa kati.
Yawezekana mnawaiga Voda ila angalieni wao wamepandisha vifurushi vyao lakini hausikii kelele mitandaoni sababu ni aina ya wateja ambao Voda waliwachagua na utamaduni walioweka tangu mwanzo.
Tigo nawaambia hivi wateja wenu hawa vijana wanawahama sababu ni kuwa wakati nyie mnawabana kuna mitandao imewafungulia milango.
Ikiwa lengo lenu ni kuua kampuni ama kuuza kwa mtu mwingine basi sawa. Ila kama mnataka kuendelea fanyeni utafiti vizuri muwajue wateja wenu.