Malalamiko ya Dulla Mbabe na Ibra Class kwa kupoteza pambano dhidi ya Katompa ni sawa na mfa maji

Malalamiko ya Dulla Mbabe na Ibra Class kwa kupoteza pambano dhidi ya Katompa ni sawa na mfa maji

Nawaza TU mfano angebebwa na akatangazwa mshindi vipi angefurahi na kuruka ruka[emoji848][emoji848][emoji848][emoji23][emoji23][emoji23]!?
Anyway hii kada Yao inasumbuliwa na suala la elimu hata ya ku reason kawaida tu kuwa Nini uongee na Nini usiongee
Hivi hata kina Matumla nao walikuwa wanaongea utumbo hadharani? Mimi nilidhani ni Mwakinyo tu ndio hupuyanga kwenye media, kumbe wapo na wengine!
 
Mimi hili pambano nimeanza kuliangalia round ya 6 kiukweli mpaka niluanza kuona aibu namna Dulla anavyolicheza pambano. Hizi fani zinavamiwa na watu wa ajabu ndio matokeo yake haya. Kuna mazingira hata ukibebwa haina shida ila kwa uchezaji ule ni aibu kubwa kwa tasnia ya ngumi. Inawezekana kwa sababu wanabebwa ndio maana hawajitumi, hawafanyi mazoezi na kadhalika.
 
Nimeskitika sn Dulla na Ibra Classic kulalamikia chama Cha ngumi Tanzania eti Dulla alikuwa ameshinda.

Kibaya zaidi Ibra Classic anaongea bila aibu eti majaji wameshindwa kumbeba Dulla kwa sababu hata wao wanapoenda Ulaya huwapiga wazungu lakini majaji huwabeba wazungu wenzao.

Professionally, hii siyo kauli nzuri, yani ubebwe kisa wewe uko nyumbani kwenu wakati ngumi zinaoneshwa LIVE na ulimwengu unaona!! Au wanataka chama Cha ngumi Tanzania kifungiwe kwa kuboronga ktk maamuzi. Au wanataka mabondia kutoka nje wasije Tanzania kwa kuogopa wenyeji kubebwa.

Sasa huko Ulaya mnakosema huwa mnaonewa ni Mtanzania gani huwa anawaona mkionewa, isije kuwa ni janja janja zenu tu Wabongo maana ndo maisha yenu mlishazoea. Mara utaskia "mabegi yamepotelea airport, mara viatu nilipewa over zise" Nonsense. Na isitoshe kosa moja haliwezi kuhalalisha makosa mengine yaendelee. Km hamtaki kucheza ngumi hameni nchi muaachie wanapoenda haki wapigane.

Nimalizie tu kwa kusema Watanzania wengi wamezoea maisha ya ujanja ujanja sana, ku fake maisha na undugu-naization ndo maan nchi haisongi mbele. Ebu Dulla na kampani yake waache maisha ya ujanja ujanja waende kwenye uhalisia. Mchezo wa ngumi ni mchezo wa wazi kila mtu anaona.

NB: Naomba chama Cha ngumi Tanzania kimfungie Dulla na Ibra Classic au wapewe adhabu kali kwa kutoa shutuma kali dhidi yenu mbele ya kadamnasi tena mbele ya kamera za AZAM TV ili liwe fundisho kwa wale wasiojua mchezo wa ngumi ila wanalazimisha kujua ngumi kwa sababu ya njaa.

BANDOKITITA nimemaliza.
Namshukuru sana Mungu kwa kuniumba Mtanzania,na naipenda Tanzania na watu wake.Dullah mbabe ulipigwa kama unapiga.Huo ndio ukweli na msijidhalilishe Tena kwenye kadamnasi,nenda kajikande maumivu.
 
Dulah mbabe wala sio bondia wa kumtafutia mapambano nje ya nchi anapigana sababu ya njaa tu lkn ameshuka sn kimedani ndio maana mara kwa mara anaomba pambano na anaishia kubondwa tu.

Dula ajikite kupiga ngoma za mchiriku au kama kuna mashamba kwao ajikite kwenye kilimo lkn ngumi zimeshamshinda....

Na akiendekeza njaa atakuja kufia uliongoni

Asijekusema hajaambiawa, shauri yake.
 
Mimi hili pambano nimeanza kuliangalia round ya 6 kiukweli mpaka niluanza kuona aibu namna Dulla anavyolicheza pambano. Hizi fani zinavamiwa na watu wa ajabu ndio matokeo yake haya. Kuna mazingira hata ukibebwa haina shida ila kwa uchezaji ule ni aibu kubwa kwa tasnia ya ngumi. Inawezekana kwa sababu wanabebwa ndio maana hawajitumi, hawafanyi mazoezi na kadhalika.
Anamkumbatia katompa kama vile anaitaka cha2!
 
Dulah mbabe wala sio bondia wa kumtafutia mapambano nje ya nchi anapigana sababu ya njaa tu lkn ameshuka sn kimedani ndio maana mara kwa mara anaomba pambano na anaishia kubondwa tu.

Dula ajikite kupiga ngoma za mchiriku au kama kuna mashamba kwao ajikite kwenye kilimo lkn ngumi zimeshamshinda....

Na akiendekeza njaa atakuja kufia uliongoni

Asijekusema hajaambiawa, shauri yake.
Bora anayejifariji kwa kauli mbiu ya"Kupigwa kama umepiga na kupiga kama umepigwa.
 
Mimi hili pambano nimeanza kuliangalia round ya 6 kiukweli mpaka niluanza kuona aibu namna Dulla anavyolicheza pambano. Hizi fani zinavamiwa na watu wa ajabu ndio matokeo yake haya. Kuna mazingira hata ukibebwa haina shida ila kwa uchezaji ule ni aibu kubwa kwa tasnia ya ngumi. Inawezekana kwa sababu wanabebwa ndio maana hawajitumi, hawafanyi mazoezi na kadhalika.
Dulla pombe na bangi nyingi akiwa maskani kwao na masela wenzake ndo maana hata pumzi hana yaani round ya 4 tuuh upepo umekata
 
Bondia gani hana nidhamu na professional yake!! pombe yeye sigara yeye anategemea nini zaidi kichapo.?
 
Back
Top Bottom