Nimewahi kuandika humu jf kuhusu mabondia wa Tanzania kubebwa , nikatoa mifano hai kabisa , lakini nikabezwa , yuko bondia mwingine alipigwa ngumi na Katompa akachanika , Pambano likavunjwa kwa madai ya uongo kwamba Katompa alipiga kichwa .
Siri hii na nyingine bwana Dulla anaijua , yawezekana ilipangwa mpango kama huu leo lakini akageukwa baada ya kuzidiwa mwanzo mwisho ( huwezi kubeba gunia la misumali )
Dulla akijua kachakazwa lakini bado akataka abebwe kama wanavyobebwa wenzake , hii ni aibu kwa familia ya ngumi .
Bado kidogo siri zote za uchafu wanaofanya zitafichuka zaidi .